Ujumbe wa Edo Kumwembe

CTX

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
1,273
984
EDO KUMWEMBE

SIKU Fulani ya maisha yako. Hakutakuwa na wale walinzi kando yako. Hakutakuwa na rafiki zako kando yako. Hakutakuwa na wale washkaji zako wa mtaani kwako. Hakutakuwa na wale wapambe wako kando yako. Hata kama watakuwepo hautawaona.

Pua zako zitakuwa zimewekwa pamba ndani ya jeneza. Foleni ya watu itakuwa ikikuaga. Hautakuwa na fahamu. Ina maana atakayeshika kifua chako hatasikia mapigo yoyote. Hautajua kama anayekuaga ni rafiki yako au adui yako. Mama yako na dada zako kando ya jeneza watakuwa wakilia wakiliwazwa na rafiki zako, ndugu na jamaa zako.

Kaka zako watakuwa bize sana kuhakikisha watu wote walio msibani wanapata mahitaji yao. Mmoja atakuwa anahakikisha kila mtu amekula. Mwingine atakuwa akifarijiwa na rafiki zako wa karibu. Mwingine atakuwa kaburuni kuhakikisha kaburi lako limechimbwa vema. Mwingine atakuwa anaongea na sheikh au askofu kuhusu mpangilio mzima wa mazishi.

Kama una cheo kikubwa sana basi wakubwa waliobaki watakuwa wanapiga saluti mbele ya jeneza lako. Hata hivyo haitasaidia sana. Haitakurudishia pumzi. Kama ulikuwa mwanamuziki mahiri sana, bado haitakurudishia pumzi. Alikufa Michael Jackson na bado hajarudishwa.

Kama ulikuwa kiongozi maarufu bado haitasaidia. Alikufa Mwalimu Nyerere na bado hajarudishwa. Alikufa Nelson Mandela, alikufa Martin Luther King, alikufa JF Kennedy. Wote hawa hawajarudi tena. Kila siku tunapita kando ya makaburi yao na kuishia kusema “Walikuwa mashujaa”.

Lakini mbona hawanyanyuki chini ya udongo na kusimama?. Kumbe hawakuwahi kuwa wakubwa kuliko wewe. Kuna mkubwa mmoja tu ambaye hapigiwi saluti lakini anabakia kuwa mkubwa. Anaitwa Mungu. Kwanini uringe sana hapa duniani? Ni swali linaloendelea kushangaza sana. Wakati mwingine maisha yanashangaza sana. Sana. Sana. Kuliko tunavyofikiri.

Wakati tukikaribia kukuaga, mtu ambaye ataendelea kuheshimika kwa muda tu, ndani ya siku hiyo, atakuwa MC wa shughuli hiyo. Hautaweza kumpinga. Yeye ndiye ambaye atatuambia muda gani ‘utabebwa’ kwenda eneo moja kwenda jingine.

Yeye ndiye ambaye atatuambia muda wa maziko, muda wa kula, muda wa kwenda makaburini. Yeye ndiye ambaye kwa mbwembwe atatuambia matanga au Arobaini yatakuwa lini.

Leo utakuwa na mbwembwe nyingi katika kundi la mashabiki wa muziki wako wanaokuhusudu. Leo utakuwa na mbwembwe nyingi kwa walinzi wanaokulinda na silaha. Leo utakuwa katika baa Fulani ya sehemu Fulani ukitoa kila amri ambayo wanyonge wanatekeleza bila ya kuguna. Unalipa bili unaondoka. Lakini duniani kuna mkubwa mmoja tu.

Wakati mwingine unajidanganya kuwa unachofanya ni sahihi. Lakini mbona hautaki kusikiliza mawazo tofauti Edo? Ni kwa sababu ya maisha ya kidunia ambayo wakati mwingine huwa tunadhani ni marefu sana. Wakati mwingine huwa tunadhania kwamba tulizaliwa kabla ya kabla ya Mlima Kilimanjaro.

Kama ungepewa pumzi ya kutafakari wakati tukikupeleka futi sita chini ya ardhi ndipo utakapogundua kuwa kuna vitu vilikuwa vikubwa kuliko wewe. Ndipo utakapogundua kuwa ile bahari ya Indi pale Coco Beach na kwinginepo ilikuwepo kabla ya wewe.

Tenda mema kadri unavyoweza. Hili sio suala la dini wala kabila wala rangi. Kuna sehemu mwanadamu unakosea sana lakini kiburi cha pumzi za muda ndicho ambacho kinatusumbua kwa sasa. Mwisho wa siku pumzi zikiisha tutaondoka makaburini kurudi nyumbani kwako na kuanza kuongelea maisha mengine ya duniani.

Nyakati hizo wengi tutajikumbusha kimoyomoyo kwamba kuna mkubwa mmoja tu ambaye anapaswa kututia hofu na sio wewe ambaye dakika chache zilizopita tulikuwa tumetoka kuweka mikono ya sala kando ya kaburi lako na kurudi nyumbani kwako kuondoa tarubai angali ukiwa haupo.

Hapa namzungumzia kila mtu mwenye madaraka makubwa na madogo, umaarufu, au pesa au hulka ya kujisikia kuliko wengine. Binafsi nilizaliwa nikiwa uchi juu ya kitanda fulani cha hospitali ya Ocean Road kuelekea mwishoni mwa miaka ya 1970. Siku nikipoteza pumzi watakaonizika wanaweza kuamua nizikwe nikiwa nikiwa uchi. Maringo ya nini?

Ni nyakati tata katika nchi yetu. Katika ngazi ya mtu binafsi au taasisi zetu au serikali Kuu. Kuna sehemu tunakosea sana kwa kujiamini kupita kiasi. Maringo ya mwanadamu yanazidi kupitiliza. Inakera sana. Wengi wanafunga mdomo. Wengi wana hofu. Nilikuwa nawakumbusha tu, kuna mkubwa mmoja tu. MUNGU.

Usijivunie kuwa bosi wa Chadema. Usijivunie kuwa na sauti kubwa kwa Waislamu au Wakristo. Usijivunie kuwa bosi wa CCM. Usijivunie kuwa kiongozi mkubwa. Usijivunie kuwa tajiri wa mtaani kwako. Kuna sehemu moja unakosea sana.

Mwanamuziki Sunday Mjeda ‘LInex’ aliwahi kulalamika katika wimbo wa “Moyo wa Subira’ akitamani kurudisha nyakati nyuma arekebishe ubaya aliowahi kuufanya. Uzuri kwa Mungu, au ubaya kwetu, ni kwamba wakati watu wakitawanyika katika misiba yetu hatutaweza kurudisha nyakati nyuma.

Ni nyakati hizo ndipo tutajua kwamba kuna mwanaume mmoja tu. MUNGU.
Walionielewa vizuri nadhani watakuwa wamenielewa vizuri sana, hasa kwa kila kitu kinachoendelea katika nchi yetu kwa sasa. Life goes on. Kuna Mungu mmoja tu. Na kuna mimi mmoja tu.
Edo kumwembe.

Na kuna wewe mmoja tu, unayesoma Makala hii. TUTAFAKARI.
 
EDO KUMWEMBE
SIKU Fulani ya maisha yako. Hakutakuwa na wale walinzi kando yako. Hakutakuwa na rafiki zako kando yako. Hakutakuwa na wale washkaji zako wa mtaani kwako. Hakutakuwa na wale wapambe wako kando yako. Hata kama watakuwepo hautawaona.
Pua zako zitakuwa zimewekwa pamba ndani ya jeneza. Foleni ya watu itakuwa ikikuaga. Hautakuwa na fahamu. Ina maana atakayeshika kifua chako hatasikia mapigo yoyote. Hautajua kama anayekuaga ni rafiki yako au adui yako. Mama yako na dada zako kando ya jeneza watakuwa wakilia wakiliwazwa na rafiki zako, ndugu na jamaa zako.
Kaka zako watakuwa bize sana kuhakikisha watu wote walio msibani wanapata mahitaji yao. Mmoja atakuwa anahakikisha kila mtu amekula. Mwingine atakuwa akifarijiwa na rafiki zako wa karibu. Mwingine atakuwa kaburuni kuhakikisha kaburi lako limechimbwa vema. Mwingine atakuwa anaongea na sheikh au askofu kuhusu mpangilio mzima wa mazishi.
Kama una cheo kikubwa sana basi wakubwa waliobaki watakuwa wanapiga saluti mbele ya jeneza lako. Hata hivyo haitasaidia sana. Haitakurudishia pumzi. Kama ulikuwa mwanamuziki mahiri sana, bado haitakurudishia pumzi. Alikufa Michael Jackson na bado hajarudishwa.
Kama ulikuwa kiongozi maarufu bado haitasaidia. Alikufa Mwalimu Nyerere na bado hajarudishwa. Alikufa Nelson Mandela, alikufa Martin Luther King, alikufa JF Kennedy. Wote hawa hawajarudi tena. Kila siku tunapita kando ya makaburi yao na kuishia kusema “Walikuwa mashujaa”. Lakini mbona hawanyanyuki chini ya udongo na kusimama?. Kumbe hawakuwahi kuwa wakubwa kuliko wewe.
Kuna mkubwa mmoja tu ambaye hapigiwi saluti lakini anabakia kuwa mkubwa. Anaitwa Mungu. Kwanini uringa sana hapa duniani? Ni swali linaloendelea kushangaza sana. Wakati mwingine maisha yanashangaza sana. Sana. Sana. Kuliko tunavyofikiri.
Wakati tukikaribia kukuaga, mtu ambaye ataendelea kuheshimika kwa muda tu, ndani ya siku hiyo, atakuwa MC wa shughuli hiyo. Hautaweza kumpinga. Yeye ndiye ambaye atatuambia muda gani ‘utabebwa’ kwenda eneo moja kwenda jingine. Yeye ndiye ambaye atatuambia muda wa maziko, muda wa kula, muda wa kwenda makaburini. Yeye ndiye ambaye kwa mbwembwe atatuambia matanga au Arobaini yatakuwa lini.
Leo utakuwa na mbwembwe nyingi katika kundi la mashabiki wa muziki wako wanaokuhusudu. Leo utakuwa na mbwembwe nyingi kwa walinzi wanaokulinda na silaha. Leo utakuwa katika baa Fulani ya sehemu Fulani ukitoa kila amri ambayo wanyonge wanatekeleza bila ya kuguna. Unalipa bili unaondoka. Lakini duniani kuna mkubwa mmoja tu.
Wakati mwingine unajidanganya kuwa unachofanya ni sahihi. Lakini mbona hautaki kusikiliza mawazo tofauti Edo? Ni kwa sababu ya maisha ya kidunia ambayo wakati mwingine huwa tunadhani ni marefu sana. Wakati mwingine huwa tunadhania kwamba tulizaliwa kabla ya kabla ya Mlima Kilimanjaro.
Kama ungepewa pumzi ya kutafakari wakati tukikupeleka futi sita chini ya ardhi ndipo utakapogundua kuwa kuna vitu vilikuwa vikubwa kuliko wewe. Ndipo utakapogundua kuwa ile bahari ya Indi pale Coco Beach na kwinginepo ilikuwepo kabla ya wewe.
Tenda mema kadri unavyoweza. Hili sio suala la dini wala kabila wala rangi. Kuna sehemu mwanadamu unakosea sana lakini kiburi cha pumzi za muda ndicho ambacho kinatusumbua kwa sasa. Mwisho wa siku pumzi zikiisha tutaondoka makaburini kurudi nyumbani kwako na kuanza kuongelea maisha mengine ya duniani.
Nyakati hizo wengi tutajikumbusha kimoyomoyo kwamba kuna mkubwa mmoja tu ambaye anapaswa kututia hofu na sio wewe ambaye dakika chache zilizopita tulikuwa tumetoka kuweka mikono ya sala kando ya kaburi lako na kurudi nyumbani kwako kuondoa tarubai angali ukiwa haupo.
Hapa namzungumzia kila mtu mwenye madaraka makubwa na madogo, umaarufu, au pesa au hulka ya kujisikia kuliko wengine. Binafsi nilizaliwa nikiwa uchi juu ya kitanda fulani cha hospitali ya Ocean Road kuelekea mwishoni mwa miaka ya 1970. Siku nikipoteza pumzi watakaonizika wanaweza kuamua nizikwe nikiwa nikiwa uchi. Maringo ya nini?
Ni nyakati tata katika nchi yetu. Katika ngazi ya mtu binafsi au taasisi zetu au serikali Kuu. Kuna sehemu tunakosea sana kwa kujiamini kupita kiasi. Maringo ya mwanadamu yanazidi kupitiliza. Inakera sana. Wengi wanafunga mdomo. Wengi wana hofu. Nilikuwa nawakumbusha tu, kuna mkubwa mmoja tu. MUNGU.
Usijivunie kuwa bosi wa Chadema. Usijivunie kuwa na sauti kubwa kwa Waislamu au Wakristo. Usijivunie kuwa bosi wa CCM. Usijivunie kuwa kiongozi mkubwa. Usijivunie kuwa tajiri wa mtaani kwako. Kuna sehemu moja unakosea sana.
Mwanamuziki Sunday Mjeda ‘LInex’ aliwahi kulalamika katika wimbo wa “Moyo wa Subira’ akitamani kurudisha nyakati nyuma arekebishe ubaya aliowahi kuufanya. Uzuri kwa Mungu, au ubaya kwetu, ni kwamba wakati watu wakitawanyika katika misiba yetu hatutaweza kurudisha nyakati nyuma. Ni nyakati hizo ndipo tutajua kwamba kuna mwanaume mmoja tu. MUNGU.
Walionielewa vizuri nadhani watakuwa wamenielewa vizuri sana, hasa kwa kila kitu kinachoendelea katika nchi yetu kwa sasa. Life goes on. Kuna Mungu mmoja tu. Na kuna mimi mmoja tu. Edo kumwembe. Na kuna wewe mmoja tu, unayesoma Makala hii. TUTAFAKARI.
ujumbe kuntu
 
Ipo siku ,siky ambayo kila nafsi itakabiliana na malipo sawia kwa matendo na mawazo yake.Siku ambayo hakuna aijuaye na wala hakuna awezaye kuizuia,tukae tukijua kwamba siku hiyo tutakuwa kimya kukabiliana navukweli.Hakuna atakayeweza kutambua mateso wala furaha tutakayokuwa tunakabiliana nayo isipokuwa sisi na Mungu tu.Natamani nitende yaliyo mema lakini nitawezaje katika dunia hii iliyojaa kila aina ya uovu?
 
Kauli za kujifariji hizi sana sana unazikuta tu huku africa hadi huyo unae msema aje afe atakuwa ameshakula bata la kutosha infact kila binadam lazma aje afe.........
 
Kwa ambaye atajiuliza na kutafakari Edo ni MCHOCHEZI WA MAISHA kwakutoa UKUMBUSHO HAPA TUNAPITA TU DUNIANI HATA UWE NA NINI AMRI ZOTE IPO SIKU UTALAZWA KTK UDONGO kibuli majivuno havitasaidia hata kama ni mwanasiasa uwe mjuzi wa kubadili gia angani zungusha miguu hata uwe wa kichurachura
 
Kauli za kujifariji hizi sana sana unazikuta tu huku africa hadi huyo unae msema aje afe atakuwa ameshakula bata la kutosha infact kila binadam lazma aje afe.........
hua nashtuka sana pale masikini wengi wanapowaambia matajiri watakufa.. kifo ni mwisho wa kila binadamu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom