Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Status
Not open for further replies.
Mimi naupinga udini na ubaguzi wa aina yoyote ile 24/7-365/366. Hata kwenye usingizi huwa naupinga udini na ubaguzi. Hata nilipokuwa ka-embryo nilikuwa napinga udini na ubaguzi na nitaendelea hivyo nikiwa kaburini na hadi motoni.
 
Wanaweza kuwa waisilamu lakini hawana Uisilamu.Who knows.
 
Wanaweza kuwa waisilamu lakini hawana Uisilamu.Who knows.

hizi sasa kashfa za ajabu na kipuuzi.

una maana gani mtu kuwa muislam na asiwe na uislam. Wanaccm kama wewe ndio hamfai kabisaaa, kuwa na uislam ndio nini? au unataka kuanza mambo kuwa rais ajaye awe mkristo ila asiwe na ukristo?
 
Guys Tanzania is a scular state. Ndiyo maana tunapinga suala la kadhi. Kwa hiyo all we are concerned is the capability of an individual. Juu ya yote kama CCM wamechagua vilaza sio bora ili iwe ndiyo njia ya luwaondoa mafisadi. Ufisadi hauna Dini. Tanzania for a long time hatukua na tatizo la Dini ingawa at some point waislam walallmika kidogo. Lakini I thank Them kuwa wameweza ku catch up hasa kwa bara. Na kuwachagua waislam inaonesha mwamko wa kidomocrasia., TATIZO NI PALE HADIJA KOPA ANPOOMBNA KURA KWA KUTINGISHA KIDOLE JUU NA KUIBUKA MA USHINDI WA JUUU!! Wacheni Udini. Please.
 
...safi sana acha hawa mafisadi watibuane na udini wao ili tupate nafasi ya kuwatimua,this is the good news kwa sisi wapenda maendeleo!
 
Hata viongozi wote wakitoka dini moja au kabila moja, mimi sioni shida. Tatizo letu ni utendaji mbovu wa viongozi na wala sio dini wanazotoka.

Afadhali kuwa na mtu wa dini nyingine anayechapa kazi, kuliko dini moja na mafisadi.
 
Hivi viongozi waumini wa dini mbalimbali wametusaidia vipi katika suala la maadili? Ni wangapi wameacha uzinzi, wizi, ubadhirifu n.k kwa sababu wao ni waamini wa dini? Leo hii kuna viongozi wamepigwa mweleka kula Dodoma wiki iliyopita kwa vile ni hawakuwa tayari kutoa rushwa kwa sababu ya dini zao, na wakati huo huo, mtu mlokole kama Chokala aliamua kuabudu mbele ya altare ya wababe wakati wa suala la vijana Ukraine na dini yake haikumsukuma kusema ukweli na hata kujiuzulu! Ni bora asiyeamini Mungu ambaye anajali watu,fedha za umma, na anawajibika kazini kuliko "mswalihina" ambaye ni mwizi, mbadhirifu na fisadi!

Hata Mwalimu alighafirika pale alipoorodhesha sifa za Rais ajaye wa Tanzania na ya kwanza akisema ni "awe mcha Mungu".. matokeo yake Mcha Mungu akawa Mkapa... sasa huo ucha Mungu umemsaidia vipi kwenye suala la Rada, kwenye suala la biashara Ikulu n.k.?

Kuwa na dini hakumfanyi mtu kuwa mwema na mkweli hadi pale ile dini iwe imemuingia, kwani wengi wetu tumeziingia hizi dini bila dini kutuingia na matokeo yake tumebakia na majina tu ya dini hizo! Kwenye Ufunuo wa Yohana inasemwa "una jina la walio hai, lakini mwenyewe umekufa"!
 
Binafsi nilikataa hayo mambo ya kuita chama fulani cha kidini au kikabila kwa kuangalia idadi ya viongozi. Nililikataa hili kwa CHADEMA na CUF. Ninakataa tena hapa kwa CCM.

Ninachoomba ni wale wenzetu waliotumia kigezo hiki ku-lable vyama vyetu vya CHADEMA na CUF kwamba ni vya kidini na kikabila wasiwe na double standards wakati huu wakijadiliwa CCM. Nakumbuka waliyoongoza hii hoja ni mgongomgongo, Fikira Duni, Kada Mpinzani, Mtalii, Mswahili, Nugwi, na wengine ambao sasa wamebadili majina. Naomba watoke clean waseme hivyohivyo na kwa CCM; vinginevyo kwa ustaraabu uliojengeka katika forum hii watoke mbele waombe msamaha na kuyakana maneno yao.
 
Kitila, ndugu yangu wavumilie tu kwani unachowaomba kufanya ni sawa na kukinga mikono kuombea mvua jangwani!
 
Ninachoomba ni wale wenzetu waliotumia kigezo hiki ku-lable vyama vyetu vya CHADEMA na CUF kwamba ni vya kidini na kikabila wasiwe na double standards wakati huu wakijadiliwa CCM. Nakumbuka waliyoongoza hii hoja ni mgongomgongo, Fikira Duni, Kada Mpinzani, Mtalii, Mswahili, Nugwi, na wengine ambao sasa wamebadili majina. Naomba watoke clean waseme hivyohivyo na kwa CCM; vinginevyo kwa ustaraabu uliojengeka katika forum hii watoke mbele waombe msamaha na kuyakana maneno yao.

Mkuu,

Naona hapa umechukia kweli kweli kwi kwi kwi!!!

Hivi Mgongo Mgongo kapotelea wapi?
 
sumu ya ubaguzi huwa haikomi.. ikishaingia kwenye kundi fulani basi kundi hilo huanza wa kubagua. Likimaliza kubagua linatafuta kipimo kingine cha kutumia kubagua. Ukishabagua makabila na kuamua kabila fulani ni duni halistahili, basi unaenda kwenye kipimo kingine; dini. Ukishawabagua watu kwa dini, ukimaliza utajiuliza "hivi wengi ni dhehebu gani?" hivyo utaanza kuwatenganisha Sunni na Shia, Wakatoliki na Waprotestanti n.k mwisho unaweza kujikuta unaanza kubagua watu kwa kuwaanangalia (nani anafanana na Mtutsi)..

La maana ni lazima tuukatae ubaguzi mapema unapojitokeza. Ratio ya CC inasema wajumbe saba kutoka pande zote mbili za Muungano (which is absurdy in itself) hiyo kutoka Zanzibar you'll probably get all seven wakiwa ni Waislamu. Halafu ukija bara wale saba hata wakristu wakiwa wanne bado kwenye general membership utakuta waislamu 10.. Sasa ukija na nafasi za viongozi wanaoingia kwa nyadhifa zao Kikwete, Shein, Karume, Makamba bado namba ya Waislamu inaongezeka. So, hilo ni jambo la mantiki, utaweza kuepuka vipi isipokuwa useme "Zanzibar ichague wakristu, au Bara ilete wagombea wakristu tu" .. na ukishafanya hivyo.. ile sumu itakuwa imekuingia!!

Labda nisaidie hapo tuukataeje ubaguzi tunapo ona unaingia?

Na utauonaje kama sumu haijakuingia?

Binafsi naona sumu ninayo, kwani
Roho yangu haina amani kabisa na teuzi za wakuu wa Wilaya na Mikoa teuzi hizi zina nuka ubaguzi wa hali ya juu! haiwezekani kwamba ni 'mere coincidence'
 
Binafsi nilikataa hayo mambo ya kuita chama fulani cha kidini au kikabila kwa kuangalia idadi ya viongozi. Nililikataa hili kwa CHADEMA na CUF. Ninakataa tena hapa kwa CCM.

Ninachoomba ni wale wenzetu waliotumia kigezo hiki ku-lable vyama vyetu vya CHADEMA na CUF kwamba ni vya kidini na kikabila wasiwe na double standards wakati huu wakijadiliwa CCM. Nakumbuka waliyoongoza hii hoja ni mgongomgongo, Fikira Duni, Kada Mpinzani, Mtalii, Mswahili, Nugwi, na wengine ambao sasa wamebadili majina. Naomba watoke clean waseme hivyohivyo na kwa CCM; vinginevyo kwa ustaraabu uliojengeka katika forum hii watoke mbele waombe msamaha na kuyakana maneno yao.

Kitila utawaweza hao sisiemu na double standard zao. Mie nilishangaa wengi wao wakimuunga mkono hapa mchambuzi kuwa eti rais ajaye lazima awe mkristo at the same time wakipondea CUF eti ni chama cha kidini!

haya yaliyotokea dodoma ingawa hayanisumbui ila kwa standard ambayo wanasisiemu wameika hapa, ingetakiwa waje kuomba msamaha au kutoa maelezo kuhusu hili. Wenyewe utawaona wako kimyaaaaaa
 
Bado namsubiri kada atoke hapa, maana nasikia yeye kateuliwa rasmi kuwa msemaji wao kwenye mawasiliano ya internet (wink)!
 
Bado namsubiri kada atoke hapa, maana nasikia yeye kateuliwa rasmi kuwa msemaji wao kwenye mawasiliano ya internet (wink)!

mbona nipo hapa, na ccm iombe msamaha kwa "member wa jf kwa kusema cuf ni chama cha kidini "??(HAYO MANENO YALITOLEWA NA KIONGOZI GANI WA CCM ALIYEIWAKILISHA CCM ?)(ACHENI UONGO NDIO MAANA KWA NGUVU ZA MWENYEWEZI MUNGU MNAANZA KUFUJA WENYEWE) aliyesema hivyo is such a crap, and nothing but a internet materialistic rubbish !
unajua watu wakiwa kwenye net wanajiona wapo MORE SUPERIOR than kweli wakiwa jukwaani na hapa ndipo wamejaa wengi na utawaona tu !

simaanishi wewe kitila !
 
Kwa msingi huu, kama wanaccm hapa walikiita chama cha cuf cha kidini kwa sababu ya viongozi wake. Nadhani sasa inabidi ccm pia kiitwe chama cha waislam.

Kuanzia sasa kwa mtizamo wangu na imani yangu ya jino kwa jino dhidi ya ccm kwa kuiita cuf chama cha kidini. Kuanzia leo ccm inabadilishiwa jina hapa kutoka CCM kwenda CCW.

CCW inamaanisha Chama Cha Waislam
 
Mgaya, hawa CCM siku zote hutumia ujanja wao na umbumbumbu wa Wtz kwa maslahi yao kisiasa; ni hao hao ndiyo huanzisha propaganda chafu dhidi ya wapinzani wao kisiasa kwa kuwaita CUF ni chama cha kidini na CHADEMA chama cha kifamilia!

Nijuavyo mimi siku zote composition ya NEC ya CCM na CC yao wengi wao ni Waislam kwa maana ya kuwa NEC ya CCM huwa na idadi sawa ya wajumbe toka pande zote za Muungano. Mara nyingi utakuta upande wa Bara Wakristo wanazidi kidogo au inakuwa 50:50 lakini kwa sababu nusu ya Wajumbe wengine hutoka Zanzibar basi kule utakuta 99% ya wajumbe niu Waislam na hapo lazima NEC ya CCM inakuwa na Waislam wengi vivyo hivyo CC.

Kwa miaka mingi hilo halikuwa tatizo hadi pale Mwalimu Nyerere alipofariki ndipo likanza kuw issue maana hatuna tena mtu wa kukemea upuuzi huo. Sasa hili suala la kazi linapata nguvu kwa kuwa Mwalimu hayupo na Serikali kwa influence ya Waislamu wengi kuwepmo katika NEC na CC ya CCM usishangae hayo unayosema yakawa kweli maana hili suala halikuwahata la kujadiliwa, lingekemewa mapema lakini kwa kuwa wanahisi umaarufu wao (CCM) umepungua wemelazimika kuweka hilo katika Ilani kwa ahadi ya kulitafutioa ufumbuzi suala hilo na ukweli ni kuwa hawawezi kulipatia ufumbuzi sahihi hadi pale watakaporuhusu Mahkama ya Kadhi ianzishwe.

Kwa maoni yangu, madai hayo yanatiwa nguvu na udhaifu uliomo katika Serikali hii ya CCM.

WAJUMBE WA NEC SIO UDINI TU,TAZAMA MAJINA YAO UTAKUTA NI WATOTO WA VIONGOZI WOTE WALIOKO MADARAKANI,SASA KAMA VIONGOZI WA NCHI WANATOKA HUKOHUKO KWENYE CCM SI WANAFAMILIA WALEWALE WANAPOKEZANA VIJITI?NA YOTE HII NI KWA MASLAHI YA NANI?YA WATANZANIA WOTE AMA TABAKA FLANI?WANASEMA CHADEMA NI FAMILIA NA CUF NI UISLAMU,WAO NI NINI?TABAKA,UKOO,FAMILIA AMA DINI?MHH WENYE MACO WASIAMBIWE TIZAMA!NCHI IMESHAGAWANYWA NA INA WENYEWE!HAYA WE!
 
Binafsi nilikataa hayo mambo ya kuita chama fulani cha kidini au kikabila kwa kuangalia idadi ya viongozi. Nililikataa hili kwa CHADEMA na CUF. Ninakataa tena hapa kwa CCM.

Ninachoomba ni wale wenzetu waliotumia kigezo hiki ku-lable vyama vyetu vya CHADEMA na CUF kwamba ni vya kidini na kikabila wasiwe na double standards wakati huu wakijadiliwa CCM. Nakumbuka waliyoongoza hii hoja ni mgongomgongo, Fikira Duni, Kada Mpinzani, Mtalii, Mswahili, Nugwi, na wengine ambao sasa wamebadili majina. Naomba watoke clean waseme hivyohivyo na kwa CCM; vinginevyo kwa ustaraabu uliojengeka katika forum hii watoke mbele waombe msamaha na kuyakana maneno yao.

Kitila Mkumbo,

Mzee mimi sidhani kama nilikiita CUF au Chadema vyama/chama cha kidini, Labda ume mix tu mimi kuonyesha mapenzi yangu ya wazi kwa CCM na kukashifu vyama vyenu. Tunabezana sometimes, lakini mimi sio extremist kama Mswahili au Nungwi.

Huwa natazama pande zote za shilingi.

FD
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom