Udhaifu katika katazo la kuuza vyakula mchana wa ramadhani Zanzibar

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
11,192
15,887
Mbali na kuzuwiwa kwa vyakula kuuzwa mchana wa ramadhani katika baadhi ya maeneo, lakini bado zuio hili halijatendewa haki.

Waislamu tunaamini kwamba ukifunga basi hata ukila ile punje ya karanga tu na ukameza kwa makusudi basi umefungua sio mpaka ule biriani au urojo bakuli zima.

Sasa ni jambo la ajabu sana kuona kuna baadhi ya vyakula eti ruhusa kuuza kama vile:
  • Ndizi
  • Karanga
  • Mapapai
  • Korosho
  • Machungwa
  • Matikiti ambayo mengine yameshakatwa tayari kwa kuliwa.
  • Maji pia yanauzwa.
  • Juisi aina zote zinauzwa madukani.
-Biskuti zinauzwa madukani na vitu vingine vingi achilia mbali vitu hivyo.

Lakini vyakula vya kupikwa vimezuiwa kabisa na migahawa imefungwa kabisa.

Mimi naona hii haiko sawa kwa sababu orodha ya vyakula nilivyotaja pia mtu akila anafungua kwa hiyo navyo ilikuwa vizuiliwe kuuzwa ama maduka yafungwe kama ambavyo migawaha imefungwa.

Siku za kawaida tunawaona watu wanakunywa maji hadharani hivyo na maji ilikuwa yapigwe marufuku yasiuzwe ama maduka yanayouza maji yafungwe.

Siku za kawaida watu hula hadharani karanga,hivyo na karanga ilikuwa zizuiwe zisiuzwe.

Siku za kawaida watu hula ndizi hadharani hivyo ilikuwa na vibanda vya matunda vipigwe marufuku lakini hawa wauza matunda ndio utawakuta wanalalamika endapo migahawa haifungwi kana kwamba wao hawauzi vyakula.

Na vinywaji vingine vyote vinavyouzwa madukani tunaona kabisa vinywaji hivyo hunywewa katika siku za kawaida.

Hivyo ilikuwa maduka yanayouza vinywaji yafungwe kama ambavyo migahawa imefungwa.

HOJA WANAYOTUMIA

HOJA: Eti migahawa inauza vyakula vya kula hapohapo yaani wanaandaa ili kiliwe kwa nyakati hizo.

JAWABU: ndizi, embe, korosho, mapapai, na machungwa maji, juisi, biskuti n.k haya yote yapo tayari kuliwa muda wote na wala hayajapigwa marufuku ama kufungwa maduka, hivyo sio sawa na maduka yafungwe pia.

Kama itasemwa kwamba migahawa watu wanakula hapo hapo nddio maana wamezuia basi wangekataza tu kwamba watu wasile migahawani lakini migahawa ipike vyakula, kidoogo ingemake sense japokuwa tungehoji zaidi.

Imagine familia yote imefunga alafu kuna mgonjwa ana vidonda vya tumbo, sasa badala ya mama kusumbuka kupika huku amefunga si angetoa pesa tu kwendakununjua chakula akarahisisha?

Huu utaratibu uangaliwe upya na kufanyiwa maboresho katika hayo maeneo ambayo taratibu hizo zipo.

Kusoma zaidi kuhusu katazo la kula mwezi wa ramadhani pamoja na marufuku nyingine Zanzibar soma:
 
Huo ni ukorofi na ni uvunjifu wa haki na amani kwa watu wengine wasioamini imani na dini hiyo, kama wanaona mungu wao anawaamrisha wafunge, wafunge tu sio kutaka watu wengine wasile mchana huko ni kuingilia uhuru wa wengine
 
Mbona ile imani nyingine wana mfungo wao lakini hawaathiri wengine wasioamini huko na hata wanaoamini hawashurutishwi kufunga? Mambo ya dini na imani ni hisia za mtu au kikundi cha watu fulani, wasitake kuathiri maisha ya watu wasioamini dini na imani yao
 
Mbona ile imani nyingine wana mfungo wao lakini hawaathiri wengine wasioamini huko na hata wanaoamini hawashurutishwi kufunga? Mambo ya dini na imani ni hisia za mtu au kikundi cha watu fulani, wasitake kuathiri maisha ya watu wasioamini dini na imani yao
Kule Kuna mfungo ndugu yaanguu!!!?
 
Tunafunga ndiyo siku 40

Lakini maelekezo ni kuwa Funga kiroho (bila kujionesha kuwa umefunga) kwa maana kufunga ni ibada na imani.

Mtu aliyefunga kwa imani na kiroho hawez kutamani kula hata akiona chakula
Unafunga like unachokipenda,maji unakunywa,ndiyo umefunga nini!!?...na Nani kafunga akamwambia anatamani au anajionesha!?
 
Mtaumia sana watu wanaendelea na maisha yao, hizi mada kila siku inashushwa, mada ileile inatofautiana vichwa vya habari tu.

Wakristu wamekua watu wa kunung'unika juu ya uislamu, Kama ilivyo yanga, Wanavyonukia Simba.

Makanisa ya kilokole waingiapo makanisani wakimaliza kulia, kinachofuata kucheza mziki na baada ya hapo ni shuhuda na kuzituhumu imani zingine.
Hawa wanaoandiki hizi habari kila Siku ni wale wanajiita walokole.
 
Back
Top Bottom