Ubalozi Malaysia, Wizara mambo ya nje na mambo ya ndani Tanzania fanyeni kazi zenu badala ya kula raha ofisini

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,260
2,889
Naomba wizara hizi turekebishane. Kuna mambo ya kifilauni yantendeka ndani ya wizara.

Nasikia baadhi ya mabalozi wanateuliwa ili kulea na kusomesha watoto wa waliowateua huko nje ya nchi. hii imeleta tabia ya kiburi na kutowajibika na mambo ya wa-TZ wa kawaida ktk nchi wanazowakilisha.

Kuna taarifa inazunguka mitandaoni ikionesha pass ya kusafiria ya mwanamke ambaye inasemekana anateseka nchini Malaysia kwa matatizo ya akili. Je hakuna balozi? Je hajisikii kufuatilia matatuizo ya aina hiyo? Ubalozi wa Afrika Kusini, tuliwasifu sana kwa kufuatilia.

Kinachofahamika kwa muda mrefu, kuna uharifu unaofanywa na makundi ya wa-TZ walioko nje na ndani ya nchi ambayo yanawashawishi mabinti kwenda kutafutiwa kazi nje ya nchi. Malaysia ni moja ya nchi hizo. Makundi hayo yanahusisha mambo ya ndani, watoaji wa passport za kusafiria.

Mabinti wanapofika huko wanalazimishwa na Wa-TZ wenzetu kuingia kwenye umalaya wa kitumwa, wakiwa ugenini, bila ndugu na pass zao hunyang'anywa. Hawa ni mabinti wema wanaojikuta ktk mtego wa waharifu. Waharifu hao hata siku moja hawahangaiki na 'Changudoa' wa hapa, wanawinda wasichana wanaojifahamu na ndo maana wengi, kwa kutotegemea hali hiyo wnaharibikiwa na akili.

Naamini kabisa ubalozi wetu Malaysia wanafahamu, lakini wako kimya tu. hawatoi taarifa muhimu kama hiyo ili wasichana wasiingie ktk mtego wa waharifu hao. Hawatoi hata taarifa za wa-TZ ambao wanafanya biashara hiyo haramu na dhalili, maana wanarudi nyumbani kama watu wema kumbe ni waharifu. Mambo ya ndani wanasaidia sana kutoa pass za safari tena kwa haraka, kwa faida binafsi, huku wakifahamu wenye pass hizo wataingia matatizoni.

1726567528811.png

We unafikiri hao wanawake wanao safirishwa huko hawajui
Nini wanaenda kufanya/shuguli gani huko

Ova
 
Tatizo la kuteua machawa kwenye nafasi zinazohitaji wataalam na weledi
 
View attachment 3098208
Tatizo la kuteua machawa kwenye nafasi zinazohitaji wataalam na weledi
Ni kweli kabisa kwamba Mabalozi wa Tanzania waliopo huko nje Wengi wao wana matatizo makubwa Sana hususani katika kuwahudumia raia wa Tanzania waliopo huko nje ya nchi kwenye nchi wanazohudumu, lakini kwa upande mwingine hata baadhi ya wa-Tanzania wenzetu huko nje huwa hamtekelezi wajibu wenu mkiwa huko ughaibuni. Mnatakiwa kutii Sheria za wenyeji ili Mabalozi au Maafisa wa Ubalozi waweze kuwasaidia pale mnapokwama na pale panapohitaji usaidizi kutoka kwa Ofisi ya Balozi wa nchi. Aidha, wa-Tanzania lazima mtambue wajibu wenu mkiwa huko ughaibuni sambamba na kuyatambua malengo yenu ya awali kabisa yaliyosababisha nyie kuamua kwenda kuishi huko nje ya nchi.
 
Ni kweli kabisa kwamba Mabalozi wa Tanzania waliopo huko nje Wengi wao wana matatizo makubwa Sana hususani katika kuwahudumia raia wa Tanzania waliopo huko nje ya nchi kwenye nchi wanazohudumu, lakini kwa upande mwingine hata baadhi ya wa-Tanzania wenzetu huko nje huwa hamtekelezi wajibu wenu mkiwa huko ughaibuni.
Wengi wa Mabalozi na staff wao ni wale walioshindwa kutimiza wajibu waona wakatupwa huko kama demotion kisaikolojia.
 
Back
Top Bottom