Udhaifu wa Naibu Spika Dr. Tulia Ackson na Uhuru wa Muhimili wa Bunge

Naibu spika ana kosa gani hapo? Waziri kesha toa maelezo kuhusu kurudishwa nyumbani hao wanafunzi ....na maelezo hayo yanaeleweka tatizo liko wapi? Na hawakufukuzwa wamerudishwa kwa muda wkt tatizo lao linapatiwa ufumbuzi wa kudumu.Muacheni naibu spika afanye kazi yake
Angeacha lijadiliwe..kwani shida ipo wapi?hii ndio mojawapo ya kazi za bunge...amepwaya.
 
Naibu spika ana kosa gani hapo? Waziri kesha toa maelezo kuhusu kurudishwa nyumbani hao wanafunzi ....na maelezo hayo yanaeleweka tatizo liko wapi? Na hawakufukuzwa wamerudishwa kwa muda wkt tatizo lao linapatiwa ufumbuzi wa kudumu.Muacheni naibu spika afanye kazi yake
kutoa maelezo ni jambo moja lakini kutoa maelezo ya kina na yenye mantiki kutokana na uzito wa jambo lenyewe ni jambo lingine.....naamini mtu yoyote aliyefuatilia maelezo ya waziri atakubali hayakujibu maswali muhimu je wanafunzi walikua na kosa gani kupewa masaa 24 tu wawe wametoka eneo la chuo? kama ni muhimu waondoke mpaka mgogoro uishe je ilizingatiwa uwezo wao wa malazi na usafiri wa ghafla hivyo kurudi makwao?hao wakufunzi walikua na madai gani ni msimamo wa serikali ni kiasi gani? nk
 
Naibu spika wa bunge la Tanzania mama Tulia Atson ni msomi mzuri na mbobezi wa sheria lakini tangu mchakato wake wa kugombea kiti hicho na kipindi uongozi wake katika bunge umeendelea kuzua maswali kuhusu uwezo wake wa kiuongozi hasa kuongoza chombo hicho muhimu chenye misuguano mingi ya kisiasa.
Hivi leo katika suala la wanafunzi wa ualimu UDOM bungeni na uamuzi wake wa kupinga hoja ya kua na mjadala wa dharura anazidi kuacha maswali mengi:
-Je alishindwa kuona udharura wa suala la wanafunzi kufukuzwa na kupewa masaa 24 tu wawe wametoka eneo la chuo?
-Je hakuona umuhimu wa kuibana serikali kutoa maelezo zaidi hasa ukizingatia suala la kuwalipa walimu halikua jukumu la wanafunzi hivyo kuwafukuza kwa ghafla kama ni wakosaji ni uonevu?
-Katika nafasi yake ya mwanasheria(mbobezi) hakuona kuna uvunjifu wa haki za kibinadamu kuwapa siku 1 wawe wameondoka bila kuzingatia hali ya malazi, chakula na nauli kwa kosa ambalo si lao?
-Je alijiridhisha kwamba serikali ilikua imetoa maelezo ya kina kuhusu utatuzi wa mgogoro huo,lini utaisha na wanafunzi kurudi chuoni?

Kwa muda wote wa uongozi wake ndani ya bunge ameonyesha udhaifu mkubwa wa kiuongozi na maamuzi yanayozua sintofahamu bungeni hivyo kuthibitisha hofu walikua nayo watu wengi tangu wakati za mchakato wa uchaguzi wake.
Ikumbukwe kua hapo kabla alikua naibu mwanasheria mkuu wa serikali(executive) akachukua fomu ya kugombea uspika na kushindwa kisha akachuka fomu ya unaibu spika na kuteuliwa ubunge na rais haraka haraka ili apate sifa ya kuwa mgombea huku wagombea wengine "wakilazimishwa"wajitoe.
Hii yote ilitia hofu kwamba angeenda kuwa kibaraka wa serikali kudhibiti bunge ili lisiwe na meno na tukio la leo linazidi kudhihirisha hofu hiyo ilikua na msingi sana na kuathiri mfumo wa kibunge wa jumuiya ya madola tunautumia ambao bunge ndio chombo kikuu cha uwakilishi wa wananchi na kusimamia serikali.

Mdau mleta hoja naafikiana na wewe kwa asilimia nyingi!

Ni ukweli ulioko wazi kuwa huyu mheshimiwa kasi na viwango vya kuliendesha bunge vimemtoa knock-out.

Hapa kuna hypothesis naziona ziko bayana kwa huyu 'anointed' wa mhimili mkuu;
-Either udaktari wake wa sheria alio nao ni wa 'makaratasi' ila ukija kwenye actual performance ni utata mtupu, au anao uwezo wa kufanya kazi ila kutokana na 'power from above' ndo kusema inabidi aburuze mambo yawe hobelahobela ili asije tia mchanga kitumbua chake.

Hata hivyo kuna mambo mengine ambayo hayahitaji ubobezi,ni common sense tu,say ukimsikia namna anavyo wa-treat watu ambao ni wazee kuliko yeye utajua kua huyu ni 'mzungu mweusi' hata namna ya kuwapa heshima wakubwa zake kwa Umri ni mzozo,yote kwa yote tusingefikia kuunganisha nukta kama angekidhi haja yetu ya kuliongoza bunge katika njia ipaswayo,na kwa nature ya bunge la vyama vingi asipoangalia ataendela kuwa kituko, na kwa ushauri wa bure tu asipangwe kusimamia kiti siku ambayo kuna mada nzito ambazo hatazimudu.

Hii inasikitisha kuona wasomi kama hawa wanavyoshindwa kusoma alama za nyakati na kubalance mambo matokeo yake wanaangukia kwenye intellectual arrogance bila kutumia busara ili kuisaidia Taifa.
 
Naibu spika anakurupuka ndo tatizo lake haishughulishi halmashauri ya kichwa chake
 
Nilitamani Mussa Zungu awe naibu spika sababu nilijua akiongoza bunge anakuwa fair yaani hana upendeleo na ana uwezo wa kutoa maamuzi yanapoletwa kwenye kiti na alionekana kipindi alipokuwa mwenyekiti wa bunge
 
Vyeo vya kugawiana kama njugu matokeo yake ndiyo hayo yanayoonekana.
Hi hi TZ sa hii ni km gari isiyo na dereva... Fujo kila kona hakuna muangilio wa mambo oyeeeeeeeeerrr... Ngoma inogile Nacheka na naona haya Kabisa Kuna watu wanaishi kwa matumaini
 
Naibu spika wa bunge la Tanzania mama Tulia Atson ni msomi mzuri na mbobezi wa sheria lakini tangu mchakato wake wa kugombea kiti hicho na kipindi uongozi wake katika bunge umeendelea kuzua maswali kuhusu uwezo wake wa kiuongozi hasa kuongoza chombo hicho muhimu chenye misuguano mingi ya kisiasa.

Hivi leo katika suala la wanafunzi wa ualimu UDOM bungeni na uamuzi wake wa kupinga hoja ya kua na mjadala wa dharura anazidi kuacha maswali mengi:
-Je alishindwa kuona udharura wa suala la wanafunzi kufukuzwa na kupewa masaa 24 tu wawe wametoka eneo la chuo?

-Je hakuona umuhimu wa kuibana serikali kutoa maelezo zaidi hasa ukizingatia suala la kuwalipa walimu halikua jukumu la wanafunzi hivyo kuwafukuza kwa ghafla kama ni wakosaji ni uonevu?

-Katika nafasi yake ya mwanasheria(mbobezi) hakuona kuna uvunjifu wa haki za kibinadamu kuwapa siku 1 wawe wameondoka bila kuzingatia hali ya malazi, chakula na nauli kwa kosa ambalo si lao?

-Je alijiridhisha kwamba serikali ilikua imetoa maelezo ya kina kuhusu utatuzi wa mgogoro huo,lini utaisha na wanafunzi kurudi chuoni?

Kwa muda wote wa uongozi wake ndani ya bunge ameonyesha udhaifu mkubwa wa kiuongozi na maamuzi yanayozua sintofahamu bungeni hivyo kuthibitisha hofu walikua nayo watu wengi tangu wakati za mchakato wa uchaguzi wake.

Ikumbukwe kua hapo kabla alikua naibu mwanasheria mkuu wa serikali(executive) akachukua fomu ya kugombea uspika na kushindwa kisha akachuka fomu ya unaibu spika na kuteuliwa ubunge na rais haraka haraka ili apate sifa ya kuwa mgombea huku wagombea wengine
"wakilazimishwa"wajitoe.

Hii yote ilitia hofu kwamba angeenda kuwa kibaraka wa serikali kudhibiti bunge ili lisiwe na meno na tukio la leo linazidi kudhihirisha hofu hiyo ilikua na msingi sana na kuathiri mfumo wa kibunge wa jumuiya ya madola tunautumia ambao bunge ndio chombo kikuu cha uwakilishi wa wananchi na kusimamia serikali.

Yaani Tanzania bwana, mi wala siielewi tu. wasomi wa nchi hii ndiyo wanaoharibu nchi kwa uongozi wao wa kijinga. Usikute huyu spika hajuwi wajibu wake japo kasomea sharia. Kwa kweli huyu bi dada yabidi atumbuliwe maana she's too useless na incompetent.
 
ukipata cheo ndani ya ccm akili yako unaweka kando kwanza. huyu mama ni mteule wa magogoni hapo anaiwakilisha serikali bungeni na sio bunge kama mhimili...
Kwa hiyo Tulia kashindwa kutulia sababu akili kaicha nyumbani inetulia na haitumiki mpaka mkutano wa bunge uishe!

Mama najua umeamua kustaafu siasa za nyumbani kwako ukiwa bado una nguvu ya kutosha lakini bado mchango wako unahitajika sana hasa kwa ustawi wa masuala mazima ya bunge, kiti cha sasa kinapwaya zaidi awapo Mwanamke mwezio, mchango wako mama unaweza kujenga zaidi, wewe ni mfano wa kuigwa katika weledi wa kuendesha bunge na umeacha pengo ambalo linaonekakana gumu kuzibika.

Tafadhali mama yangu mwite kijana wako mwanamke na mwanachama mwezio mpe darasa mambo yanamwndea Kombo, mwelekeze namna ya kua mvumilivu kama kiongozi anayeweza kua na uwezo wa kutumia mizani vizuri awapo katika kiti chake.Sipendi sana kuona mwanamama akilalamikiwa sana kwa utendaji wake, mfunde namna ya kuchuja hoja zenye maslahi ya kitaifa na zisizokua na maslahi ya kitaifa, mfunde namna ya kusikiliza hata kama anona ni pumba maana kila mtu anayo haki ya kutoa hoja na kusikilizwa, mwele atambue kua anaongoza kila aina ya kichwa na asili yake.Mwambie ifike mahali apime upepo kulingana na aina ya tukio linalotolewa hoja,Mfunde namna ya kutafuta suluhu kwa mazungumzo na maridhiano kama ulivyokua ukifanya wewe maana ubabe hua una kikoma.

Ni rai yangu kua wewe kama malkia wangu wa nguvu utatumia busara na hekina zako kuweka baadhi ya mambo sawa pindi unapoona hayaendi sawa ikikubidi. Najua kaka yangu Ndungai anao uwezo huo lakini naona pengine darasa lake bado halijamkolea kijana huyu mwanamama maana naamini pia kwa Ndungai kuna kitu ulimwachia kwa muda wote ulipokua pamoja nae.
Uongo mbaya kwa sasa tunamkumbuka huyo mama maana alikuwa ana uma na kupuliza kama panya, lkn huyu ni kuuma na kutafuna kama simba
 
Mkuu huu ni ushauri mzuri sana na pia nakusifu kwa jinsi ulivyo pangilia
 
Hawana tofauti na moderator wa humu, kila mada wana delete tunakoelekea hii forum itakuwa haina maana coz now inapoteza mvuto kadri siku zinavyozidi kusonga. Zitabakia posts za udaku tu. #Freedom of speech mkini piga ban i don't care
 
Udhaifu wa Tulia ndio udhaifu wa aliyempendekeza na kumsimamia apate cheo hicho. Tusipende kuficha ficha maradhi kilio kitatuumbua.
Aliyempendekeza na kushinikiza ndiyo anayeomba kila siku tumuombee, sasa kila mtu amuombee anavyoweza.
Mimi namuombea aache kutumia BmW za mkwere atumie bajaj na nyie endeleeni kumuombea kivyenu
 
Back
Top Bottom