Tuwe wakweli! Mchina alishawahi kutoa msaada gani kwa nchi za kiafrica zaidi ya kutuuzia vitu vyenye ubora feki!

Morning_star

JF-Expert Member
Apr 21, 2018
6,042
17,298
Baada ya Trump kusitisha misaada Afrika, kumetokea sintofahamu nyingi zikisema, "Haya sasa, huyo Mchina ajitokeze!"

Ukweli ni kwamba Mchina ni mlaghai na mpigaji kuliko hao mabeberu. Angalau, pamoja na kutupiga, wametuwezesha na sisi mdogomdogo kusogea! Nchi zote zilizokopa kwa Mchina na kushindwa kurejesha zimejikuta zikinyang’anywa mali zao, kama ilivyotokea Zambia na Kenya, ambapo viwanja vyao vya ndege vimechukuliwa na kumilikiwa na Mchina mpaka watakaporudisha senti yao ya mwisho.

Tanzania, kipindi cha Kikwete, tulikopa na kuweka rehani gesi yetu yooote ya Mtwara, na sasa inaenda China bure, huku sisi tukiendelea kupikia kuni na mkaa maana gesi haikamatiki kwa Watanzania wengi, hasa vijijini. Mchina aliuziwa Bandari ya Bagamoyo chini ya Kikwete na kupewa mkataba wa miaka 99 bila kulipa kodi kwa masharti dharimu kabisa—masharti ambayo Magufuli aliyakataa na kuupiga chini huo mradi.

Kwa ufupi, hakuna mashetani kwenye vita vya uchumi vya unyonyaji kama China. Bora mzungu, ana utu—siyo Mchina! Kwa hiyo, kama Mmarekani katuachia Mchina, basi tupambane naye! Twaafwaa!
 
Mi naona wote ni wale wale
Endapo wangechukua 60%na kuipa afrika 40 kwenye biashara basi afrika ingekuwa maili nyingi sana kuliko hapa tulipo
 
Baada ya Trump kusitisha misaada Africa, kumetokea sintofahamu nyingi zikisema haya sasa huyo Mchina ajitokeze! Ukweli ni kwamba mchina ni mlaghai na mpigaji kuliko hao mabeberu angalau pamoja na kutupiga lakini wametuwezesha nasisi mdogomdogo kusogea! Mchi zote zilizokopa kwa mchina zikashindwa kurejesha zimepelekea kunyanganywa mali zao kama Zambia na Kenya kunyanganywa umiliki wa viwanja vyao vya ndege na kumilikiwa na mchini mpaka watakaporudisha senti yao ya mwisho. Tanzania kipindi cha Kikwete tulikopa na kuweka rehani gesi yetu yooote ya mtwara na inaenda China bure na sisi kuendelea kupikia kuni na mkaa maana gesi haikamatiki kwa watanzania wengi hasahasa vijijini. Mchina aliuziwa bandari ya Bagamoyo na Kikwete kuiendesha miaka 99 bila kulipa kodi kwa masharti dharimu kabisa ambapo Magufuri aliyakataa na kuupiga chini huo mradi. Kwa ufupi hakuna mashetani kwenye vita vya uchumi ya unyonyaji kama China. Bora mzungu ana utu sio mchina! Kwahiyo kama mmarekani katuachia mchina tupambane naye! Twaafwaa!
Mchina hauzi hata 7% Afrika kwa bidhaa zake anazouza duniani. % kubwa ya bidhaa zake zinanunuliwa marekani na ulaya. Nyie hiyo 7% ni ya bidhaa ambazo mnaweza kuafford.
Wewe leo unaenda kariakoo unapata Smart TV inche 50+ kwa milioni labda 2. Hivi unadhani ingekuwa bidhaa ya mmarekani ungeipata kwa pesa hiyo.
Mchina kwa kutengeneza bidhaa zake kwa grades, kumewafanya hata nyie afrika mpate kuwa na vitu ambavyo huenda kwenu vingekuwa ndoto au vya watu wachache.
Kitu cha mchina ambacho unakinunua laki, kikitoka kwa mmarekani au mgermany utakinunua laki 4.
 
"Hakuna pombe za bure kipo wanachotaka,

We kunywa tu, watakubaka."

Nay Wa Mitego - Sijalewa.
 
Mchina hauzi hata 7% Afrika kwa bidhaa zake anazouza duniani. % kubwa ya bidhaa zake zinanunuliwa marekani na ulaya. Nyie hiyo 7% ni ya bidhaa ambazo mnaweza kuafford.
Wewe leo unaenda kariakoo unapata Smart TV inche 50+ kwa milioni labda 2. Hivi unadhani ingekuwa bidhaa ya mmarekani ungeipata kwa pesa hiyo.
Mchina kwa kutengeneza bidhaa zake kwa grades, kumewafanya hata nyie afrika mpate kuwa na vitu ambavyo huenda kwenu vingekuwa ndoto au vya watu wachache.
Kitu cha mchina ambacho unakinunua laki, kikitoka kwa mmarekani au mgermany utakinunua laki 4.
Haya unanunua plasma tv ya mchina laki ndani ya miezi 3 imekufa beyond repair. Unanunua nyingine ndani ya miaka 2 umetumia million 10. Sasa Mzungu unanunua moja million 2 yenye guarantee ya miaka 2 hadi 5 unatumia. Nani bora kati Mchina au Mzungu! Mchina muuaji!
 
Huo ni mtazamo wako.
Kama unataka msaada kwa China utasubiri sana.
China ni partners,bila China hao matajiri wote wa kariakoo wasingekuwepo,Biashara nyingi zilizowatajirisha watu zisingekuwepo,watu walioajiriwa kwenye biashara hizo wasingekuwa na Kazi.
Bidhaa nyingi tunazozitumia zingekuwa zinazalishwa Marekani ni Wazi tusingeweza kumudu kuzimiliki!
Madaraja,Majengo,Bandari,Barabara,nk..Vingekuwa vinajengwa na wazungu basi Africa ingekuwa bado ipo nyuma sana kimaendeleo.
Kwa kweli Idumu China Ili tuendelee kuheshimiana hapa mjini.
 
Haya unanunua plasma tv ya mchina laki ndani ya miezi 3 imekufa beyond repair. Unanunua nyingine ndani ya miaka 2 umetumia million 10. Sasa Mzungu unanunua moja million 2 yenye guarantee ya miaka 2 hadi 5 unatumia. Nani bora kati Mchina au Mzungu! Mchina muuaji!
Mbona watu tuna tv za mchina zaidi ya miaka 10? Hao akina litop sijui takataka gani si product za mchina. And by the way nimekwambia mchina bidhaa anazouza Afrika hazifiki hata 7% ya bidhaa anazouza duniani. Hivyo usimlaumu mchina, laumu wafanyabiashara wenu wakienda china wanachukua low quality products kwa sababu wanajua ndizo mnazoweza kuziafford. Huko Marekani unadhani bidhaa za china zinazouzwa huko ni sawa na hizi za kwenu?
 
kwani tanzagiza na afrika zimeshawahi kutoa msaada gani kwa nchi yoyote ile dunia hii?
 
Haya unanunua plasma tv ya mchina laki ndani ya miezi 3 imekufa beyond repair. Unanunua nyingine ndani ya miaka 2 umetumia million 10. Sasa Mzungu unanunua moja million 2 yenye guarantee ya miaka 2 hadi 5 unatumia. Nani bora kati Mchina au Mzungu! Mchina muuaji!
TV gani hiyo ya wazungu? Hebu tuelimishe
 
Huo ni mtazamo wako.
Kama unataka msaada kwa China utasubiri sana.
China ni partners,bila China hao matajiri wote wa kariakoo wasingekuwepo,Biashara nyingi zilizowatajirisha watu zisingekuwepo,watu waliojariwa kwenye biashara hizo wasingekuwa na Kazi.
Bidhaa nyingi tunazozitumia zingekuwa zinazalishwa Marekani ni Wazi tusingeweza kumudu kuzimiliki!
Madaraja,Majengo,Bandari,Barabara,nk..Vingekuwa vinajengwa na wazungu basi Africa ingekuwa bado ipo nyuma sana kimaendeleo.
Kwa kweli Idumu China Ili tuendelee kuheshimiana hapa mjini.
Kila kitu kina faida na hasara! Nchi yenye nguvukazi kwa bei rahisi ni china ndo maana baadhi makampuni ya wazungu yalihamisha viwanda vyao na kwenda kuvijenga china. Sumsang mobile phone iliyotengenezwa china bei yake ni nusu ya iliyotengenezwa nchi za magharibi. Kwa hilo nawasifu maana wengi tusingeweza kumiliki samsung s6 ☹😍😍😍
 
China anafanya projects za ujenzi wa barabara,reli,viwanda, hospital kwa mikopo ambayo nchi za Africa haziwezi kulipa. Mchina ana project yake ya China Road and Belt Initiative ambayo ataunganisha Africa,Asia na America ili afanye biashara na project zake kirahisi, mpaka wazungu wanaona mchina baadae hatakuwa hatari
 
Back
Top Bottom