Tuwe wakweli! Mchina alishawahi kutoa msaada gani kwa nchi za kiafrica zaidi ya kutuuzia vitu vyenye ubora feki!

Baada ya Trump kusitisha misaada Afrika, kumetokea sintofahamu nyingi zikisema, "Haya sasa, huyo Mchina ajitokeze!"

Ukweli ni kwamba Mchina ni mlaghai na mpigaji kuliko hao mabeberu. Angalau, pamoja na kutupiga, wametuwezesha na sisi mdogomdogo kusogea! Nchi zote zilizokopa kwa Mchina na kushindwa kurejesha zimejikuta zikinyang’anywa mali zao, kama ilivyotokea Zambia na Kenya, ambapo viwanja vyao vya ndege vimechukuliwa na kumilikiwa na Mchina mpaka watakaporudisha senti yao ya mwisho.

Tanzania, kipindi cha Kikwete, tulikopa na kuweka rehani gesi yetu yooote ya Mtwara, na sasa inaenda China bure, huku sisi tukiendelea kupikia kuni na mkaa maana gesi haikamatiki kwa Watanzania wengi, hasa vijijini. Mchina aliuziwa Bandari ya Bagamoyo chini ya Kikwete na kupewa mkataba wa miaka 99 bila kulipa kodi kwa masharti dharimu kabisa—masharti ambayo Magufuli aliyakataa na kuupiga chini huo mradi.

Kwa ufupi, hakuna mashetani kwenye vita vya uchumi vya unyonyaji kama China. Bora mzungu, ana utu—siyo Mchina! Kwa hiyo, kama Mmarekani katuachia Mchina, basi tupambane naye! Twaafwaa!

Mii nilifikiri unasema, baada ya Trump kuachana na WHO pia kupunguza kwa kiwango kikubwa misaada kwa masikini. Waafrika wayanyeje? Sasa wewe unataka mChina afanye nini kwetu. Hilo halitatusaidia. Huyu naye anajitufuta kwa ajili ya watu wake.
 
Haya unanunua plasma tv ya mchina laki ndani ya miezi 3 imekufa beyond repair. Unanunua nyingine ndani ya miaka 2 umetumia million 10. Sasa Mzungu unanunua moja million 2 yenye guarantee ya miaka 2 hadi 5 unatumia. Nani bora kati Mchina au Mzungu! Mchina muuaji!
Nina Star X tangu 2018
 
Back
Top Bottom