Uhujumu Uchumi: Shehena kubwa ya bidhaa toka ng'ambo yakamatwa Bandari bubu Tanga

Ah Boti ninunue mimi nimpe Mvuvi aniletee Hesabu so abebe mali asizojua na akamatwe chombo changu ndio kitaifishwe? hizi Sheria za Wapi mtenda kosa ndio akamatwe mali zake alizobeba za wizi... Huu ni Uonevu Sheria zetu kama zipo hivyo zibadilishwe... Magufuri ulisema utawasaidia wavuvi na mabaharia... wasaidie vyombo hivyo ni mali ya mmiliki... Mbona yale Magogo yaliyobebwa na Meli za Kinana hazikutaifishwa... Hizi Sheria zipoje au kwa Wanyonge tu? Magari yaliyobeba Kura za Wizi hayakutaifishwa? Mabasi yaliyokamatwa yakibeba Magunia ya Bangi hayakutaifishwa... Ndege zinazobeba Madawa ya Kulevya hazitaifishwi maana Nimestushwa Kutizama TV kiongozi anatamka wazi wazi ati Sheria za nchi watataifisha Hizo Mali na Boti zilizobebea hiyo Mizigo...Aombe Radhi hio sio Sheria ya Nchi.... kama zinachagua
 
Kila chanzo haramu kikidhibitiwa uchumi wetu utakaa vizuri sana, hizo bandari bubu zimejaa karibu katika kila pwani ya kila mkoa wa Tanzania. Serikali ijipange kwenye logistics za ulinzi kwani wakati mwingine wanaoingiza mizigo kwa njia za panya wanakuwa na mtandao mpana.
 
Waje mbweni wanasindikizwa NA haohao mpaka kwenye lami kamaujawalip vema wanakusakizia mbeleni else hukuu mnapoteza mabillion
 
tanga18.jpg

Shehena ya bidhaa mbalimbali zenye thamani ya mamilioni ya shilingi ikiwemo vipuri vya magari kutoka nchi tofauti za Pakistan, India na Ubelgiji zimekamatwa katika bandari bubu ya Kigombe iliyopo wilayani Muheza wakati zikiingizwa nchini kinyume cha sheria bila kulipiwa ushuru.

ITV imeshuhudia askari wa jeshi la polisi zaidi ya 100 wakiwa wamezingira boti zilizotumika kubeba bidhaa hizo ambapo kamimu kamanda wa polisi mkoani Tanga mratibu mwandamizi wa jeshi polisi Mayala Towo amesema shehena ya mzigo huo ni pamoja na mafuta ya kupikia kutoka Ubelgiji, sukari kutoka India na vipuri kutoka nchi za Ulaya.

Kwa upande wake meneja wa mamlaka ya mapato nchini (TRA) tawi la Tanga Bwana amekiri kuwa hali ya ukwepaji wa kodi katika bandari bubu ya Kigombe ni ya kutisha kwa sababu sehemu kubwa ya bidhaa zinazouzwa katika maduka mbalimbali katika baadhi ya maduka yaliyopo katika jiji la Tanga, Muheza na Mkinga zinatoka nje ambazo inadaiwa kuwa zimeingizwa nchini kinyume cha sheria hatua ambayo imesababisha bidhaa zinazozalishwa katika viwanda vya ndani kukosa soko.

Kufuatia hatua hiyo kaimu meneja wa forodha mkoa wa Tanga Bwana Jumbe Magoti amesema wazingatia sheria zilizowekwa katika zoezi la tozo za faini kisha watataifisha vyombo vilivyotumika katika usafirishaji wa bidhaa hizo kutoka kisiwani Zanzibar kuingizwa bara bila kulipiwa ushuru.
Kahangaikeni kukamata makontena 11,000 yaliyo letwa na Miji meli mikubwa na kutoweshwa pasipo kulipiwa kodi. Hivyo vingalawa mnavionea na mmeamua kuwatoa kafara ili mtengeneze majina yenu. Si kwamba hiyo ni mara ya kwanza kwa mizigo kuingia kupitia hivyo vi bandari bubu na ukweli mnaujua na wengine wenu mkishiriki katika biashara hizo. Subirini wenye uchungu na nchi wapate nafasi mje vuliwa nguo kweupe.
 
hata siwaelewi hawa watu.
kinachoshangaza bidhaa ikitoka zanzibar ikija bara lazima ilipiwe tena ushuru hata kama zanzibar ilishalipiwa.
mi naona muungano ungevunjika tu,ni mateso kwa wazanzibari..
nje hawatambuliki..
misaada ya UN FIFA yote kuishia bara..
wakileta biashara bara ni shida..
pesa zao za iliokua benk ya EAC zimeishia bara..
makusanyo ya bandari yao foreign currency utalii mahesabu jioni hufanyika bara..
wazanzibar wanachangia serikali ya Jamhuri ambayo Zanzibar haipo kumbe ni serikali ya Tanganyika,kilichopo Zanzibar ni hawa mazombie tu a k a askari wanaotumiwa na bara kuidhibiti Zanzibar na kufanya mauwaji kama yale ya janyary 27 2001.
 
Tuko pamoja mkuu. Huu ni wajibu wetu wote Kama Watanzania. Mzigo ulikuwa mkubwa sana. So you can imagine hapo nyuma ilikuwaje!!?? Wahusika wamekusikia muda si mrefu utasikia kimenuka huko Boko mkuu.
Hizi ni sinema tuu mkuu ,kwani unafikiria ilikua haijulikani ?? Mbezi beach tu hapa ni bandari bubu ,madawa ya kulevya ndio yanapitishiwa hapa na wanajua vizuri
 
Utasikia mi natoa mil tano, mchango huo wa ujenzi wa kanisa, kumbe ni wezi, ngoja waisome.
Wacha michango ya kanisa iendelee!
Kutoa Ni Moyo wa ukarimu .
Lbd ungelaumu watu wanaoenda weekend kustarehe Dubai , Hong Kong nk, michango ya CCM mtu anatoa hadi 100M ili kujiweka karibu na watawala nk.
JPM Ni tofauti tuache tu kuvunja sheria ndio tutaelewana nae!
 
Hoja yako ni ya msingi. Serikali huwa inatoa vibali kila mwaka kwa waagizaji kutoka nje kutokana na mahitaji ya Watanzania. Na nyingine huwa inatoka kwenye viwanda vya ndani. Hao wanaopitisha njia za magendo sidhani Kama ndio suluhisho la upungufu wa Sukari hapa nchini.
Kama utakumbuka kabla ya Rais wa awamu ya tatu kuanzisha utaratibu wa makampuni machache kupata vibali vya kuagiza sukari nje, bei ya sukari ilikuwa chini. Walipopewa kibali cha kuhodhi tu biashara, bei ilipanda na haijashuka tena. Machoni mwangu wahujumu uchumi ni hao wanaohodhi biashara kubwa na ku-control bei za bidhaa.
 
Tuko pamoja mkuu. Huu ni wajibu wetu wote Kama Watanzania. Mzigo ulikuwa mkubwa sana. So you can imagine hapo nyuma ilikuwaje!!?? Wahusika wamekusikia muda si mrefu utasikia kimenuka huko Boko mkuu.
Huo ni mzigo mmoja tu kati ya maelfu ya mizigo inayopitishwa kila siku, na wahusika wanajua, hapo itakuwa hawakwenda sawa, ila wakielewana itaendelea kupitishwa kama kawaida bila kukamatwa. Hii ndio Tanzania iliyooza..
 
Huo mchongo unajulikana muda mrefu mbn na jamaa walikuwa mbona wanaramba sana posho hata bagamoyo ununio, nyamisati na sio shehena ya magendo tu hata unga unaletwa kwa makilo huko baharini uvivi hakuna ni dili kubwa tu
Nyamisati ni noma.
 
Ah Boti ninunue mimi nimpe Mvuvi aniletee Hesabu so abebe mali asizojua na akamatwe chombo changu ndio kitaifishwe? hizi Sheria za Wapi mtenda kosa ndio akamatwe mali zake alizobeba za wizi... Huu ni Uonevu Sheria zetu kama zipo hivyo zibadilishwe... Magufuri ulisema utawasaidia wavuvi na mabaharia... wasaidie vyombo hivyo ni mali ya mmiliki... Mbona yale Magogo yaliyobebwa na Meli za Kinana hazikutaifishwa... Hizi Sheria zipoje au kwa Wanyonge tu? Magari yaliyobeba Kura za Wizi hayakutaifishwa? Mabasi yaliyokamatwa yakibeba Magunia ya Bangi hayakutaifishwa... Ndege zinazobeba Madawa ya Kulevya hazitaifishwi maana Nimestushwa Kutizama TV kiongozi anatamka wazi wazi ati Sheria za nchi watataifisha Hizo Mali na Boti zilizobebea hiyo Mizigo...Aombe Radhi hio sio Sheria ya Nchi.... kama zinachagua
Hizo sio sheria za Tanzania tu. Kama haujui sheria ya haya mambo jinsi zilivyo wewe ni bora upite kimya.
Huyo nahodha wa chombo inatakiwa ahakikishe documents zote za mizigo ziko sawa kabla hajapakia na kusafirisha huo mzigo.
Marekani ukijihusisha na biashara haramu na gari yako ikikutwa imebeba dawa za kulevya kwa Lengo la usafirishaji hiyo gari ni mali Yao na Kama umekutwa na kiasi chochote cha fedha ni Mali ya police or sheriff's office.

Unaposema mabasi yanayobeba magunia ya Bangi hayataifishwi huo ni Unafiki uliobobea. Nenda kaulize vizuri kwenye vyombo vya Dola jinsi wanavyotaifisha Mafuso,mabasi na vyombo vingine kila mara kwa kosa la kubeba Mirungi,Bangi n.k.
Hii ni Awamu ya Tano..yaliyopita si ndwele. Vunja Sheria uone.
 
Shehena kubwa ya Bidhaa Haramu ikiwemo Matairi,sukari,mafuta ya kupikia imekamatwa Bandari bubu Tanga kutokea Zanzibar.

Operesheni hiyo imefanywa na Polisi 100 wakishirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na Usalama.

Vyombo vilivyohusika katika usafirishaji wa shehena hiyo vyote vimetaifishwa. Walikuwa wanakwepa Kodi. Hii vita ya Uhujumu UCHUMI ni nzito.

Chanzo:
ITV.
Hii ni vita nzuri maana wakwepaji ushuru wanakwepa pia ubora na hivyo kuleta madhara mara mbili maana ukiingiza bidhaa bila kupitia njia halali maana yake na watu wetu wa TFDA na TBS hawakujaliwa nafasi ya kujiridhisha kama ni salama kwa matumizi nchini kwetu. Hongera vyombo vya usalama kwa kuokoa taifa hili dhidi ya manyang'au hao
 
Hapa kazi tu! Ukweli ni kuwa hali hii ipo kwa miaka mingi ila sasa kwa serikali hii naona sasa wamebanwa. Hongera sana TRA na muwe macho zaidi kwani wengine watataka kutumia njia hizi kukwepa ushuru baada ya madeal yao kukwepa ushuru bandarini kuminywa.SAFI SANA.
 
Uchumi utakua tukijua Thamani ya madini tuliyonayo..angalau hata lingekuepo somo la lazima la aina zoote za madini na mbuga zetu na uthamani wake katika shule zetu za sekondari..tupo busy na mafuta ya kupikia mara magari...Madini yenye Thamani amabayo kiasi kidogo tuu kikisimamiwa kwa umakini maisha ya Watanzania wanatoka katika daraja hili..Mungu Naomba Tusaidie Tupate Japo Ufahamu wa Rasilimali Tulizonazo na ziwe Faida kwa Watanzania woote..
 
Ah Boti ninunue mimi nimpe Mvuvi aniletee Hesabu so abebe mali asizojua na akamatwe chombo changu ndio kitaifishwe? hizi Sheria za Wapi mtenda kosa ndio akamatwe mali zake alizobeba za wizi... Huu ni Uonevu Sheria zetu kama zipo hivyo zibadilishwe... Magufuri ulisema utawasaidia wavuvi na mabaharia... wasaidie vyombo hivyo ni mali ya mmiliki... Mbona yale Magogo yaliyobebwa na Meli za Kinana hazikutaifishwa... Hizi Sheria zipoje au kwa Wanyonge tu? Magari yaliyobeba Kura za Wizi hayakutaifishwa? Mabasi yaliyokamatwa yakibeba Magunia ya Bangi hayakutaifishwa... Ndege zinazobeba Madawa ya Kulevya hazitaifishwi maana Nimestushwa Kutizama TV kiongozi anatamka wazi wazi ati Sheria za nchi watataifisha Hizo Mali na Boti zilizobebea hiyo Mizigo...Aombe Radhi hio sio Sheria ya Nchi.... kama zinachagua

Hapo mvuvi wako ni kama amevua bomu. Mali na boti vyote vinazama na mvuvi wako mahatuti.
 
Kahangaikeni kukamata makontena 11,000 yaliyo letwa na Miji meli mikubwa na kutoweshwa pasipo kulipiwa kodi. Hivyo vingalawa mnavionea na mmeamua kuwatoa kafara ili mtengeneze majina yenu. Si kwamba hiyo ni mara ya kwanza kwa mizigo kuingia kupitia hivyo vi bandari bubu na ukweli mnaujua na wengine wenu mkishiriki katika biashara hizo. Subirini wenye uchungu na nchi wapate nafasi mje vuliwa nguo kweupe.

Bandu bandu humaliza gogo.
 
Uchumi utakua tukijua Thamani ya madini tuliyonayo..angalau hata lingekuepo somo la lazima la aina zoote za madini na mbuga zetu na uthamani wake katika shule zetu za sekondari..tupo busy na mafuta ya kupikia mara magari...Madini yenye Thamani amabayo kiasi kidogo tuu kikisimamiwa kwa umakini maisha ya Watanzania wanatoka katika daraja hili..Mungu Naomba Tusaidie Tupate Japo Ufahamu wa Rasilimali Tulizonazo na ziwe Faida kwa Watanzania woote..

Uchumi wa Tanzania utakuwa kwa kukusanya kodi, kubana matumizi, na kuelimisha wananchi wake siyo kujua thamani ya madini tuliyonayo.
 
Back
Top Bottom