Ufafanuzi wa mapato na matumizi ya serikali kwa mwezi Machi, 2016

Huu ndio uwazi unaotakiwa kwa kuwa ni rahisi kuhoji matumizi yasiyo rasmi. Lakini isiishie hapa wizara ya Fedha ishuke mpaka kwenye taasisi. Ingawa wakubwa wataupinga huu mfumo kwa kuwa utawapunguzia ulaji. Kama iwapo wataendelea namna hii tunaweza kufika mbali.
 
Naopongeza utaratibu huu. Kwani taarifa kuhusu mapato na matumizi ya kodi ni incentive kwa walipa kodi

Halafu mwisho wa mwaka pia wanaweza ku- consolidate hizi taarifa wananchi wakajua kwa mwaka zimekusanywa shilingi ngapi, sekta zipi zimetumia fedha nyingi, na wapime value for money kwa recipients wa hizi fedha za walipa kodi.
lete uthibitisho kuwa kilichosemwa ndicho kilicho kisanywa
 
Katika vitu ambavyo Magufuli atajiletea heshima ni huu utaratibu wa kueleza mapato na matumizi. Sasa kwa mara ya kwanza naanza kuona kodi yangu iko kwenye mikono sahihi. Hongera rais wangu JPM, najua kwa sasa umetingwa kulipa madeni ya mtangulizi wako lakini kwa mwendo huu matumizi yajayo yataenda zaidi kwenye miradi ya maendeleo.

Naisubiri bajeti yako kwa matumaini makubwa
 
Nani alikwambia PSPF hawana hela. Nenda kaangalie miradi waliyowekeza hasa Yale majengo pacha pale karibu na TRA. Hivi unapoamua kuwekeza kwenye mradi mkubwa vile ina maana HAWAKUFANYA Actuarial Valuation??? Principle ya liquidity haikufanyiwa assessment before choice and form of investment??

Queen Esther

Kumbe serikali haina mpango na deni la mifuko ya hifadhi ya jamii hasa PSPF kwa sasa!???
 
Mwelekeo mzuri huu! Big up jembe letu kutoka kanda ya ziwa!! Ila kwenye mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ni kwa ajili ya semester ya 3 tu au walikuwa wanamaanisha nini?
 
Ujenzi wa viwanda umetengewa ngapi wakuu maana wengine tunavisubiri kwa hamu kubwa sana!
 
Mimi nilitegemea utauliza RUZUKU KWENYE VYAMA VYA SIASA imetumikaje???? Waweke nao wazi mapato na matumizi ndio waanze kuikosoa Serikali kwenye mapato na matumizi. Wanachama nao wana haki ya kujua mapato na matumizi. ANDAMANA KWA HILI NDG

Queen Esther

Uu wiz kama vp tuandamane
 
Hivi kwenye ruzuku ya vyama vya siasa wanachama wanapata nini???

Queen Esther

MIMI HIZI HADITHI HIZI HUZICHUKIA HASWA.....
MAKUSANYO HAYO OK...SASA SISI TUNAPATA NINI HAPO?....NI SAWA NA YALE YA UCHUMI KUKUA WAKATI KILA KUKIKUCHA AFADHALI YA JANA.
 
Nani alikwambia PSPF hawana hela. Nenda kaangalie miradi waliyowekeza hasa Yale majengo pacha pale karibu na TRA. Hivi unapoamua kuwekeza kwenye mradi mkubwa vile ina maana HAWAKUFANYA Actuarial Valuation??? Principle ya liquidity haikufanyiwa assessment before choice and form of investment??

Queen Esther


Najua natoka nje ya mada lkn nimeguswa na matumizi yako ya hilo neno actuarial, wewe ni Mwanahisabati au uko kwenye mambo insurance kwa maana neno hilo hutumia zaidi na Mathematician waliobobea kwenye mambo ya Bima au kama ni neno lenye matumizi ya kawaida basi pia nisahihishe kwa hilo!
 
Back
Top Bottom