Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 59
Chuma,
Unataka mpaka watangaze kwenye kwenye gazeti la Uhuru, ndio ujue wanafanya la maana?
Ukifikiria kufanya ya maana kuna maana ya kusaidia Tanzania yote, hapo sahau. Maendeleo ya Tanzania yanakuja pale mtu mmoja mmoja, familia moja nk zinapofanya jambo lolote la maendeleo.
Kama mtu anasomesha familia yake, anawatunza wazazi wake, tayari kafanya la maana kwa nchi. Maendeleo ni sum total of contributions by individuals in the country concerned. Hii sum total inachangiwa na watu mbalimbali kuanzia mipango ya serikali mpaka mipango ya mtu mmoja mmoja.
Pia sio kila mtu lazima asaome, wasomi na wasio soma wote wana nafasi ya kuchangia maendeleo ya Tanzania. Mbeba box anaweza kuchangia zaidi kuliko msomi fisadi anayehamisha pesa toka TZ na kuzificha nje. Mtu akiona hana uwezo au hataki kusoma sio mwisho wa maisha,kuna njia nyingine chungu nzima za kuweza kujisaidia yeye na familia yake.
JF imejaliwa watu wenye hoja hadi inapendeza. Asante sana Mtanzania kwa hii analysis.