SoC04 Uhai wa asasi zisizo za kiraia: Wito kwa serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Mamshungulii

Senior Member
May 3, 2023
172
85
Licha ya umuhimu wa kazi wanayofanya, watendaji wengi wa utawala wa kidemokrasia wanaofanya kazi na asasi za kiraia wanakabiliwa na udhaifu mkubwa wa uwezo wa ndani wa kuendesha ofisi kuwa endelevu katika kutatua matatizo yanayokabili maendeleo. Udhaifu huu unazidishwa na ukosefu wa njia za ufadhili za kuaminika na endelevu ambazo zitawaruhusu kuwekeza katika uwezo wao wa ndani na kazi kuu za msingi. Ukosefu wa uwezo na uendelevu huchangia zaidi miungano na mienendo dhaifu na kuwafanya wahusika hawa kukabiliwa na vitisho kutoka nje.

Pia asasi zisizo za kiserikali zinapenda kushiriki kwa pamoja na watendaji wengine wa serikali katika mchakato wa kuboresha sera na sheria. Hatahivyo, ushirikishwaji wa mashirika haya katika utungaji wa sera na sheria umekuwa wa kimchongo sana na kujuana, usio na uwazi, usio na matokeo thabiti, na hauzingatii itakiwavyo kushirikisha wenye ulemavu.

Aidha, asasi za kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali yanakabiliwa na mazingira magumu ya kisheria na udhibiti kutoka kwenye mamlaka za kiserikali. Sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali ya 2019 inaweka mamlaka za asasi kupitia mamlaka mbalimbali ya serikali ,suala hili linaathiri sana mashirika machana na yenye uwezo mdogo.

Sheria ya uhalifu wa Mtandao, Sheria ya Takwimu, Sheria ya vyama vya siasa, na sheria ya huduma za vyombo vya habari pia huathiri uwezo wa mashirika ya afua mbalimbali ikiwemo zinazohusiana na vijana kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Mashirika yasiyo ya kiserikali kwasasa yanafanya kazi katika maeneo mbalimbali kama vile afya, elimu, maji, haki ya uhuru na demokrasia, kuboresha hali ya kiuchumi na masuala ya kibinadamu na utu. Katika kutekeleza mashirika hutumia mbinu mbalimbali kama vile mikutano, kujengeana uwezo, kutekeleza miradi ya ujenzi, sanaa, muziki na habari, kupitia harakati zake mashirika haya yamepata mafanikio makubwa kama vile:-
• Kupitishwa kwa sheria ya vijana ya taifa ya mwaka 2015 na kanuni zake 2017
• Mikopo isiyo na riba ya asilimia 4 kutoka halmashauri
Vuguvugu la vijana mjini hasa wa vyuo vikuu na kwenye mitandao ya kijamii kama vile JAMII FORUM wamechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza idadi kubwa wa viongozi wa vyama vya siasa a kuwezesha vijana kuunda majukwaa mbalimbali ya elimu na maendeleo.
Ingawa kuna changamoto lakini kuna ongezeo kubwa la asasi zisizo za kiserikali kujisajili na kuzidi uaminiwa katika ushirikishwaji na utendaji wa kazi.

CHANGAMOTO MBALIMBALI ZINAZOWAKUMBA ASASI ZISIZO ZA KISERIKALI NI:-
• Sheria zisizo rafiki kwa Asasi zisizo za kiserikali kama vile namna ya kupeleka taarifa za utekelezaji kila robo mwaka, kupata ruhusa ya kuendelea na mradi kama pesa itazidi milioni 20 na kusajili shirika upya kila baada ya miaka 10.
• Sheria zinazosimamia uendeshaji wa asasi zisizo za kiserikali zilibadlishwwa kwa hati ya dharura.
• Aasasi kutokuwa na ajenda ya pamoja na mbinu endelevu za kubadilisha mahusiano ya kiutendaji.

HIVYO BASI ANDIKO HILI LINATOA RAI KWA SERIKALI:-
1. Kutunga sheria za kupiga marufuku mila na desturi zote zenye madhara kulingana na mikataba ya kimataifa na ya kikanda.
2. kuridhia utekelezaji, na kutoa ripoti kuhusu mikataba yote inayolinda na kukuza haki ya vijana
3. kuidhinisha, kutekeleza, na kutoa ripoti kuhusu mikataba yote inayolinda na kukuza haki za vijana
4. kushirikiana na makundi yaliyotengwa na mashirika yao kuunda kampeni za muda mrefu na afua zingine kushughulikia kanuni za kijamii za kibaguzi.
5. Kuzingatia kuunda mazingira rafiki na wezeshi yanayofaa kwa ufadhili wa mashirika ya kiraia na uendelevu.
6. kuhakikisha ujumuishaji na ufikiaji katika majengo, mifumo na michakato yake
7. Kuhakikisha mifuko ya fedha ya taifa inatekeleza wajibu wake ili kuwezesha asasi zifanye kazi itakiwavyo.
8. Ifufue mchakato wa kutekeleza uwepo wa mabaraza ya watu wa aina husika ili kuwapa fursa ya kufanya kazi pamoja na kuzungumza wanayoyahitaji kupitia majukwaa yao.
9. Kushirikisha asasi za kiraia na wadau wengine kwa muda muafaka katika michakato ya kutunga sheria, na pia kuacha kabisa kutunga sheria kwa kutumia hati ya dharura.
10. Kuruhusu wananchi na asasi za kiraia kuhoji ujumuishwaji wa maoni yao katika sera na sheria zinazotoka.
PIA ANDIKO HILI LINATOA RAI KWA ASASI ZISIZO ZA SERIKALI NA ZA KIBINAFSI: -
a) Kutoa ufafanuzi wa dhana juu ya mabadiliko ya kijinsia na masuala ya ujumuishi.
b) Kuiwajibisha serikali kwa utekelezaji wa mikataba na mikataba ya kitaifa na kikanda kuhusu utawala wa kidemokrasia na nafasi ya kiraia, pamoja na haki za vijana.
c) Kushauri na kushawishi serikali na watendaji wengine juu ya mikakati madhubuti ya ujumuishaji.
d) kutetea na kushawishi utungwaji wa sheria zinazopiga marufuku mila na desturi zote zinazodhuru kulingana na uingiliano wa kimataifa na kikanda.
e) kwa pamoja kuandaa na kuendesha kampeni za kushughulikia kanuni za kibaguzi na ambazo zinaleteleza kuathiri mabadiliko ya mitazamo na tabia zinazozunguka tabia za vijana kuhusu haki za vijana.
f) kuwa majasiri, wachapakazi, wabunifu na wazalendo katika kusukumia kuleta mabadiliko ya kijinsia katika utawala na nafasi ya kisiasa
g) Kushawishi uwepo wa ufadhili wenye uwajibikaji kutoka kwa serikali na wabia wa maendeleo.
h) Kutumia majukwaa mbalimbali ya kiuratibu ili kushawishi wadau wa maendeleo kutoa ufadhili wa muda mrefu, wenye urahisi wa kubadilisha matumizi kuendana na mazingira, na wenye kufadhili shughuli za kiuendeshaji za shirika, pamoja na zana na mifumo.
i) Kutengeneza mikakati endelevu na harakati mbalimbali ili kutoa usaidizi wa kiufundi kwa asasi zenye uhitaji.
BILA KUSAHAU WAFADHILI AMBAO WANAFADHILI MAENDELEO IPO HAJA KWAO:
I. Kusaidia uingiliaji kati wa muda mrefu ambao unasaidia mabadiliko katika kanuni za kijamii katika vizazi
II. kutumia diplomasia ya umma na binafsi kushinikiza kutungwa kwa sheria zinazopiga marufuku mila na desturi zote hatari kama zile zinazoendana na mikataba ya kimataifa na kikanda.
III. kusaidia mashirika mwamvuli kwa vijana na wenye afu husika kufikia jamii nyingi za vijijini na ambazo ni ngumu kuzifikia.
IV. kuhakikisha upatikanaji katika miradi yote inayofadhiliwa na wafadhili, ujenzi na michakato
V. Kutoa msaada wa kiufundi ili kuwezesha asasi zisizo za kiserikali zenye uwezo mdogo kiutendaji kuimarika na kutekeleza wajibu.
VI. Kuanzisha utaratibu mzuri wa kufadhili mashirika yanayofika ndani sana huko vijijini kuweza kutoa huduma kwa urahisi.
VII. Kuwezesha mashirika yasiyo ya kiserikali kushawishi mabadiliko ya kisheria ili kuboresha mazingira ya ushiriki wa wananchi katika michakato ya utawala wa kidemokrasia.


View: https://www.instagram.com/tv/C7gG9eXK8hR/?igsh=MXhkbnR0cGRxY2J1dQ==



View: https://www.instagram.com/p/CyBD1fANeON/?igsh=OHNzOGpsbWY4bnQ1




View: https://www.instagram.com/p/C16o2oiNl05/?igsh=MWozZnVrOWN4bWpwag==




View: https://www.instagram.com/p/CyA0IXbNi6w/?igsh=M3BoMmF1dGxuOWdi



View: https://www.instagram.com/reel/C7wghkCtLF4/?igsh=eDBpNTM4ZWQ0aTJv



View: https://www.instagram.com/reel/Cx_ksXhtBq6/?igsh=ZzZpcnRhbzZzeTg5




View: https://www.instagram.com/reel/C7J_q2st2Ep/?igsh=bmJldDg0a2dwaGFo



View: https://www.instagram.com/reel/CyC-qhHNaWM/?igsh=angybWV1YzF6bGlz




View: https://www.instagram.com/reel/Cx7u8c0NZuB/?igsh=bHB6YjN0NDkzN2Vi
InShot_20240608_181044958.jpg
 

Attachments

  • NSNS ENGLISH VERSION - FINAL.pdf
    2.5 MB · Views: 5
Back
Top Bottom