Uhusiano kati ya Presha kupanda na nguvu za kiume

namba moja tuu

Senior Member
May 4, 2017
162
142
Kupungua nguvu za kiume

Uhusiano wa matatizo ya nguvu za kiume na presha ya kupanda ni mkubwa sana. Kwa nini kuna uhusiano mkubwa? Presha ya kupanda husababisha damu ndogo sana kutiririka ndani ya uume. Uume unatakiwa upokee damu ya kutosha tena yenye kuja kwa nguvu au kasi ili uweze kusimama vizuri na kwa uimara.

Presha ya kupanda hudhuru kunyanzi za mishipa ya damu na hivyo kusababisha mishipa hiyo kukakamaa na njia yake ya kupitisha damu kuwa nyembamba zaidi (athererosclerosis).

Presha ya kupanda husababisha mishipa ya ateri kushindwa kufunguka vizuri na hata kupelekea kupasuka.
 
Hata baadhi ya dawa zinazotumika kutibu pressure ya kupanda nazo pia zinaathiri nguvu za kiume.
 
Back
Top Bottom