Twaha Mwaipaya: Namna ya kujilinda katika nyakati hizi za watu wasiyojulikana

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
14,987
31,239
1. Usipende kuwasha location ya simu yako kila mara.

2. Usipende kutembea mwenyewe nyakati za usiku.

3. Hakikisha kabla hujalala kuna mtu umempa taarifa au umemtakia usiku mwema na amejua upo wapi.

4. Wakija watu kukukamata hata wakijitamburisha kwamba wao ni Polisi hakikisha kuna mtu amejua, wakitaka kukuchukua kwa nguvu lia kilio cha kufiwa na mama.

5. Ukitongozwa na Binti au Binti akijilengesha kirahisi kaanae mbali.

6. Rafiki yako akikupigia simu mkutane, hakikisha kuna mtu amejua, anaweza akakamatwa yeye ili wakupate wewe.

7. Usipende kununua Luku kwa njia ya simu kwani, watekaji wana uwezo wa kujua unaishi maeneo gani kirahisi zaidi.

8. Ukipita maeneo ukiwa na mashaka chukua simu mpigie mtu uwe unatembea huku unaongea nae ukigushwa tu, mwambie huyo mtu kwamba unatekwa.

9. Usiishi kama mfu, muombe Mungu, pia ishi vizuri na watu watakusaidia siku moja.

UTAJUAJE KAMA UNAELEKEA KUPOTEZWA.

1. Hata kama umekamatwa na watu waliojitamburisha kwamba ni Polisi ila ukienda kituoni hautaingizwa kwenye reja book.

2. Ukiona umeenda kituo cha Polisi umewekwa chumba cha peke yako na vyumba vingine vikiwa na watu hakikisha ukipata upenyo unatoa ujumbe wakusema wewe ni nani na umetokea wapi, kwani hapo utakua umehifadhiwa tu wazee wa kazi watakuja kukuchukua.

3. Ukipandiswa kwenye gari utafungwa pingu na utawekwa katikati, kulia kwako na kushoto atakaa mtu, tambua haupo salama.

KWA LEO TUISHIE HAPA.
 
Tuna muda kweli wa kuizingatia hayo wakati kila siku ni furahi day aisee. Tuzaliwe Kwa taabu, tusome Kwa taabu, makausha damu yatutese bado Tena uishi Kwa kujibana.. Basi usipende tu kutoka uishi kama introvert na hapo madeal yako mengi yawe ya online ila sio harakati navyozijua
 
Bado..hayo yote uwe umefanya nini mpaka usakwe namna hiyo..???? Ungejikita hapo...hizo ulizoeleza ni matokeo ya kufanya kitu fulani.
Screenshot_20240628_065623_Parallel Space.jpg
 
Bado..hayo yote uwe umefanya nini mpaka usakwe namna hiyo..???? Ungejikita hapo...hizo ulizoeleza ni matokeo ya kufanya kitu fulani.
😂😂😂
Hayajawahi kukukuta wewe, nilishawahi kubebwa na hao watu lakini nilitoa taarifa mapema sana na nikapelekwa Oystebay ya zamani pale, kuanzia Alhamis mpaka Jumatatu nilikuwa ndani. Hiyo kesi yenyewe sasa. 😂😂😂
Chamsingi ni kumtegemea na kumuomba sana Mungu.
 
1.Usipende kuwasha location ya simu yako kila mara.
2.Usipende kutembea mwenyewe nyakati za usiku.
3.Hakikisha kabla hujalala kuna mtu umempa taarifa au umemtakia usiku mwema na amejua upo wapi.
4.Wakija watu kukukamata hata wakijitamburisha kwamba wao ni Polisi hakikisha kuna mtu amejua, wakitaka kukuchukua kwa nguvu lia kilio cha kufiwa na mama.
5.Ukitongozwa na Binti au Binti akijilengesha kirahisi kaanae mbali.
6.Rafiki yako akikupigia simu mkutane, hakikisha kuna mtu amejua, anaweza akakamatwa yeye ili wakupate wewe.
7.Usipende kununua Luku kwa njia ya simu kwani, watekaji wana uwezo wa kujua unaishi maeneo gani kirahisi zaidi.

8.Ukipita maeneo ukiwa na mashaka chukua simu mpigie mtu uwe unatembea huku unaongea nae ukigushwa tu, mwambie huyo mtu kwamba unatekwa.
9.Usiishi kama mfu, muombe Mungu, pia ishi vizuri na watu watakusaidia siku moja.

UTAJUAJE KAMA UNAELEKEA KUPOTEZWA.

1.Hata kama umekamatwa na watu waliojitamburisha kwamba ni Polisi ila ukienda kituoni hautaingizwa kwenye reja book.

2.Ukiona umeenda kituo cha Polisi umewekwa chumba cha peke yako na vyumba vingine vikiwa na watu hakikisha ukipata upenyo unatoa ujumbe wakusema wewe ni nani na umetokea wapi, kwani hapo utakua umehifadhiwa tu wazee wa kazi watakuja kukuchukua.

3.Ukipandiswa kwenye gari utafungwa pingu na utawekwa katikati, kulia kwako na kushoto atakaa mtu, tambua haupo salama.

KWA LEO TUISHIE HAPA.
Kuna njia moja ''local'' isiyo na gharama iwapo umeshikwa na wahusika wanataka kukuingiza kwenye gari kwa nguvu. Piga kelele sana, huku ukiwauma watekaji kwa meno, na pia ukijinyea na kujikojolea.
 
Unapopanda gari ya mtu binafsi unaposafiri kalili namba ya gari tuma ujumbe kwa ndugu zako kisirisiri,
na kama hakuna umuhimu wa kukimbizana usipande gari za private zinazobeba abilia njiani, Kuna mwana Hadi Leo Yuko kwenye kesi ya ujambazi alikamatwa na majambazi menzake wakitokea Moshi,ndani ya gari wakiwa na smg mbili na mapanga kwenye Buti, na nauli alilipa ,hawajui hata majina, alidhani ni abilia wenzake kumbe wazee wa matukio wanawahi dar, wakaona isiwe tabu wachukue abilia ili kujazilizia wese na kupunguza mashaka ya polisi, ,,
 
Bado..hayo yote uwe umefanya nini mpaka usakwe namna hiyo..???? Ungejikita hapo...hizo ulizoeleza ni matokeo ya kufanya kitu fulani.
Unadhani wote waliohukumiwa ni waharifu?
Unaweza ukasakwa na watu wakiangamize kwa sababu ya mafanikio yako, unaweza ukasakwa kwa ajili ya kukemea maovu, au kwa kutetea wengine tu.
Au kwako wewe wote wanaosakwa kwa nguvu kiasi hicho ni waharifu?
 
😂😂😂
Hayajawahi kukukuta wewe, nilishawahi kubebwa na hao watu lakini nilitoa taarifa mapema sana na nikapelekwa Oystebay ya zamani pale, kuanzia Alhamis mpaka Jumatatu nilikuwa ndani. Hiyo kesi yenyewe sasa. 😂😂😂
Chamsingi ni kumtegemea na kumuomba sana Mungu.
Ni vile hatujuani...lakini lazima Kuna kitu ufanye ndio jamaa wakusake kwa style hizo ..amini kwamba jamaa hawana muda na issue ndogo ndogo
 
Unadhani wote waliohukumiwa ni waharifu?
Unaweza ukasakwa na watu wakiangamize kwa sababu ya mafanikio yako, unaweza ukasakwa kwa ajili ya kukemea maovu, au kwa kutetea wengine tu.
Au kwako wewe wote wanaosakwa kwa nguvu kiasi hicho ni waharifu?
Hajui kitu huyo Mpemba na bila kukutwa na misukosuko wewe sio kitu, huwa hafuatilii hata vile Walivyomtesa na kumbambikia kesi Maxence Melo na kutaka hela kibao?
 
Back
Top Bottom