Uhusiano wa producers na studio wanazofanya kazi

ukwaju_wa_ kitambo

Senior Member
Sep 15, 2024
148
168
PRODUCERS NA STUDIO..

1. Kumthamini Producer

Master J na Hermy B waliamua kujiweka kando
kiasi na kuleta maproducer wengine kusimamia
studio hizo. Master Jay alimchukua Marco Chali
kutoka Kama Kawa Records takriban miaka 7
iliyopita, huku Hermy B akimtoa Pancho Latino
kutoka Dhahabu Records na hadi leo maproducer
hao si tu hawajawahi kuondoka, bali hawana
kabisa mpango wa kuondoka. Sababu kubwa ni
namna wanavyothamiwa.

2. Uhuru kwa Producer

Ukiwa mmiliki wa studio na ukataka kumsimamia
producer kwa kila anachokifanya na ukahisi
anaweza kupiga vimeo, ni rahisi kuanza
kuonekana bosi mkuda na kumnyima producer
uhuru. Marco Chali na Pancho Latino wana uhuru
mkubwa katika studio hizo, imradi tu hawavunji
sheria za kawaida. Ndio maana Marco Chali
amekuwa na uhuru hadi wa kuanzisha Marco
Chali Foundation ambayo inapewa support na
Zantel. Master Jay angekuwa mswahili, angeleta
zengwe kwa fikra kuwa Marco anafaidi sana.

3. Mchukulie Producer kama partner na sio
kama Mwajiriwa..

Marco Chali na Pancho Latino katika studio zao
hawachukuliwi kama waajiriwa, bali ni kama
partners. Hisia hiyo huwafanya wafanye kazi kwa
kutofikiria malipo bali hufikiria kufanya kazi kwa
bidii kuzipeleka mbele zaidi studio zao.

4. House Style/Identity

B’Hits ni mabingwa wa hili. Hawa jamaa wana
namna yao peke yao ya kufanya kazi na huenda
hawafanani kabisa na studio zingine. Ni jambo
zuri kila studio ikiwa na utambulisho wao na
namna yake ya kufanya kazi.
5. Professionalism
MJ Records na B’Hits zimetoka kwenye kuwa
kama studio tu bali pia kama kampuni. Na ndio
maana B’Hits ni Music Group ikiwa na matawi
Tanzania na Kenya. Kazi zao wanazifanya kama
ofisi kubwa zifanyazo mathalan mikataba ya
wasanii na mambo mengine. Kukaa Marekani
kwa Hermy kumemfanya ajifunze jinsi studio za
huko zinavyofanya kazi na amekuwa akijaribu
ku’apply’ baadhi ya mambo yanayowezekana kwa
Tanzania kwenye studio yake.

6. Utaratibu wa kuachia nyimbo

Sitotaja jina, lakini kuna producer wa studio moja
ambaye kila siku huwa napata email mbili ama
tatu za nyimbo mpya. Utawezaje kuachia nyimbo
tatu kila siku? Zinaenda wapi? MJ Records na
B’Hits wanaweza wakae hata miezi 6 bila
kuachia nyimbo na hiyo haimaanishi kuwa
hakuna nyimbo wanazorekodi. Ni utaratibu tu
waliojiwekea katika kuachia nyimbo na sio ‘bora
nyimbo’. Quality ni bora kuliko Quantity.

7. Hakuna ubosi

Marco Chali anamchukulia Master J kama ‘bro’
na Pancho kwa Hermy hivyo hivyo. Hakuna ubosi
ndio wamedumu.

8. Ubahili ni adui

Kama producer anaingiza fedha nzuri, kwanini
mmiliki usimlipe vizuri na kumfanya afurahi?
B’Hits na MJ Records wanaujua mchezo.

9. Ushirikiano
B’Hits ni mfano mzuri katika hili.

Wimbo mmoja
unaweza kushambuliwa na watu zaidi ya wanne.
Pancho atatengeneza mdundo, msanii ataingiza
sauti, Hermy B atakuja kufanya mastering ama
kuutuma Kenya kwa Randy wa B’Hits Kenya
kuongeza kitu pia. Wimbo ukitoka unakuwa na
ubora unaotakiwa. Kwa upande wa MJ Records
tunafahamu jinsi Marco Chali anavyowatumia
wadogo zake kutengeneza ladha tofauti za
midundo.

10. Hakuna Ubabaishaji

Hii ni sababu kwanini MJ Records inaongoza kwa
kutengeneza matangazo mengi ya biashara.
Makampuni makubwa kama ya simu hutumia
advertising agency zinazoendeshwa kisomi.
Haziwezi kufanya kazi na studio zenye longo
longo.

Ukwaju wa kitambo
#tunakurudisha_kaleeeeee
0767 542 202

(KATIKA PICHA)
Pancho Latino, producer wa B’Hits
FB_IMG_1726746879213.jpg
 
Hii makala umeitoa wapi? Mbona unazungumzia watu waliotangulia mbele ya haki kana kwamba wako hai?
 
Au mimi ndio mshamba huyu pancho latino unae msemea hapo si alishakufa kitambo tena alikufa kwa ajali ya maji kule kidimbwi kama ni hivo wewe ni mchambuzi mpeche mpeche huna lolote @ukwaju_wa _kitambo
 
Back
Top Bottom