Udogoni Dar es Salaam 1960s

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,902
31,972
UDOGONI DAR ES SALAAM 1960s

Kila nipitapo Maktaba hukutana na picha zinazonikumbusha mengi.
Picha hii alinipa Abdallah Mgambo miaka mingi ilioyopita.

Ilipigwa kwenye picnic mwaka wa 1965.
Kulia ni Adam Kingui, Abdallah Mgambo na Kleist Sykes.

Hawa wote walikuwa wanafunzi wa sekondari.
Adam Kingui na Abdallah Mgambo wakisoma St. Joseph's Convent na Kleist Aga Khan.

Nakumbuka nini kwa hawa rafiki zangu?
Vipaji vyao.

Hawa wote walikuwa watoto wa Gerezani.
Adam Kingui alijaaliwa kipaji kikubwa sana cha muziki.

Nakumbuka akiwa Kitchwele Boys siku ya Parent's Day kulikuwa na maonyesho.

Adam na wenzake kama wanne walipanda kwenye jukwaa wamevaa mashati meusi bow tie nyeusi, suruali nyeusi na viatu vyeusi.

Kikundi hiki kikawa kinaimba na kucheza.
Walikuwa wanaimba nyimbo gani?

Walikuwa wanaimba nyimbo za Kizulu kutoka Afrika Kusini huku wanacheza.

Walikuwa wanacheza kwa steps yaani choreography.
Wanainama kwa pamoja na kuinuka hivyo hivyo.

Wanakwenda kulia na kushoto kwa pamoja.
Utapenda.

Hizi nyimbo zilikuwa za Manhattan Brothers kundi kutoka Johannesburg, Afrika Kusini, nyingine za Dorothy Masuka, Miriam Makeba na Spokes Mashiane.

Hii ilikuwa mitindo ya Jive na Kwela.

Nyimbo hizi zilikuwa maarufu zikipigwa Tanganyika Broadcasting Corporation (TBC) toka miaka ya 1950.

Sisi kama watoto tuliathirika sana na mambo haya kama walivyoathirika wazee wetu.

Wazee wetu hapa Dar-es-Salaam wakivaa suti kama walizokuwa wakivaa vijana wenzao katika mitaa ya Johannesburg.

Adam namuona kwa macho yangu akicheza na kuimba pale jukwaani.

Nakumbuka siku moja Adam anatoka shule Kitchwele anakwenda kwao Mtaa wa Kipata na Sikukuu na mbele Livingstone.

Kanikuta mimi nimesimama duka la Mwarabu nyumbani kwa Mama Kilindi.
Radio ilikuwa inapigwa rekodi, "Young World."

Adam akasimama akawa anaimba ile nyimbo anafatisha neno kwa neno.
Adam tukicheza mpira pamoja uwanja wa Shule ya Nanaki.

Hii ilikuwa shule ya Masingasinga kabla ya uhuru 1961.

Adam alikuwa na kipaji cha mpira akicheza Fullham timu iliyokuwa Mtaa wa Kipata.

Lakini Adam alipenda muziki zaidi na akaanzisha bendi yake The Rifters yeye akipiga lead guitar.

Rifters waliondoka Dar-es-Salaam na wakahamia Mombasa katika miaka ya katikati 1970s.

Adam Kingui akiweza kuiga guitar la Steve Cropper, Bobby Womack, Bavon Marie na wapigaji wengine wengi.

Abdallah Mgambo alikuwa Pele wetu katika mpira - key player na star.

Alicheza Cosmopolitan toka yuko shule na ndiye alikuwa Head Prefect St. Joseph's Convent wakati wetu.

Abdallah alikuwa mtu mpole sana na nadhifu.

Kleist akicheza mpira mzuri.
Kuna kisa Kleist alinihadithia.

Alipewa hela akanunue viatu vya shule yeye akaenda Dar-es-Salaam Music and Sports House akanunua Puma viatu alivyokuwa akivaa Pele.

Hili duka lilikuwa maarufu sana kwa kuuza vyombo vya muziki pamoja na santuri na vifaa vya michezo yote.

Asubuhi Kleist na nduguze wanaingia kwenye Mercedes ya baba yao kwenda shule Kleist akaonekana kuvaa viatu vya zamani.

Kuulizwa akasema kanunua viatu vya mpira Puma.

"Sikupi hela nyingine kununua viatu vya shule utavaa hizo Puma zako kama Pele."

Nini kilikuwa kipaji cha Kleist?
Akikimwaga Kiingereza vuzuri sana utapenda kumsikiliza akizungumza.

Ndugu zangu hawa wote wametangulia mbele ya haki.

Tulibakia marafiki ndugu kwa mapenzi ya dhati hadi mwisho ukubwani na tukazikana.

Mwenyezi Mungu awasamehe dhambi zao na awatie peponi.

1716291493932.jpeg

Kulia Adam Kingui, Abdallah Mgambo na Kleist Sykes 1965​
 
Mbona sioni picha hapa...🤔
 
View attachment 2995987
Kulia Adam Kingui, Abdallah Mgambo na Kleist Sykes 1965​
Nia uhadithie Sykes!!
 
Nia uhadithie Sykes!!
Narumuk,
Hapana.

Historia ya Kleist ni historia yangu.

Mama yake Kleist Bi. Mwamvua bint Mrisho alikuwa shoga wa mama yangu Bi. Baya bint Mohamed.

Bibi yake Kleist Bi. Mruguru bint Mussa alikuwa pia shoga wa bibi yangu Bi. Zena bint Farijala.

Babu yake Kleist, Kleist Abdallah Sykes alikuwa rafiki wa babu yangu Salum Abdallah Popo wakifanya kazi pamoja Tanganyika Railways na nyumba zao zikitazamana Mtaa wa Kipata.

Baba yake Kleist, Abdulwahid Sykes na baba yangu wamesoma shule moja Al Jamiatul Islamiyya Muslim School na wamekuwa marafiki hadi mwisho wa kuhitimishana.

Baba yangu Said Salum ananihadithia anasema Bi. Zena bint Farijala mama yake alikuwa na biashara ya kuuza vitumbua.

Yeye na Abdul Sykes kazi yao ilikuwa kila jioni wakimtwangia mchele wake.

Bibi akishamaliza kuchoma vitumbua vyake anaweka viwili pembeni, kimoja cha baba yangu na kingine cha Abdul.

Hii ndiyo ilikuwa ahsante yao.

Sasa historia hii yapata miaka 100.

Wanangu nikiwahadithia husisimkwa.

Halikadhalika watu wengi wa Dar es Salaam ambao kwangu ni wadogo na hawakuziona enzi hizi wananiomba niandike historia ya maisha yangu.

Kwani wewe huna historia ya kwenu?
Huwakumbuki wazazi wako baba, mama, babu na marafiki zao?

Lazima itakuwapo na itakuwa na mengi ambayo hapa yatatufunza kitu.

Andika historia ya wazee wako ni jambo jema wala sidhani kama kuna mtu atachomwa moyo na historia hiyo labda awe na hasad yaani wivu wa kupitiliza.

1716292165984.jpeg

Kleist na mimi katika utu uzima wetu tuko Msikiti wa Kipata msikiti waliosali babu zetu, kisha baba zetu na tukasali sisi wajukuu.
Vipi nisiipende historia hii?
Picha tulipiga 2015
 
Narumuk,
Hapana.

Historia ya Kleist ni historia yangu.

Mama yake Kleist Bi. Mwamvua bint Mrisho alikuwa shoga wa mama yangu Bi. Baya bint Mohamed.

Bibi yake Kleist Bi. Mruguru bint Mussa alikuwa pia shoga wa bibi yangu Bi. Zena bint Farijala.

Babu yake Kleist, Kleist Abdallah Sykes alikuwa rafiki wa babu yangu Salum Abdallah Popo wakifanya kazi pamoja Tanganyika Railways na nyumba zao zikitazamana Mtaa wa Kipata.

Baba yake Kleist, Abdulwahid Sykes na baba yangu wamesoma shule moja Al Jamiatul Islamiyya Muslim School na wamekuwa marafiki hadi mwisho wa kuhitimishana.

Sasa historia hii yapata miaka 100.
Wanangu nikiwahadithia husisimkwa.

Halikadhalika watu wengi wa Dar es Salaam ambao kwangu ni wadogo na hawakuziona enzi hizi.

Kwani wewe huna historia ya kwenu?

View attachment 2995993
Kleist na mimi katika utu uzima wetu tuko Msikiti wa Kipata msikiti waliosali babu zetu, kisha baba zetu na tukasali sisi wajukuu.
Picha tulipiga 2015
Unaona ulivyokuwa ukimnyenyekea! Umefunga mikono wakati yeye yupo kawaida. Ni kama Bwana na Mtwana wake mwenye miwani
 
Narumk,
Nimecheka sana.
Bwana na Mtwana.

Kitu gani kinachokughadhibisha kiasi hiki?
Kipi kibaya nilichofanya?

''Bwana'' Mzulu na ''Mtwana'' ni Mmanyema.
Angalia na hii nyingine tumepiga tulivyokuwa wadogo mwaka wa 1968.

Kleist alikuwa na miaka 18 mimi miaka 16:

1716297656906.jpeg

Kulia waliosimama wa kwanza ni mimi, Yusuf Zialor, Kleist Sykes Bubby Bukhari, Abdallah Tambaza.
Kulia wa kwanza waliochutama Abdul Mtemvu, Wendo Mwapachu na Kais​
 
Narumk,
Nimecheka sana.
Bwana na Mtwana.

Kitu gani kinachokughadhibisha kiasi hiki?
Kipi kibaya nilichofanya?

''Bwana'' Mzulu na ''Mtwana'' ni Mmanyema.
Angalia na hii nyingine tumepiga tulivyokuwa watoto mwaka wa 1968.

View attachment 2996072
Kulia waliosimama wa kwanza ni mimi, Yusuf Zialor, Kleist Sykes Bubby Bukhari, Abdallah Tambaza.
Kulia wa kwanza waliochutama Abdul Mtemvu, Wendo Mwapachu na Kais​
Kumbe Mmanyema wa Kariakoo? Unajua historia ya Wamanyema jinsi walivyojenga Kariakoo? Unajua hata lile jengo ambamo TANU ilizaliwa lilikuwa ni jengo la mwanamke wa kimanyema? Huwezi tofautisha Wamanyema na DRC ukumbuke. Mwisho juzi rafiki yangu alisema hajawahi kuona Mmanyema asiye Mwislam, sijui kama yupo sahihi.
 
Naam Mmanyema wa Kariakoo.
Babu yangu ndiye Mmanyema kizazi cha kwanza kuzaliwa Tanganyika.

Alizaliwa Shirati, Musoma kwenye Boma la Wajerumani ambako baba yake Muyukwa Samitungo alikuwa askari aliyetokea Bukavu akaingia Germany Ostafirka kaongozana na Wajerumani.

Mama yake alikuwa Mtusi.

Jengo ambalo TANU ilizaliwa pale 1954 kulikuwa kiwanja kitupu hapakuwa na nyumba.

Naijua vizuri sana historia ya ofisi ile ambayo ilikuwa ya African Association na ilijengwa kwa kujitolea kati ya 1929 na 1933.

Wazee wetu walikuwa wakikutana hapo kila Jumapili wakijenga kwa kujitolea
.
Babu yangu akiwa mmoja wa hawa wajenzi.

Hakika asili yetu Wamanyema ni Belgian Congo.

Kweli mimi binafsi nina miaka 72 sasa sijapata kukutana na Mmanyema ambae si Muislam.

1716299531820.jpeg

Picha ya ufunguzi wa Ofisi ya African Association 1933 na ilifunguliwa na Gavana Donald Cameron
(Picha hii ni kwa hisani ya Maktaba ya Picha ya Sykes na ipo katika kitabu cha Abdul Sykes)​
 
View attachment 2996108
Picha ya ufunguzi wa Ofisi ya African Association 1933 na ilifunguliwa na Gavana Donald Cameron
(Picha hii ni kwa hisani ya Maktaba ya Picha ya Sykes na ipo katika kitabu cha Abdul Sykes)​
Hili si sawa! Pale palipo na jengo jirani na barabara inayotenganisha jengo la Uhuru na ccm, ilikuwa ni nyumba ya mama wa kimanyema. Aliigawia TANU, hata picha zipo. Kwa bahati nishawahi kuhudumu OND hapo Lumumba. Kesho Nenda hapo utasoma mwenyewe. Wamanyema wengi wa Kariakoo walikuwa ni akinamama walio toka Bukavu kuja Tanganyika kusaka noti na kupelekea wazazi wao huko DRC. Wazee wa Kiswahili walikuwa wanawahonga Majumba.

Niendelee au nisiendelee
 
Naru...
Tunazungumza sehemu mbili tofauti.

''Unajua hata lile jengo ambamo TANU ilizaliwa lilikuwa ni jengo la mwanamke wa kimanyema?''

Haya ndiyo uliyoandika na mimi nikakueleza kuwa hapo hapakuwa na nyumba.

Ndipo nikakueleza historia ya ofisi ya African Association Mtaa wa New Street na Kariakoo 1929 nikakuwekea na picha.

Hapa ndipo ilipozaliwa TANU mwaka wa 1954:

1716308387588.jpeg

1716308527623.jpeg

Hapa aliposimama Abdul Sykes 1954 baba yake alisimama mwaka wa 1933 siku ya ufunguzi wa ofisi ya African Association.
1716308700351.jpeg

Picha kutoka ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika, London 1998
1716308921639.jpeg

Naru...
Tunazungumza sehemu mbili tofauti.

''Unajua hata lile jengo ambamo TANU ilizaliwa lilikuwa ni jengo la mwanamke wa kimanyema?''

Haya ndiyo uliyoandika na mimi nikakueleza kuwa hapo hapakuwa na nyumba.

Ndipo nikakueleza historia ya ofisi ya African Association Mtaa wa New Street na Kariakoo 1929 nikakuwekea na picha.
Tatizo unazunguka. Nazungimzia lile Makamba alibomoa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom