BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,817
Uchunguzi wa kundi la kwanza la masanduku 9 kati ya 15 ya kura zilizoagizwa kuhesabiwa upya na Mahakama ya Juu haukuweza kuonesha hitilafu zozote za wazi katika matokeo ya uchaguzi wa Urais.
Wakati wa kuchapisha, ni masanduku tisa pekee kati ya 15 ya kura yalikuwa yamefunguliwa, kuchunguzwa na kura kuhesabiwa upya katika zoezi ambalo lilisimamiwa na msajili wa Mahakama ya Juu, Bi Letizia Wachira, na wafanyakazi wake.
Masanduku hayo tisa yalikuwa ya shule za msingi za Majengo na Mvita kaunti ya Mombasa.