realoctopus
JF-Expert Member
- May 11, 2014
- 3,232
- 1,982
Pongezi nyingi kwa LEMA na wananchi wa Arusha.
Wewe huna kumbukumbu
Nakupa tanoHongera Mandela wa arusha
Hongera Hon.Lema juhudi zako tunaziona Na kushuhudia ahadi zako.Long live Hon.Lema.Safi sana magufuli.
Talk less, do more
Ulichoahidi ndicho unachotenda ,siyo kama chadema leo unahubiri Lowasa ni fisadi kesho unahubiri Lowasa ni mleta mabadiliko aende ikulu!!!!
Kajiweka mwenyewe kisongoLema ni Jembe,hata wamweke Rumande mwaka mzima,atachaguliwa tu kuwa mbumge wa Arusha.
Amefanya jitihada gani za kizuia?Pamoja na jitihada RC wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kutaka kukwamisha jitihada za Mbunge huyo hatimaye zimegonga mwamba.
Mandala hakuwa mwizi, tafadhari acha kulinganisha Mandela na vitu vya kijinga.Hongera Mandela wa arusha
Moja ya sere za za chama cha Maigizo ni kuweka watu ndaniWacha Gumbo aendelee na drama zake, Mbunge wetu kazi anayopiga yunaitambua
HakikaMiaka 5 ni michache mnoooo
Kampuni ya kichina iliyoshinda zabuni ya kujenga Hopsitali maalumu kwa ajili ya mama na mtoto eneo la Matevesi Wilaya ya Arusha, CRJE (EA) Ltd imekwisha aanza kazi ya ujenzi baada ya kukamilisha usajili wa mradi na kuandaa eneo la kazi, ofisi na kuunganisha umeme na maji.
Mradi wa Hospitali maalumu kutatua kero kwa masuala ya kina mama na watoto uliasisiwa na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema na kutangazwa kwa umma mwaka 2010 wakati wa kampeni za Uchaguzi mkuu za mwaka huo. Wananchi wa Arusha walimuelewa na kumchagua Godbless Jonathan Lema kuwa Mbunge wao.
Mwaka mmoja baadae Mbunge Lema kupitia taasisi aliyoianzisha baada ya kuwa Mbunge ya ArDF-Arusha Development Fund, akafanikiwa kupata kiwanja cha kujenga Hospitali hiyo kutoka kwa Mawalla Advocates kupitia kwa Mkurugenzi wake marehemu Nyanga Mawalla mahali ambapo ndipo inapojengwa Hospitali hiyo sasa.
Makabidhiano ya kiwanja hicho toka kwa Mawalla Advocates kwenda ArDF yalishuhudiwa na Kiongozi Mkuu wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mh Freeman Mbowe, Mkurugenzi wa ArDF Elifuraha Mtowe pamoja na viongozi wa chama chake wananchi wengine.
Kikapita kipindi cha ukimya wakati huo Mbunge Lema akiwa amevuliwa ubunge. Aliporudishiwa baada ya kukata rufaa na kushinda akaendeleza wazo lake kwa kutafuta wafadhili wa kuweza kufanikisha mradi wenyewe tayari akiwa na kiwanja mkononi.
Jitihada za Lema kupitia marafiki na wadau mbalimbali zilimkutanisha na watu wa ulaya kutoka Shirika la Maternity Africa ambao waliafiki wazo lake na kuamua kuendeleza mchakato kwa kuanzisha michango kwa jamaa zao ulaya ili kupata fedha za kugharamia mradi.
Kufikia mwaka 2015 ArDF ya Lema wakasainishana mkataba na Maternity Africa wa kuendeleza mradi huo kwa ArDF kuwakabidhi rasmi kiwanja maalumu kwa Hospitali hiyo. Sherehe za makabidhiano zilifanyikia kwenye kiwanja hicho na kushuhudiwa na wadau wa pande zote wakiwemo wenye maslahi na mahitaji ya kimsingi ya kina mama na watoto.
Mpaka kufikia mwezi Agost 2016 Maternity Africa walikuwa wameshapata pesa za ujenzi na kuandaa michoro na kumtafuta mtaalamu mshauri na mkandarasi ambaye ndio sasa amekwishakuanza kazi ya ujenzi ambayo inatakiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja.
Hospitali hiyo ikikamilika itasaidia kupunguza kero ya huduma za uzazi kwa mama na mtoto, kama ambavyo Mh Lema aliona miaka mingi na kudhamiria kulifanikisha bila kujali ingemgharimu muda na pesa kiasi gani.
Ni jambo la kutia faraja sana kwamba Mbunge yuko Magereza kwa zaidi ya miezi miwili sasa lakini aliyoyaasisi yanaendelea kuwepo.
Tuzidi kumuombea mkandarasi, wataalamu wengine na wafadhili wakamilishe mradi huu kwa wakati kama walivyopanga ili wananchi wa Arusha waonje matunda mengine ya Mbunge Lema.