Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 4,955
- 4,329
Rais wetu anakubalika sana kimataifa na ameweza kutufungua kimataifa. Ni rais pekee, executive president, mwanamke barani Afrika na wengi wako tayari kumsaidia ili kuonesha ulimwengu hasa wa Afrika kwamba wanawake wanaweza, tena sana tu kuliko wanaume wengi.
Wengi wanapenda kuona rais wetu anaipaisha kiuchumi na kiusalaama nchi yetu ya Tanzania ili iwe mfano kwa nchi zingine za Afrika ili nazo ziwe zinachagua akina mama kwenye nafasi hizi za ukuu wa nchi. Wakina mama ni wapole, wana huruma, hawapendi vurugu na ni watu makini sana.
Bahati mbaya rais wetu ameingia madarakani kipindi ambacho nchi inakabiriwa na athari kubwa za kiuchumi zilizosababishwa na janga la mlipuko wa covid 19. Pia ni kipindi ambacho mikopo ya fedha tuliyokopa miaka mingi ya nyuma ikawa ndiyo imeiva (mature) na kupaswa kuanza kuilipa. Karibu theluthi moja ya bajeti ya nchi inabidi itumike ku service madeni hayo! Na kama hayo hayatoshi yamezuka madhara ya kiuchumi kutokana na vita ya Russia na Ukraine.
Hizi tunatumaini marafiki zetu waliotukopesha enzi hizo pamoja na benki kama World Bank na African Development Bank watatuelewa na kuweza kuahirisha ulipaji wa baadhi ya madeni hayo kwa angalao miaka mitano. Baadhi yake wanaweza hata kutusamehe kabisa marafiki zetu. Hiki ni kitu cha kawaida ambacho hutokea baina ya mkopaji na mkopeshaji hali inapokuwa ngumu.
Hili likikubalika litatuwezesha kupata karibu TZS 6 trillion kila mwaka kutoka kwenye makusanyo yetu itakayoelekezwa kwenye ujenzi wa miradi mikubwa ya SGR, JNHPP na Chuma cha Liganga - Mchuchuma. Haya yatawezesha nchi yetu kuwa nchi ya viwanda ya mfano kwenye bara la Africa.