Katika kuandaa vyakula vya mifugo protini hutumiwa kwa wingi. Chanzo kikuu cha protini ni bidhaa kama dagaa, soya nk. Ila sasa hivi dagaa wameadimika na kuwaweka wazalishaji wa vyakula vya mifugo katika hali mbaya.Kipo chanzo kingine kizuri cha protini kwa vyakula vya wanyama, na chanzo hiki kimeanza kuchangamkiwa na wajasiriamali. Chanzo hicho ni mende na senene. Mende wanaotakiwa ni wale wakubwa wanene (wanapenda kuishi chooni).Kwa harakaharaka leo 26/12/2016 nilimsikia mtu mmoja akizungumzia jambo hili la ufugaji mende kituo cha tbc1, lakini mtangazaji alishindwa kumhoji huyo mgeni kuhusu namna na mawasiliano ya ufugaji mende, ila aligusia kwamba kilo moja ya mende ni shs 15,000.Nimeingia google na kutafuta habari zaidi bila mafanikio isipokuwa nilichoambulia ni jinsi ufugaji mende unavyotajirisha watu huko china.
Kwa hapa tanzania sijapata habari yoyote.
Je, kuna yeyote aliyeinyaka habari hii ya ufugaji mende na senene vizuri atudadavulie?