Uchaguzi mdogo Majimbo ya Konde na Ushetu kufanyika Oktoba 9, 2021

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,880
6,366
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema Uchaguzi Mdogo katika Majimbo ya Konde (Mkoa wa Kaskazini Pemba) na Ushetu (Shinyanga) utafanyika Oktoba 09, 2021

Wagombea watachukua fomu kuanzia 13-19 Septemba, uteuzi utafanyika Septemba 19 na Kampeni zitaanza 20 Septemba hadi 08 Oktoba

Jimbo la Konde lipo wazi baada ya Mbunge Mteule kujiuzulu na aliyekuwa Mbunge wa Ushetu na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa , Elias John Kwandikwa alifariki dunia Agosti 02

2.jpg

1.jpg
 
Namuona Mzee masifa akichukua form Ushetu wanamuira Chief basi sawa njaaa imemshika kidogo anapambana arudi amalizie dak zilizobakia.
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo ineyangaza mchakato wa Uchaguzi katika Majimbo ya Ushetu mkoani Shinyanga na Konde Mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo Uchaguzi huo umepangwa kufanyika Oktoba 9,2021.
IMG_20210827_165511_059.jpg
IMG_20210827_165516_128.jpg
 
Back
Top Bottom