political monger senior
JF-Expert Member
- Nov 26, 2020
- 1,827
- 5,990
Leo tuangazie adui wa maendeleo kwa watu wa rika zote anayejulikana kama aviator na maarufu kwa jina la Kandege. Mchezo huu umegubikwa na siri nyingi sana na ambazo wenye betting sites wamekuwa wakizitumia kuchota mamilioni ya fedha kutoka kwa wateja wao bila jasho. Wachezaji wa huu mchezo wametawaliwa na mawazo yenye wingi wa tamaa na wengi huamini kuwa ipo siku na wao watashinda kiasi kikubwa cha pesa.
JE, MCHEZO HUU WA AVIATOR UKO FAIR KWA PANDE ZOTE MBILI; MWENYE BETTING SITE NA MTUMIAJI?
Ukiingia kwenye mchezo wenyewe utaona maneno kuwa mchezo uko fair. Lakini katika ulimwengu halisi wa mchezo huu hakuna fairness hata kidogo.
SIRI ZILIZOPO KATIKA MCHEZO AMBAZO NDIO MWIBA KWA WATUMIAJI:
1. Kila mtumiaji huwekwa kwenye chumba chake mwenyewe (Each user is treated individually). Ukiingia kwenye aviator utaona namba kubwa sana ya users jambo ambalo humfanya mtumiaji kujiona yeye ni miongoni mwa jamii pana. Kama unafikiri kuwa watumiaji huwekwa pamoja kwa kila mzunguko basi unajidanganya. Account ya mtumiaji inasimamiwa kivyake na ndio maana mtumiaji akishusha stake amount (kiasi cha kubetia) flight results go higher and higher. Ila akiongeza stake basi flight results go down immediately. So hakuna njia ya kuvuna pesa kwenye aviator hata uwe expert wa aina gani.
2. Aviator inaongozwa na AI (artificial intelligence) yaani akili bandia katika kusimamia kila account ya mtumiaji. No matter how smart you are, you cannot defeat the AI.
Ushahidi wa hoja hii ni kitendo cha watumiaji wapya kuvuna pesa wakati wa mwanzo wa usajili wao. Katika muda huo AI huwa bado inatengeneza data kwa kuzingatia tabia za mtumiaji. Tabia kama vile mahusiano ya stake amount na cashing out. Baada ya kukamilisha kuandaa behavioural profile ya mtumiaji huanza kujichotea pesa kilaini kabisa. Kama umepanga kucash out kwenye 2.00 yenye inakatia kwenye 1.99. Utaliwa na mwisho ujinyonge ufe.
3. Automated cashing out service. Hii ni hatari sana kwa watumiaji. Mtumiaji anapoweka huduma ya automatic cash out anakuwa ameirahisishia system mara 10000 tofauti na kama asingeweka. Hata ungekuwa ndio wewe sasa unajua kabisa ikifika 2.00 fulani atachota 1,000,000 kutoka kwako, ungeruhusu itokee? Kwenye automatic cash out hata ukiweka kwenye 1.1 bado utaliwa tu.
4. Matumizi ya watumiaji mfu (ghost users). Sio kweli kuwa ile namba ya users inayoonekana kwenye aviator ni halisi. Na ndio maana hakuna majina halisi yanayotumika. Ulishawahi kujiuliza kwann huandikwi jina lako kama ulivyojisajili? Sababu wangefanya hivyo ingekuwa rahisi kujua siri nyingine kama ile ya kwanza hapo juu. Je, mbinu hii ina madhara yoyote kwa mtumiaji? Jibu ni ndio! Ghost users wanaweza kukushape kimtazamo na kukufanya upoteze pesa kwa kuwaiga. Ghost users wanaweza kuweka stake ya 1,000,000 na flight ikapaa mpaka 100 na bado asicash out. Wewe mtumiaji halisi ukithubutu hata kuweka 1000 chamoto utakipata. Kwann? Jibu kwasabu wewe umeweka pesa halisi na hiyo ndio inayotafutwa na system na sio pesa bandia ya ghost users.
5. Kukata network Yao pale wanapoona hatari ya kupoteza fedha. System inaweza kukata mfumo wa internet na kumfanya mtumiaji ashindwe kucash out. Mtumiaji anaweza kuhisi ni mtandao wa simu yake kumbe imetengenezwa makusudi kulinda pesa zao.
HITIMISHO:
Hakuna mwenye uwezo wa kutengeneza kipato kupitia aviator na online casino games nyingine. Kitumie kipato chako wisely kwa mustakabari wa maendeleo yako na Tanzania kwa ujumla.