Tuwe wazalendo na tuseme ukweli,sitting allowance za wabunge kwa miaka 5 ni fedha kiasi gani?

Kwa hiyo mwisho wa siku sababu hata raisi amepitia kwa walimu wa shule ya msingi unataka wamzidi rais mshahara
Nimekuonesha ulipotoa coment yako kumdharau mwalimu wa shule ya msingi huyo ndo aliekutoa tongotongo rais sijawah kumsikia akidharau walimu wa shule ya msingi ww ndo unadharau unaona mbunge ndo kila kitu
 
Hili la posho ya makalio ndo la muhimu sana kuliko kuuza sura luningani wanakokazania eti bunge liwe live
 
Mnyukano Mkubwa majimboni wa kuwania Ubunge,ni harakati ya kufukuzia ULAJI.Bunge letu limejaa wabunge maslahi,rejea kashfa za rushwa juzi juzi tu hapa.Sasa kwa wabunge ambao uadilifu wao unatia shaka,lugha ya kuondoa sitting allowance wataielewa?
 
Lakini mbunge hawez kuishi kimasikini pia.haiwezekani unalipua dili za watu bungeni alafu ukalale guest ya 20,000.kumbuka mbunge hana ulinzi kama wa raisi.Bado bunge ameshikilia dhamana kubwa sana kwa nchi
 
Kumbuka bado wanalipwa perdiem ambayo ni shilingi 120,000 kwa siku mbali na hiyo sitting allowance.Perdiem ni haki yao lakini hiyo sitting allowance kwakweli haingii akilini hata kidogo.
Ila sitting allowance kama sikosei ni laki 3 na sio 2
 
Wapinzani wangeuza sana kwa hoja hii, lakini wapo kimaslahi zaidi ya ccm,bahati yao mbaya hawajapata fursa.
Hii ndio hoja kubwa ambayo wapingani wangeisimamia kipekee na kuonyesha uzalendo,
Kimsingi JPM hawezi kufanya kila kitu, yao mambo ambayo ilikuyafanya anahitaji uungwaji mkono. Hatutaraji ccm kuunga mkono hoja hii, ndio maana jicho linatupwa upinzani ili kumpa nguvu Raisi.
Jambo la pili linaloweza kufanyika ni kwa Raia kupaza sauti, maandamano, mabango, nk.

Bado naona nafasi ya media na wanaharakati ambao kama hataingiza mikono yao itakuwa ni msaada mkubwa.
Tukumbuke nguvu na mamlaka waliyonayo wabunge ni makubwa sana na bila shaka Raisi hawezi kufanya jambo ambalo litamtumbukiza kwenye mtafaruku au mvutano na waheshimiwa hawa.
Lakini wananchi ndio wenye power kuliko hata hilo binge, yeyote atakayekuwa upande wetu wananchi si bunge wala chama kinachoweza kumwangusha
 
Zitto Zubery Kabwe...ndiye pekee aliyeweza kukataa posho ya masaburi..ohh sorry..makalio.katika hili pamoja na mapungufu yake yote,yeye ni MWAMBA..
 
Hapo kwenye posho ndo utawajua wabunge walioenda bungeni kimaslahi yao binafsi na wale wenye moyo wa dhati wa kuwatumikia wananchi.
 
Hi nchi Tajiri sana aise, kwa Siku 1 sitting allowance za wabunge tu Tsh 79.4M? Hiyo ni nje ya wale maafisa wa binge nk. Aise.

Binafsi sipingi hiyo posho unless utafutwe utaratibu mwingine wa wao kuishi Dodoma, Mimi napendekeza idadi ya wabunge ipunguzwe, napendekeza tuondokane na mfumo wa kimajimbo badala yake kila wilaya iwe na mbunge 1 tu, kwa mfano Dar iwe na wabunge 3 tu, Kinondoni, Temeke na Ilala kwasababu siioni impact ya wabunge kwenye uchumi na maendeleo ya nchi.
Kweli kabsa wanakua wabunge wengi na impact yao kwny maendeleo ni ndogo sana inabd wakae waangalie umuhimu wa wabunge kwny baadhi ya maeneo co lazma kote kugawanywe kimajimbo
 
Lakini mbunge hawez kuishi kimasikini pia.haiwezekani unalipua dili za watu bungeni alafu ukalale guest ya 20,000.kumbuka mbunge hana ulinzi kama wa raisi.Bado bunge ameshikilia dhamana kubwa sana kwa nchi
Tambua kwa siku pia wanalipwa perdiem ya sh 120,00 mbali na hiyo 200,000 ambayo hulipwa kama sitting allowance.
 
Lakini mbunge hawez kuishi kimasikini pia.haiwezekani unalipua dili za watu bungeni alafu ukalale guest ya 20,000.kumbuka mbunge hana ulinzi kama wa raisi.Bado bunge ameshikilia dhamana kubwa sana kwa nchi
Sijawahi kuona na sitawahi kuona faida ya mbunge afadhali m/kiti wa serikali za mitaa kuliko mbunge
 
Hivi wakiondoa mishahara na kama kuna allowance nyingine, wakabakiza hiyo sitting allowance ambayo ikatwe kodi itakuwaje? Mimi karibu siku zote naliona bunge li wazi. Kama kuna anayefahamu pesa wanazopata wabunge alete info ili tupige hesabu vizuri.
 
Sababu wapinzani wanapita humu.. TU mwambie kiongoz wa upinzani alichukue apeleke kama Hoja binafsi, ili tuone uzalendo wao
Ukitaka kuona umoja wao basi ni sehemu moja tu penye hili 95%huwa pamoja na kama hayo yakipita usishangae mwaka 2020 mkawa mnabembeleza watu kwa kuwapigia magoti wawe wabunge wenu na si huu unafiki wa wengi wao kusema nipeni ubunge bwana mkubwa anataka kufanya kazi nami.
Pangepigwa hosteli nzuri tu hapo idodomya tungepunguza hizi figisufigisu ila ndo hivyo utasikia tumekuwa wanafunzi sie.
 
halafu tunaongeza mzigo tena wabunge wa viti maalumu na wakuteuliwa,angalau wabunge wa kuteuliwa kuliko viti maalumu hawa kazi yao ni nini hasa?mimi naona kazi kubwa ya mbunge ni kutunga sheria lakini kuna wabunge wengi wala hawatusaidii kwa hilo,ndio sababu wanapitisha sheria ambazo saa nyingine hazina maana eti kila mwananchi alipie laini yake ya simu kila mwezi halafu wakasema ni hela ndogo tu wakijifananisha wao ambao wanapata allowance kibao kwa siku ambazo kwa wengine ni mishahara ya mwezi mzima.Halafu matatizo ya jimbo lolote nchi hii ni sawa au yanakaribiana na matatizo ya nchi yoyote ya afrika kwamba matatizo ni yaleyale yanajulikana hakuna haja ya kuwa na watu wengi wanapigia kelele matatizo hayohayo bila tija nakubaliana na alieshauri kwamba jiji kama DAR liwe na wabunge watatu tu kwa maana ya wilaya ili kupunguza gharama.
 
Back
Top Bottom