mkuu kama una dondoo nyingine ya kupunguza matumizi please just share tujifunze,Jinsi ya kupunguza gharama za gypsum board.
Piga hesabu unahitaji boards ngapi. Mfano unahitaji 50pcs. Nunua 20pcs kwanza. Mwambie fundi aweke nzima nzima,yaani aweke sehemu zinazoingia nzima nzima nyumba nzima. Zile sehemu zinazohitaji vipande aziache kwanza.
Utashangaa nzima zinaingia 20 au pungufu.
Zile sehemu zinazohitaji vipande nenda hardware ongea nao wakuuzie damaged boards(hizi huwa zinakuwa zimemeguka kidogo wakati wa kumshusha mzigo hawawezi kuuza kwa wateja wa kawaida) hizo utauziwa moja 5000-7000. Unanunua kama 30pcs ndio unaenda kuweka sehemu zinazohitaji vipande.
Hesabu iko hivi
Boards nzima 50 ni 50*14,000=700,000
Kwa njia hii nilioshauri
Board nzima 20 ni 20*14,000=280,000
Damaged board 30*6000=180,000
Total 460,000
700,000-460,000=240,000
Umeokoa 240,000.
hii ya gypsum nimeipenda.