Ikiwa ingekubidi ule vyakula vichache pekee maisha yako yote nini ungekula na kwanini ?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,813
45,495
Tufanye umeambiwa uchague vyakula fulani bora ila vichache na itakubidi ndo uvile maisha yako yote usibadilishe aina nyingine me nadhani ambavyo ningeweza kufikiria vingekuwa ni.

1.parachichi Kwa sababu ya afya ya moyo.

2.kabeji au tembere maana ina vitamini k,na itazuia saratani.

3.samaki maana mafuta yake mazur hayana cholesterol.

4.kitunguu saumu na cha kawaida pale nakuwa nimemaliza Kwa ishu ya pressure

5.karanga na Maharage hapo nakuwa nimemaliza Kwa ishu ya kupata protini.

6.machungwa hapa nafukuzi vitamini C.

7.viazi vitamu chanzo kikubwa cha carbohydrate

Maana yangu ni nini yaani kama ukichagua hivyo ndo ujue vyakula vingine vya kawaida hutakula maishani sijui wali, kitimoto, dagaa, ugali, n. K
 
Ugali dona na dagaa mchelee, jani - tembele na figiri - tunda ndizi, chungwa, parachichi
Sema kwenye tunda hapo ujue matikiti na matango source nzuri Sana ya zinc na magnesium.. Itakuaje kuzikosa mwaka mzima na zinasaidia mambo ya sex
 
Tufanye umeambiwa uchague vyakula fulani bora ila vichache na itakubidi ndo uvile maisha yako yote usibadilishe aina nyingine me nadhani ambavyo ningeweza kufikiria vingekuwa ni.

1.parachichi Kwa sababu ya afya ya moyo.

2.kabeji au tembere maana ina vitamini k,na itazuia saratani.

3.samaki maana mafuta yake mazur hayana cholesterol.

4.kitunguu saumu na cha kawaida pale nakuwa nimemaliza Kwa ishu ya pressure

5.karanga na Maharage hapo nakuwa nimemaliza Kwa ishu ya kupata protini.

6.machungwa hapa nafukuzi vitamini C.

7.viazi vitamu chanzo kikubwa cha carbohydrate

Maana yangu ni nini yaani kama ukichagua hivyo ndo ujue vyakula vingine vya kawaida hutakula maishani sijui wali, kitimoto, dagaa, ugali, n. K
Ugali dagaa, maharage,tembele

Viazi mbatata
 
Siku ukipata mgeni inabidi uingie gharama za kununua vyakula ambavyo yeye ameruhusia kuvila,hata kwenye mahotel kutakua na Menu ya kila mtu!

:D

Haya mambo ya kufikirika zaidi kiongozi. Mwenyezi Mungu katuwekea vyakula mbali mbali tuchague na kula tunachokipenda.

Sasa huyu ndege JOHN homeboy naona anataka kutuzonga tu.

Chamsingi angejaribu kuweka aina ya vyakula na faida zake ili isaidie wasomaji kujua ni vyakula Gani wavitafute kutokana na mahitaji ya miili Yao.
 
Back
Top Bottom