Nature
JF-Expert Member
- Nov 5, 2014
- 814
- 2,184
Malasusa amepata kura 167 ambazo ni asilimia 64 ya kura zote zilizopigwa
Askofu Malasusa alikuwa anagombea dhidi ya askofu Abednego Keshomshahara wa Dayosisi ya Bukoba aliyepata kura 73 na Askofu Dr George Fihavango wa Dayosisi ya Njombe aliyeshindwa katika duru ya kwanza.
Hii itaakuwa ni mara ya pili kwa Askofu Malasusa kuwa mkuu wa kanisa la Kiinjili la Kiliteri Tanzania (KKKT) tangu alipochaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2007, hadi mwaka 2015 ambapo alimuachia kijiti askofu Fredrick shoo ambaye ameongoza kwa kipindi cha miaka nane.
Hongera Askofu Malasusa, Hongera KKKT.
---
Mkutano Mkuu wa 21 wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) umemchagua Askofu Alex Malasusa kuwa mkuu mteule wa KKKT.
Askofu Malasusa wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani anachukua nafasi ya Askofu Fredrick Shoo aliyemaliza muda wake wa uongozo wa awamu mbili.
Anarejea tena kwenye nafasi hiyo aliyoihudumu kuanzia 2007-2015 alipomaliza na nafasi yake ikiongozwa na Askofu Shoo.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo mwenyekiti wa uchaguzi huo,Askofu Amon Mwenda,amesema kura zilizopigwa zilikuwa 241 ambapo kati ya hizo Malasusa amepata kura 167 sawa na asilimia 69.3 huku Askofu Abednego Kesho Mshahara akipata kura 73 sawa na asilimia 30.3
Askofu Malasusa alizaliwa Aprili 18, 1961; katika kijiji cha Kiwira Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya.
Ni mtoto wa pili katika familia ya watoto nane ya Marehemu Mchungaji Gehaz Japhet Malasusa na Subilaga Timoth Malasusa.
Askofu Malasusa amewahi kuwa Mkuu wa Kanisa kwa miaka 8 tangu 2007 hadi 2016 na Mkuu wa Chuo Kikuu Tumaini Makumira kwa kipindi chote.
Mstari wa Biblia anaoupenda ni Yohana 3:30 ‘’Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua.’’