Uchambuzi: Prof. Kabudi anaweza kuongea wakati wa kula?!

Kama ni Profesa wala tusijali kwani hawana msaada kabisa kwa nchi na wengine wamekuwa vichefuchefu! mfano ni yule 'propesa' aliamua kuweka 'makazi bgrn malapa'.
 
kama wewe ungeteuliwa ungeongea wakati unakula?
Kama wewe uliimba lowasa fisadi akiwa CCM alivyohamia chadema ukaimba siyo fisadi na ni rais wako wa moyoni ndiyo itakuwa huyo Profesa kwani yeye hana njaa?
Ila njaa za hawa maprofesa ni zaidi ya njaa! nafikiri ni utapiamlo! si wamuona yule aliyehamia Bgrn malapa?
 
Yawezekana kuna harufu mkulu aliisikia akaona amzibe mdomo mapema.sababu ukiangalia wale waliokuwa na misimamo tofauti na ccm ndiyo anawachagua ili wasiweze kuongea
 
kama wewe ungeteuliwa ungeongea wakati unakula?
Kama wewe uliimba lowasa fisadi akiwa CCM alivyohamia chadema ukaimba siyo fisadi na ni rais wako wa moyoni ndiyo itakuwa huyo Profesa kwani yeye hana njaa?
kama wewe ungeteuliwa ungeongea wakati unakula?
Kama wewe uliimba lowasa fisadi akiwa CCM alivyohamia chadema ukaimba siyo fisadi na ni rais wako wa moyoni ndiyo itakuwa huyo Profesa kwani yeye hana njaa?
Ukiwa si mchezaji ukamkosoa anayecheza uwanjani watu watakwambia kacheze wewe kama unamuona yule anakosea! bado unaweza kuwajibu kuwa me sijui kucheza ndo maana sijaenda na yeye asingeenda kucheza angewaacha wanaojua nisingemkosoa.
 
Niache mie nikajilie ugari wangu...Kamwe hawezi kukosoa maana ata kabla ya uteuzi bado alikua kimya mfano katazo haramu la mikutano ya kisiasa
 
Kama tunavyofahamu Guru wa Sheria na aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Katiba Mpya Prof.Kabudi Palamagamba ameteuliwa kama mbunge wa viti maalumu.

Uteuzi huu ni mwendelezo wa kuteuliwa kwa waliokuwa wajumbe wa tume ya katiba,awali akiteuliwa Bwn.Polepole na kufuatiwa Mwenyekiti Warioba kuwa mwenyekiti wa moja ya bodies

Kutokana kumbukumbu zilizopo kwa wateuliwa wa rais huweka kando misimamo na weledi wao na kuwa kitu kimoja na mteuaji!Ajabu hii hufanyika pia hata kwa wanasheria wasomi. Tumeshuhudia Dr.Mwakyembe akinukuu katiba na sheria kinyumenyume. Sote tulisikia akisema katazo la mikutano ya kisiasa na maandamano ni kwa mujibu wa katiba lakini mpasa sasa hajawahi kunukuu kifungu cha katiba wala sheria......list ni ndefu

Ni kwa nini tusiamini kuwa Prof.Kabudi hatakuwa anaongea wakati wa kula?! Kama yamewezekana kwa Dr.Ayubu Rioba,H.Polepole kwa nini isiwe kwa Prof.Kabudi?Tutegemee toka kwa muumini wa katiba Prof.Kabudi kwamba katiba sio kipaumbele tuache rais anyooshe nchi kwanza? Serikali tatu je?

Maono yangu yanaonyesha Prof.Kabudi anaenda kuteuliwa kuwa waziri wa sheria na katiba baada ya Dr.Mwakyembe kutokuonyesha dira yeyote! Je waziri mtarajiwa huyu atawezaje kufunguka na matonge mdomoni?

Wadau mnifikishie
Mkuu, sio viti maalum.

Viti maalum huwahusu akina mama pekee na mchakato wake hufanywa ndani ya vyama husika. Prof. Kabudi kuteuliwa katika zile nafasi kumi ambazo Rais amepewa kikatiba. Ni Mbunge wa kuteuliwa na si viti maalum.
 
Mimi nikajua ni kwasababu huwa ananyesha vibaya mno wakati wa kuongea. Jamaa ananyesha na ukiwa naye karibu unaweza kulowa kama umenyeshewa mvua..! Kumbe umeongea kinyumenyume mkuu!!! Basi sawa.
 
kama wewe ungeteuliwa ungeongea wakati unakula?
Kama wewe uliimba lowasa fisadi akiwa CCM alivyohamia chadema ukaimba siyo fisadi na ni rais wako wa moyoni ndiyo itakuwa huyo Profesa kwani yeye hana njaa?

Hebu tuwe wakweli; tuache ushabiki.

Hivi kama Lowasa ni fisadi, ni kitu gani kinazuia vyombo vya dola kumchukulia hatua stahiki?!
 
Chadema walisema ni fisadi wakati akiwa CCM wakamtangaza kwenye orodha ya aibu.
Kwahiyo waliosema Lowasa fisadi ni Chadema siyo serikali wala CCM.
Siku chadema wakipata urais watamfikisha mahakamani.
 
Mimi nikajua ni kwasababu huwa ananyesha vibaya mno wakati wa kuongea. Jamaa ananyesha na ukiwa naye karibu unaweza kulowa kama umenyeshewa mvua..! Kumbe umeongea kinyumenyume mkuu!!! Basi sawa.

Mkuu mambo mengine uwe unakausha basi...hilo yatizo kweli analo pia anakuwaga na ute ute mweupe kwenye angle za mdomo...hili tatizo nilishawaona watu kadhaa wanalo...la kunyesha duuu Jamaa ni noma...hili nalo Sijui ni la kigenetik maana....duuu ngoja nijinyamazie mie..
 
Maproo wengi in waganga njaa, wakishateuliwa huwa kimya. Wale vizuri. Ole wao! Mwl alitoaga mfano Wa mkulima kutumwa na kijiji kitafuta chakula wakati Wa njaa, sijui kama wasomi wetu wanasomaga nasaha za Mwl.
 
Toka lini na wewe ukawa mtabiri? tuache siasa kwenye professional.

Prof Kabudi ni mtu makini sana na alistahili kuwa hapo ili alitumikie Taifa letu. Tumuunge mkono bila kujali itikadi ya vyama vyetu
 
Kama tunavyofahamu Guru wa Sheria na aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Katiba Mpya Prof.Kabudi Palamagamba ameteuliwa kama mbunge wa viti maalumu.

Uteuzi huu ni mwendelezo wa kuteuliwa kwa waliokuwa wajumbe wa tume ya katiba,awali akiteuliwa Bwn.Polepole na kufuatiwa Mwenyekiti Warioba kuwa mwenyekiti wa moja ya bodies

Kutokana kumbukumbu zilizopo kwa wateuliwa wa rais huweka kando misimamo na weledi wao na kuwa kitu kimoja na mteuaji!Ajabu hii hufanyika pia hata kwa wanasheria wasomi. Tumeshuhudia Dr.Mwakyembe akinukuu katiba na sheria kinyumenyume. Sote tulisikia akisema katazo la mikutano ya kisiasa na maandamano ni kwa mujibu wa katiba lakini mpasa sasa hajawahi kunukuu kifungu cha katiba wala sheria......list ni ndefu

Ni kwa nini tusiamini kuwa Prof.Kabudi hatakuwa anaongea wakati wa kula?! Kama yamewezekana kwa Dr.Ayubu Rioba,H.Polepole kwa nini isiwe kwa Prof.Kabudi?Tutegemee toka kwa muumini wa katiba Prof.Kabudi kwamba katiba sio kipaumbele tuache rais anyooshe nchi kwanza? Serikali tatu je?

Maono yangu yanaonyesha Prof.Kabudi anaenda kuteuliwa kuwa waziri wa sheria na katiba baada ya Dr.Mwakyembe kutokuonyesha dira yeyote! Je waziri mtarajiwa huyu atawezaje kufunguka na matonge mdomoni?

Wadau mnifikishie
Hii nchi ni laana.Waandishi kama makasuku kesho wanajaza habari kuwa ni wanasheria wa dunia.
 
Back
Top Bottom