Uchaguzi 2020 Ukara: Wananchi wamuua mtu aliyetaka kumteka mgombea udiwani wa kata ya Bwisya kwa tiketi ya CHADEMA

Mtu mmoja ameuawa asubuhi hii na wengine wawili kufanikiwa kutoroka baada ya kujaribu kumteka mgombea udiwani wa kata ya Bwisha Ukara kwa tiketi ya CHADEMA.

Inadaiwa watu hao wamezingirwa baada ya mgombea huyo kupiga ukunga na ndipo walipozingirwa na kushushiwa kipigo ambapo mmoja ameuawa huku wawili wakifanikiwa kutoroka.

Hilo ni tukio la kwanza la mauaji yanayohusishwa na mambo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ambapo kunatabiriwa kuwepo kwa visa vingi vya vurugu kutokana na sintofahamu ambazo zimeanza kujitokeza.

Habari hii imethibitishwa na Katibu wa kanda ya Victoria- CHADEMA ndugu Zacharia T. Obad
Ukiona hilo, ni kwa sababu leo angeshindwa kurudisha fomu akiwa mateka. CCM wamelikoroga wao wenyewe kwa kuleta majina yasiyokubalika na sasa wanaona ugumu wa kuwatetea majukwaani.
 
Hii roho mbaya ya kutekana inaonekana kushamiri. Kama waliweza kumthibiti wasingemua ili tujue ni akina nani waliowatuma.....
Polisi wangemchukua na kumficha kisha kumuachia. Safi sana wakara huwa nawaaminia sana. Nyerere pia alikuwa na historia yao kwa upande wa 'mambo ya jadi'
 
Huwajui hawa binaadamu wewe
Mkuu Kiukweli ni mjinga tu ndio ataamini kuwa haya matukio yanaratibiwa na ccm, yaani wafanye huu utekaji na uuaji kwa makusudi kabisa huku wakijua kabisa lawama zitatupwa kwao na kuwapaka matope tena kwenye kipindi hiki cha uchaguzi?
Basi kama ni hivo watakuwa wapumbavu kweli kweli.
 
Wale wa Hai - Kilimanjaro waliorusha mawe ni chama gani ?
Hapa ndio upate majibu kuwa Ccm inahusika katika haya matukio na ndio wanaratibu 100%
Ndio mana nikasema kuwa kama ni kweli wao ndio wanaratibu hayo basi watakuwa ni wapumbavu wa kiwango Cha lami.
Yaani uende kujianika kabisa kurusha mawe kwenye msafara wa kiongozi wa upinzani huku ukiwa umevaa nguo za chama chako? Una akili kweli kichwani kweli hapo? Mi siamini Kama ni wajinga kiasi hiki mkuu.

Yaani wachome ofisi ya CHADEMA Arusha na tuhuma, lawama na zingo lote la ubaya kutupwa kwao kisha eti kabla ya watu hawajasahau kilicho tokea huku kila Kona wakisemwa vitaya eti wanakwenda kuchoma ofisi nyingine ya CHADEMA Mbeya? hata Kama akili huna kabisa lakini huwezi kufanya vitu vya namna hiyo, siamini kabisa kama ni wajinga wa kiwango hiki mkuu.
 
mfano kama huo ufanywe hata kwa mkurugenzi mmoja tu ili wengine wajifunze, mambo gani ya kihuni hayo wanaleta.
 
Mkuu Kiukweli ni mjinga tu ndio ataamini kuwa haya matukio yanaratibiwa na ccm, yaani wafanye huu utekaji na uuaji kwa makusudi kabisa huku wakijua kabisa lawama zitatupwa kwao na kuwapaka matope tena kwenye kipindi hiki cha uchaguzi?
Basi kama ni hivo watakuwa wapumbavu kweli kweli.
Wanaoamini usiwaite wajinga, ila wewe usiyeamini ndo tunajiuliza ni mtu wa aina gani. Uliuona umati uliojitokeza kutaka uongozi ndani ya CCM? umeshuhudia pesa iliyotumika na kiwango? Baadaye jiulize uelewa wa viongozi wa CCM.

Miaka 43 tangu CCM kuundwa na miaka 66 tangu TANU, bado ni chama chenye wenyeviti wa mikoa na wilaya darasa la 7. Hawana ajira nyengine na hawana kipato kingine zaidi ya kuitegemea siasa. Mtu wa aina hiyo atapanga mbinu gani za kisiasa?
 
Unapoteza maisha kwa sababu ya someone else's bread, akishakuwa diwani huoni hata hela yake...sad
 
Mauwaji ya MKIRU yalikua ya tofauti sana sana na ndio maana jeshi liliingilia kati, huenda ilikua ni zaidi ya yale tuliyokua yunayajua, all in all tupendsne na kuheshimiana maana chaguzi zitapita ila maisha yatakuepo
Sasa Kama kule kibiti walifanya watu wengine wabaya ndio maana jeshi likaingilia swali je kwanini walikuwa wanaua Wana CCM pekee na polisi?

Huoni kuwa watu Kama hao inawezekana wakatumia kipindi hiki cha uchaguzi kufanya matukio ya hovyo Kama haya ili kutuvuruga?

Mimi nimeuliza hivyo ili tu upate picha kuwa katika kipindi kama hiki Cha uchaguzi sio rahisi kwa chama fulani kuanza kufanya mauaji ya hovyo hovyo kiasi hicho tena mbele za watu kabisa wakati wakijua kabisa yataharibu Imani ya wapiga kura kwa chama chao, hili haliwezekani mkuu hata Kama ungekuwa wewe usingekuja na mbinu ya kijinga kiasi hiki.
 
Mungu atuepushie huu ujinga, Tanzania ni nchi ya amani na naomba usiku na mchana amani, upendo , kuheshimiana kubaki kama mojawapo ya tunu zetu
Tunu ya kwanza ni haki. Taifa likipada mti wa haki litavuna tunda la amani! Kinachotokea sasa ni ushahidi tosha wa jinsi kusivyo na haki Tz. Bila haki hakuna Demokrasia. Lakini Mhe. Bashiru alisema wazi kweupe kuwa ccm kitatumia vyombo vya dola kubaki madarakani. Sitashangaa vurugu na mauaji zaidi kwa sababu waTz wachotaka ni haki. Hivi kuna mgombea kule Tunduma yupo ndani kwa kubambikiwa kosa la ujambazi wa kutumia silaha. Alikamatwa ili kuchunguzwa uraia lakini kufikishwa polisi kosa likabambikwa lingine, na polisi. Hii ndio maana ya kutumia vyombo vya dola kubaki madarakani.
 
CCM siyo chama cha siasa tena bali ni genge la wahuni

Tangu lini genge la wahuni likawa na weledi na busara zaidi ya uhuni tu ??
Hebu jaribu kufikiri mara mbali mkuu kuna kitu hapa hakiko sawa.

Ila Kama utaweka mbele siasa zaidi basi sawa utakuwa sahihi kwa upande wako, najua hata hao wanao fanya matukio ya hivi wanalenga kutujengea Imani fulani ambayo ukiweka tu siasa mbele bila kufikiri nje ya box lazima tu utaingia kwenye mtego wao.
Ni wajanja sana hawa jamaa na Kama wakiendelea na mbinu hii na vyombo vya usalama visipo washitukia mapema na hii mihemko ya kisiasa tulio nayo basi lazima tu watafanikiwa kutuvuruga vibaya sana.
 
Back
Top Bottom