Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Wanaforum,

Wakati tunajadili suala la TRA hebu tuangalie profile za "wanene" wake, can we deduce something in line with our discussion on "uchaganaizesheni" in TRA?

Board of Directors
Chairperson
Dr. Mrs. Marcellina M. Chijoriga
Members
Mr. Gray S. Mgonja
Mr. Khamis M. Omar
Mr. Daudi T. S. Balalli
Hon. Elisa Mollel(MP)
Hon. Estherina Kilasi(MP)
Dr. Enos S. Bukuku
Secretary
Mr. Ludovic B.S. Kandege
Source http://www.tra.go.tz/board.htm

Management Team
Mr. H. M. Kitillya Commissioner General
Mr. P. J. Luoga Deputy Commissioner General
Mr. L. B.S. Kandege Secretary to the Board and Chief Counsel
Mr. J. A. Mally Commissioner for Domestic Revenue
Ms. C. Shekidele Joint Commissioner for Domestic Revenue
Mr. G. P .E. Lauwo Commissioner for Customs and Excise
Mr. L. B. Mwaseba Commissioner for Tax Investigation
Mr. P. N. Kassera Commissioner for Large Taxpayers
Mr. N. N. Msoffe Director for Human Resources and Administration
Mr. P. J. Mwangunga Director for Finance
Mr. K. Wakati Director for Information Systems
Mr. S. B. Mshoro Director for Internal Audit
Mr. T. K. Muganyizi Director for Research Policy and Planning
Mr. P. H. Mmanda Director for Taxpayer Services and Education
Source http://www.tra.go.tz/team.htm
 
Mzee Mlowezi,
Kwanza jibu lako la kwanza ni HAPANA!.. lakini swali linalofuata ni leading question ambayo inatafuta jibu ulilopangia!..
Ukabila hauwezi kwisha kabisa na wala ubaguzi wa aina yeyote ile hauwezi kwisha sehemu yoyote duniani kama vile tunapodai hakuna tena Ujambazi ama machafu mengineyo, haina maana kwamba hakuna kabisa. kama ndio hivyo sidhani kama kuna mtu angeweza kutoa tafsiri ya Ukabila kwa sababu hatujauona. machafu ama dhambi zozote yapo na yataendelea kuwepo maadam binadamu tumeumbwa kwa akili za kuchagua matendo mema (thawabu) na mabaya (dhambi), na ndio maana tumekuwa na sheria, mikakati na hata sera ambazo zinahimiza kufanya mazuri badala ya mabaya.

Mswahili,
Nitalifuatilia swala lako lakini hapo juu naona Mtz katupa list nzuri sana ambayo kwa uharaka nawaona baadhi ya watu nawafahamu hawana asili wala hawajawahi kuishi Moshi.
Mshikaji hata mtu kuishi Moshi umekuwa mchagga na kama sii mchagga basi Ukristu unamwondoa mtu ktk kundi la watihaniwa!...Yes wewe mkali bob!
 
Mtz.
Human resource & adminstration yupo mtu wa kilimanjaro hapo ajira haendi kwingine. halafu fuatilia watendaji wa chini ya hawa policy makers.

fuatilia RRO/MANAGERS, fuatilia officers in charges wa long room(Dar),na boarders, then utapata jibu vipi kilimanjaro walivyothibiti idara hii nyeti.

nakupa zaidi RRO wa airport alikuwa Kimaro ambaye ni mchagga,

RRO long room alikuwa sabuni nae kilimanjaro, ukienda officer in charge majahazi alikuwepo Lyimo nae mchagga akaja Mushi nae mchagga, na ukienda RRO BANDARINI alikuwepo mzee Maleko mchagga bandari iko chini yake kabla yake alikuwepo Foyi nae mchagga,RRO wharf alikuwepo Kisaka mchagga ambaye sasa ni deputy commissioner,hawa ndio watendaji wanaopitisha ushuru.

na documents zote za bandari Dar lazima zinapitia kwa head declaration officer(HDO) MR. MCHIRA huyu nae kilimanjaro,

officer in charge wa container terminal bandari dar,ni mr. steven mchagga,
officer in charge border ya Tunduma ni mr, Niko ni mchagga na ukienda border ya Namanga kuna mr. Mosi nae mchagga,

hawa ndio watendaji pitieni muone kama kuna usawa. na aliyetoa statement ya kuthibitisha ukabila(ukilimanjaro) ni MManda ambaye ni mchagga yeye alisema tusishangae TRA twende jeshini kwanza.yeye aliye huko hakupinga kama hakuna uchagga na ukilimanjaro. tizameni benki kuu nako
 
Duuuuuh!

Mswahili ndugu yangu umeasha watu!... damn..
Ebu nirudie upya kuyasoma.i
 
Yote hiyo ya Ukaskazini ni tangu Msuya, Mtei na sasa Mramba anaendeleza angalia kule walikopita..............................................Ukilijua hilo utakula nao sahani moja. Inasikitisha lakini Tutafika tu.

Si umesikia yule dada ambaye alikwenda Brussels kumpigia debe JK tayari anasubiri uwaziri .................................halafu unataka nchi iendelee, what a joke.
 
Ahsante ndugu Mkandara, kwa hiyo kufuatana na maelezo yako ukabila upo Tz. Sasa kama huu ukabila unatumiwa katika process ya kuajiri wafanya kazi mbalimbali hilo ni suala lingine. Lakini, hata hivyo naona ndugu Mswahili katoa data ambazo kwa haraka haraka zaonyesha kwamba yaweza kuwa hivyo. Kwa hiyo kwa maoni yangu la msingi hapa ni kuongelea namna yakulikabiri suala hili badala yakukanusha kwamba halipo. Ndugu zangu lazima tuelewe kwamba tunapokanusha kama tatizo fulani halipo, jambo hilo latufanya tushindwe kutafuta utatuzi wake.
 
Mkandara.

hawa ndio watendaji wanaopitisha documents zote na kufanya assessment za kodi.
akina chijoriga wao ni policy makers tu, hawawezi kuona document ya MENGI Reginald wala Ndesamburo watendaji ndio hao ma RRO ambao sasa wanaitwa managers, HDO NA Officers incharge ndio wahusika.

acha assessors na wakaguzi waliochini ya hawa mabwana hapa ndio usiseme hata tukianza kuorodhesha majina yao naamini hapatoshi ila ni Mushi, shirima,Lauwo,tesha, temba, lyimo, ndesamburo, mrema, tarimo,mramba, msuya etc.

Mkandara.

kamishina wa ushuru na forodha George Lauwo amempa kazi mdogo wake mr Lauwo yuko bandari container terminal ni form six tu hana shule yeyote lakini kapewa kitengo nyeti kisa mchagga na kaka yake kamishna na pia TRA nyumbani kwa wachagga na wapare.

mkandara hata MManda kathibitisha hilo hakubisha.

naomba fuatilia mkasa wa mr. Benny lusege aliyekuwa na masters toka UK lakini wachagga wakamchomea moto nyumba yake, na pia kuwekwa porini na kupewa kazi ambayo haifanani na elimu yake. zaidi huyu bwana alikuwa akifanya kazi kwa misingi ya kazi.

Mkandara TRA kuchafu tena kuna nuka ukabila.fuatilia wizi wa benki kuu na ikihitajika njoo kwenye rada na ndege niweke vitu.

pia kuna mikutano ya Mramba na Kittlya kuwakamua wafanyabiashara. Mramba huandaa harambee za kuchangia maendeleo ya shule na huduma za jamii za kilimanjaro anaita wafanyabiashara kama 20 in a time na pembeni anakaa Kittlya halafu kila mfanyabiashara anaombwa achangie mbele ya Kittlya kifupi ni ujambazi na uporaji unaotumika. Mramba kila mwaka ana vikao havipunguwi 20 na kila kimoja kinakuwa na wafanyabiashara wale wakubwa kabisa na kila kikao Kittlya pembeni. yaani rungu la TRA linatumika kuwakamua watu.unasimamishwa unaambiwa toa ahadi yako na unamuna kitllya mbele yako lazima ujifunge kitanzi mwenyewe.
 
Nilisahau Border Ya Holili Jimboni Kwa Mramba (fupi) Officer Incharge Ni Mr.ndupa Nae Ni Mchagga Na Hiki Kituo Cha Tra Holili Ilikuwa Kiwekwe Tanga Kwani Kina Kipimo Cha Kukagua Mizigo Toka Bandari Ya Mombasa Na Jiulize Tanga Na Kilimanjaro Wapi Karibu Na Mombasa? Na Pia Tanga Kuna Bandari Ambapo Mizigo Hiyo Inabidi Iende Kilimanjaro. Huo Ndio Ukabila Wa Tra.

Na Huyu Mr. Fupi(mramba) Hafai Senti Moja.
 
Ndugu Wakulima na Wafanyakazi wa JF,

Kwa maoni yangu naona kuwa pande zote mbili za mada hii zinasema ukweli.

(a) Walioona ukabila katika baadhi ya idara za serikali wanasema ukweli kuwa watu wanoepwa kazi kule wanatoka makabila fulani tu. Ukiacha nafasi za juu ambazo zinajazwa kwa kuteuliwa, nafasi za chini zinatolewa kwa upendeleo kufuatana na kuelewana. Kuelewana huko inawezekana kunatokana aidha na urafiki au undugu; mara nyingi undugu hutumika na hivyo wachaga wenye ndugu huko juu ndio wanaopta nafasi hizo kuliko kuliko makabila mengine. Ninakumbuka kijana mmja wa kichagga aliyemaliza B.Sc. (Edu) pale UDSM lakini hakwenda kufundisha badala yake akaajiriwa Customs pale airport. Kuna uwezekano kuwa imbalance kubwa ya kikabila katika TRA ilianzia kwenye kodi ya mapato wakati Baltazar Mwendwa alipofanyiwa maarifa fulani na mchaga mmoja (sikumbuki jina lake) na hivyo kunyanganywa madaraka; bwana huyu alihakikisha wasaidizi wake ni marafiki zake wa karibu sana ambao walihappen kuwa ni wachaga. Lengo lake lilikuwa ni kulinda masilahi yake binafsi na wala sidhani kuwa alikuwa anawazia kuwa na wachaga tu kwenye idara yake. Baada ya idara zote za kodi kuwa chini ya mamlaka moja ya TRA, wachaga na wameendelea kuwa wengi.

(b) Wanaosema kuwa hakuna ukabila nadhani wanasema kuwa siyo instutionalized ukabila kama ilivyo nchi nyingine. Nadhani si vizuri kuuita ukabila, badala yake tungesema ni upendeleo tu kwa vile ingawa kweli upendeleo huo uko skewed kwenye kabila fulani lakini ni kujuana ndiko kunakotumika bila kujali kabila la mtu. Akitokea mnyamwezi mmoja anayejuana sana na Kitilya tangu mashuleni kwao akamtaka Kitilya amsaidie mwanawe halafu kukawa na mchagga ambaye hajuani kabisa na Kitilya, ni wazi kuwa yule mnyamwezi atapata hiyo kazi iwapo anazo sifa zinazohitajika. Vile vile wanosema kuwa wachaga anapata kazi hizo kutokana na elimu yao pia wanasema ukweli. Ni kwa kesi chache sana ambapo utamkuta mchaga anafanya kazi ambayo hana utaalamu nayo, kwa mfano yule jamaa wa B.Sc (Ed) alivyopewa kazi iliyokuwa inahitaji B.Comm or equivalent.

(c) Kulinganisha ukabila wa TRA na jeshini siyo sahihi kwa vile watu wa makabila yote wanataka kazi za TRA lakini hawazipati, wakati siyo watu wengi wanaoomba kazi za jeshini na kutimiza requirements zake; badala yake ni wakulya na wahehe ndio wanoomba kazi hizo kwa wingi kuliko makabila mengine.
 
Kichuguu.
kesi ya TRA NI UKABILA KUNA MTU ALIOMBA KAZI MARA KADHAA KWA JINA LA KOMBA AKAWAHAPATI KITU.
AKABADILI JINA KWA DEED POLL NA SURNAME YAKE KUWA YA MUSHI ALIPATA KAZI BILA YA KUWA NA MTU. NINA VINGI AMBAVYO SIWEZI HATA KUZIWEKA HAPA. ILA TAMBUA TU TRA UKABILA UPO. FUATILIA KWA MAOFISA WASIO WACHAGGA AMBAVYO HAWANA HATA AMANI YA KAZI YAO.
 
mswahili,

mwaga/tapika mavitus mwanangu...............

I love this JF, wallahi!!
 
Hili suala la ukabila TRA lipo. Kuna hata mbunge mmoja alilizungumza bungeni siku za nyuma lakini akanyamazishwa. Katika siasa perception is as good as reality. Hongera Mswahili kwa kutoa data za uhakika!!
 
mswahili vipi bado hujaelewa tu kwamba TRA au taasisis yoyote makini wanahitaji elimu...wamlima wamesoma ...sasa tatizo lipo wapi...embo soma vizuri thread hii huko nyuma n kuna post nzuri ya namna mwalimu nyerere alivyoongelea ukabila...sasa kama kuna kazi ya tax collector ,requirement ni digrii ya biashara au sheria...utampa mtu aliyeishia form four ...

sasa mswahili mimi nimefanya kautafiti kadogo... TRA ..pale kuna nafasi mbalimbali za kazi kazi kuanzia utarishi ,udereva ,ulinzi,kwa kifupi zinaitwa SUPPORTING SERVICES STAFFS...hawa ndio wengi TRA na kwa kweli asilimia kubwa ni ndugu zako MSWAHILI so usilalamilke ,ukweli ni kuwa wafanyakazi wengi TRA ni hao unaowataka ...sasa tatizo ni kwenye PROFFESSIONAL STAFFS hapa wengi ni wamlima...na hapa wanataka vyeti tu...si vinginevyo...na hawa wala sio wengi ...ila ndio wanaoendesha mambo si unajua shule haiongopi...so mswahili nakushauri hata kama UMEJILIPUA na shule uliyoenda umeingia MITINI ,,,jaribu tu urudi uje uombe kazi ya UDEREVA au UMESENJA pale TRA ,hutakosa kwa sababu hiyo ndio stahili kutokana na kiwango chako cha elimu...hata kama umeishia form six na unajua kizungu kama huna vyeti bado tutakuchukulia kama LAYMAN , you are not proffessional yet hata mtu aliyeishia la saba na kufanya kozi ya ufundi VETA nakushinda ..yes yeye tutamuita FUNDI na ataajiriwa kama fundi ...
 
Mmanda atetea wingi wa Wachagga TRA

Written by Charles Mullinda
Friday, 21 July 2006

*Asema walipata elimu mapema

HATIMAYE Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa tamko dhidi ya madai ya kuwapo ukabila katika mamlaka hiyo.

Imesema madai hayo si ya kweli ingawa kuna idadi kubwa ya Wachaga wanaoshikilia nafasi nyeti katika taasisi hiyo.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa walipa kodi wa TRA, Evod Mmanda jana aliiambia Tanzania Daima ofisini kwake kuwa, wingi wa Wachaga katika taasisi hiyo unatokana na watu wa kabila hilo kuelimika mapema zaidi kuliko makabila mengine.

"Hakuna suala la ukabila TRA, haya mambo yanazushwa tu na watu kwa sababu mbalimbali, zikiwamo za chuki binafsi na wengine ni hulka yao kuzua mambo.

Kweli TRA ina watumishi wengi katika nafasi nyeti ambao ni Wachaga, lakini hili ni suala la historia, huwezi kulikwepa, kumbuka Wachanga ni kabila ambalo watu wake walipata elimu ya juu mapema kabla ya watu wa makabila mengine.

Na hapa sio TRA tu, angalia madaktari wengi hasa wa zamani kidogo ambao sasa ni mabingwa, wengi ni Wachaga, na kwa Tanzania nafasi za kazi hazitolewi kwa ukabila bali sifa za muhusika na uwezo alionao katika kuifanya kazi hiyo," alisema Mmanda.

Alisema Wachaga wengi wanapenda masomo ya biashara na ni wafanyabiashara kwa asili, hivyo sio ajabu kuwa wengi katika taasisi za fedha kwa sababu wamesoma na kubobea katika masomo hayo.
Hata hivyo, Mmanda alisema mambo yanabadilika kwa sababu historia ya Wachaga kupenda elimu sasa haipo na hata vijana wanaoajiriwa katika sekta ya fedha nchini wengi sio Wachaga.
Alisema Wachaga wanaolalamikiwa ni wale waliosoma zamani na mchango wao ni mkubwa katika mafanikio ya TRA.

"Sisemi haya kwa sababu mimi ni Mchaga, hapana, bali hata wewe fuatilia ukweli, tunao Wachaga TRA, lakini wote ‘wanafiti' katika nafasi zao, na hawa ni wale waliosoma zamani, leo vijana wa Kichaga wameishia biashara ya kuuza ndizi, wasomi ni wachache na makabila mengine ambayo yanazingatia elimu sasa yanaibuka," alisema Mmanda.

Aliwataka wanaoibua hoja hiyo kuiangalia vizuri historia ya elimu hapa nchini, inayoonyesha jinsi Mkoa wa Kilimanjaro ulivyokuwa na shule nyingi za sekondari katika miaka ya 1960 tofauti na mikoa mingine.

Alisema pamoja na kuwa na shule nyingi, jamii ya Kichaga ya wakati huo ilitilia mkazo maalumu suala la elimu kwa vijana ambao sasa ndio maofisa katika nafasi mbalimbali.

Alisema iwapo wingi wa watu wa kabila moja ndani ya taasisi yoyote nchini utachukuliwa kama kukithiri kwa ukabila katika taasisi hiyo, ya kwanza kutuhumiwa kuhusu hilo ni jeshi ambalo lina watu wengi wa Musoma.

Hii kitu niliiweka kwenye memory yangu na iliandikwa last year. Are you referring to this?

Sina hakika but I bet!
 
worm i remember that article ,and i read it too....and i went further and some human resource people there told me they employ on merits ,however they say many of professional posts wich are not that many in TRA are held by chaggas,hayas,nyakyusas,pares,maasai...just in that hiererchy...but still the remaining supporting posts are held by other fellows with less education...
 
Sishangai hili kutokana na politics za Africa na haswa Tanzania ambako watu wanakuwa BRAINWASHED kuwa hakuna UKABILA SERIKALINI lakini makabila yapo

what a bunch of lies

Nakumbuka niliwahi kusoma kwenye ippmedia.com sometimes back kuwa kuna Mbuge/Waziri aliwahi kulalama kwa kwa spika bungeni kuwa contracts nyingi za kujenga barabara zinapelekwa mikoa ya kaskazini na spika naye alimuunga mkono kuwa kuna walakini katika hilo

sikumbuki jina la huyo mbunge/waziri wala sina link ya ile article


Tatizo la ukabila serikalini lipo na tusijifanye eti sisi watanzania ni malaika kuliko hao wakenya na nchi zinginezo na ni vizuri watu wakakubali na ndio maana tunalijadili humu

Japo Mwalimu alijaribu at least in public kuliondoa hili lakini in Private hili tatizo lilikuwa likishamiri na matokeo yake nadhani yanaonekana


Hilo la kusema kuwa watu wanapewa based on merit na elimu nalo nadhani halina nguvu sana kwa sababu nchi imekuwa huru takriban miaka 40 sasa hebu tujiulize hivi mtu kusoma na kuwa na hiyo MBA inachukua miaka 40?

Sijui source ya MSWAHILI ni nini

lakini naomba UTUPE ya IKULU na WIZARA ya MIPANGO kama ulivyofanya ya TRA
 
PM

Hivi ukimuuliza mla rushwa kwamba yeye anakula rushwa atakubali? Nafikiri inabidi kuliangalia hili kwa makini bila kukurupuka kwani aisifiaye mvua imemnyea. Kweli ukabila upo na watu kupeana kazi kindugu etc. Mfano BWM alipokuwa foreign minister alimpeleka Maro kule Zimbabwe kwenye ubalozi ambaye alikuwa hana qualification hata za form six, sasa hapa unaweza kutetea kwamba watu wanaajiriwa kwa merit kweli? Na ni hivyo hivyo tu kwenye balozi zetu nyingi tu nje ya nchi huu ni mfano moja.

Mswahili ametoa majina kule TRA watu ambao kwa kweli anasema ni form six lakini kazi walizopewa ni kwa kugongeana tu Je, umefika wakati hawa wakachunguzwa? Tusidanganyane hapa kwamba hakuna wasomi katika makabila mengine huu ni uongo wapo sasa hivi watanzania wengi tu wanauwezo. Mikutano anayofanya Mramba ya kukusanya harambee ni uongo au ukweli? Pinga hizi hoja kama una data sio kuzidismiss tu. Mwalimu alionya kuhusu ukabila kama MKJJ alivyoandika lakini watu wengi wameziba masikio kama vile hawakusikia na wanaendeleza ukabila ambao ni lazima upigwe vita kama ukoma.
 
PM

Mfano BWM alipokuwa foreign minister alimpeleka Maro kule Zimbabwe kwenye ubalozi ambaye alikuwa hana qualification hata za form six, sasa hapa unaweza kutetea kwamba watu wanaajiriwa kwa merit kweli? Na ni hivyo hivyo tu kwenye balozi zetu nyingi tu nje ya nchi huu ni mfano moja.



Hili nilikuwa silijui na nashangaa wanaojua mambo ay FOREIGN humu wako kimya kuhusu hili


Mswahili ametoa majina kule TRA watu ambao kwa kweli anasema ni form six lakini kazi walizopewa ni kwa kugongeana tu Je, umefika wakati hawa wakachunguzwa? Tusidanganyane hapa kwamba hakuna wasomi katika makabila mengine huu ni uongo wapo sasa hivi watanzania wengi tu wanauwezo. Mikutano anayofanya Mramba ya kukusanya harambee ni uongo au ukweli? Pinga hizi hoja kama una data sio kuzidismiss tu. Mwalimu alionya kuhusu ukabila kama MKJJ alivyoandika lakini watu wengi wameziba masikio kama vile hawakusikia na wanaendeleza ukabila ambao ni lazima upigwe vita kama ukoma.



Kisha n=jiulize ni akina nani wanaopata Tenda kubwa kubwa za serikalini?
 
Back
Top Bottom