UKAWA sasa hivi wameunganisha makundi yao ili kuendesha harakati za kuivuruga serikali isijikite kwenye maswala yake muhimu.Makundi yanayotumika ni yale yaliyotumika kipindi cha kampeni.Ukifuatilia siku za karibuni utagundua kuwa yale makundi yametoka makaburini kuanza uanaharakati kwa pamoja.Inaelekea walikaa wakakubaliana wakasema moja,mbili,tatu anza .
Makundi haya ni
1.Wabunge wa UKAWA kuendesha harakati za upinzani bungeni
2.Vyama vya upinzani kuanza harakati mfano CHADEMA kuzunguka nchi nzima kwa mikutano na maandamano
3.ACT wazalendo na Zitto kabwe kuwa kwenye mambo ya kipinzani kwa nguvu kubwa nk
4.Kupitia KIGODA cha mwalimu watu kama akina Ulimwengu nk kulipuka mambo ya kipinzani
5.Akina Kijo Bisimba kuibuka na kuanza kushambulia
6.JUKATA ambalo ni jukwaa la katiba la akina Deus KIBAMBA kuanza porojo za kudai katiba
7.Akina Gwajima KUIBUKA na kuanza kushambulia huku na kule
8.Akina LOWASA na SUMAYE kuanza kukutana na wanafunzi wa vyuo vikuu wa CHADEMA na kufanya mikutano nao nk nk
9.Maalim Seif kutimukia Marekani kwa kile kinachoiitwa kuhusiana na Zanzibar!!!!! nk nk
Ukiyaangalia matukio yote na timing yake unaona kuwa ni mpango uliosukwa na kuratibiwa kwa nia ya kuivuruga serikali katika kona tofauti tofauti.
Lakini Kila silaha itakayoshindana na serikali ya Magufuli haitafanikiwa