Kitendo cha Kamati Kuu ya CCM chini ya uenyekiti wa Dokta (asiye na PhD) Jakaya Kikwete kupitisha majina matatu ya wanawake pekee na kulazimisha Spika ajaye awe mwanamke kwa kutumia wingi za kura za wabunge wa CCM ni ukiukwaji wa haki za binadamu.
Katiba ya Tanzania na katiba ya CCM yenyewe zinatamka bayana kuwa binadamu wote ni sawa (kama alivyosema JF Senior Expert Member Kiranga kwenye mchango wake hapa JF.)
Hivyo basi, kitendo cha CCM kuwabagua wagombea wengine na kuwazuia wasigombee kwa kuangalia jinsia zao tu ni kinyume kabisa na katiba ya nchi inayotamka kuwa binadamu wote ni sawa.
Hata kama ni lengo ni zuri la "affirmative action" lakini huwezi kuvunja katiba na kunyima watu haki zao za msingi kwa kusingizia 'women empowerment'. CCM iwe jasiri na kueleza sababu halisi za uamuzi wake.
Makamba aliwaambia waandishi wa habari kuwa Spika wa Bunge aliyemaliza muda wake, Samuel Sitta, ni shupavu na mchapa kazi, lakini kosa lake ni moja tu - si mwanamke.
Hii dhambi ya jinsia ni sumu kama ubaguzi wa wagombea kwa kuangalia dini au kabila yao.
Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, katika moja ya hotuba yake maarufu alitoa mfano wa kiongozi mmoja mwenye sifa zote lakini akakataliwa kwa sababu moja tu -- kabila lake Mkara.
Hivyo basi CCM wanasema Sitta ana sifa zote safi za kuwa kiongozi, tatizo lake moja tu -- mwanaume.
Natoa wito kwa Wabunge wa CCM wapinge ubaguzi huu wa kijinsia na uvunjaji wa katiba uliofanywa na chama tawala kwa kumpigia kura mgombea wa upinzani awe Spika ili kuonesha hasira zao.
CHADEMA SI MUMCHUKUE SITA. Kwani tabu iko wapi, wao wameamua kubadili safu na nyie pangeni ya kwenu.
Vyanma vingine si vielewi kabisa, baada ya kueleza ushupavu wa MABERE MARANDU mnakimbilia kuwakosoa ccm.
AAAH kweli hata kutoshirikiana kwa vyama vya upinzani ni dhambi ya CCM!!!!!!