Ufafanuzi wa matumizi na michango: Kila familia ilipewa Sh 1m siku ya kuaga, Zitapewa Sh 3,857,143

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema anasikitishwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa ambao wamelichukulia suala la vifo vya wanafunzi 32 wa Lucky Vicent kisiasa.

Katika taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari, Gambo amesema uongozi wa mkoa wa Arusha umeamua kutoa taarifa ya wazi kwa yumma kuhusu michango iliyotolewa na matumizi yake.

“Hili si tukio la kisiasa bali ni mtihani na changamotyo kubwa uliozikumba familia za wananchi wetu. Wakati serikali inahangaika na shida za watu tunasikitika kuona baadhi ya viongozi wa kisiasa wanahangika na mitandao ya kijamii,”imesema taarifa hiyo

Taarifa hiyo iliyoambatana na jedwali lenye mchanganuo wa rambi rambi hizo inaonyesha kuwa jumla ya michango ya serikali na ya wadau ni Sh 261.3 milioni.

Michango ya Serikali ni Sh 102.7milioni na ya wadau ni Sh 158.5milioni.

Katika mchanganuo wa taarifa hiyo, Gambo amesema familia za wafiwa hao zitapewa Sh 3,857,143 kwa kila familia. Kila familia ilipewa Sh1milioni siku ya kuaga miili uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Chanzo: Mwananchi
Walitanguliziwa 1Million, je zilizobaki zilikuwa ni ahadi?
 
Gambo ndiye ameufanya msiba wa watoto wetu wapendwa kuwa siasa.

Mbaya zaidi anaifanya serikali ionekane inafanya visivyo ktk rambirambi za msiba huo. Mchanganuo alioutoa haungii akilini hata kidogo.

Namshauri aache kuichonganisha serikali na wananchi halafu anajifanya kumtafuta mchawi wakati mchawi ni yeye mwenyewe.
 
Nchi hii viongozi wanaombea majanga yatokee waweze kuneemeka na rambi rambi, eti tuliwapa 1M zingine tutakuja kuwapa,
Ni aibu kubwa sana watu wajitolee kwa ajili ya wafiwa mkusanyaji anazitia kapuni?hapo hata shetani anashangaa kwa kweli
 
Angeweka na hako kamchanganuo humu ingesaidia sana. Sasa mbona walipewa 1M tu badala ya kupewa zote? Lengo la kuwapa kidogo kwanza ilikuwa nini???
fedha za michango huwa hazifiki kwa pamoja maana kila mtu anatoa kwa wakati wake
 
Naomba niwatkane wote waliotoa michango. Kwani hawajui policy ya michango ya maafa kwa nchi hii. Wajinga. Kila mmoja angeliwapelekea wafiwa personally! Tunajenga miundo mbinu ya daraja lililoleta maafa! Haraka haraka wamesahau ya kagera. Watanzania wajinga! (Note: ujinga sio tusi please)
Haya mkuu ila upumbavu ndo tusi..... angeweka wazi michango yote ni kiasi gani by names au kwa asiye taka tajwa aweka amount bila jina.... harafu kwa wafiwa aonyeshe wazi kazigawa vp maana kuna wanao sema yule yatima hakulipwa, kama hakulipwa ni kwa nn? Kwa nn wasipewe wamiliki wa alipo kuwa anaishi na yatima wenzake, mara mwalim na dereva hawakulipwa... .yawezekana wamelipwa lakini awe muwaz bana hasa katika nyakat hiz za waswas wa rambirambi za kagera la sivo halitamwacha salama hili na atakuwa anakuwa mentioned by name yeye kwa jinsi alivo handle issue nzima.....
 
Mwenye kuelewa anieleweshe.

1,Kwa nini gharama za kusafirisha miili ya marehemu kutoka eneo la tukio karatu hadi hospitali zitokane na rambirambi, je ina maana mtu akipata ajali ndugu wanalipia gharama za kusafirisha maiti kutoka eneo la ajali hadi hospitalini siku ya kuchukua maiti au?

2,Kwa nini gharama za kuwalisha viongozi wa serikali waliohudhuria mazishi kwa siku tatu zitokane na michango ya rambirambi, kwa vile walihudhuria mazishi tena kama muwakilishi hiyo safari labda ina malipo kwa hiyo wangekula kama waombolezaji wengine (maji) kama wanahitaji zaidi anunue kwa hela yake

3,Marehemu wapo 35, sijaelewa gharama za magari 45 kusafirisha marehemu sehemu mbalimali kwa ajili ya maziko zinatoka wapi na pia tunaambiwa kuna mabasi 8 yalikodiwa kwa ajili ya mazishi yaliofanyika arusha.
 
alifanya hivyo baada ya ahadi kukusanywa, wabunge na wadau wengine
Huwezi kusema zilipatikana kiasi kadhaa hapo hapo ukawa umejumuisha na ahadi, fuatilia tamko lake utaelewa kwanini watu walianza kuhoji baada ya taarifa yake.
 
Back
Top Bottom