Powder
JF-Expert Member
- Jan 6, 2016
- 4,805
- 6,301
Dah! Niliumia Sana! Na bila Mama kumfuma angeua wote.Imerushwa hiyo kwenye WhatsApp nahisi ninayo sijaifuta
Dah! Niliumia Sana! Na bila Mama kumfuma angeua wote.Imerushwa hiyo kwenye WhatsApp nahisi ninayo sijaifuta
HaaaaahaaaaNlimchana live. Akaaga mwenyewe. Nna mambo ya msingi ya kumuomba Mungu na sio kupambana na viuchawi vya kijinga
Hadi utumie macho ya rohoni.Hivi uchawi hauonekani kwenye cctv?!
Pole mama.Mimi nilishapata house girl mshirikina yeye alikuja na furushi la dawa za kutumia ili kufanikisha mipango yake.cha kwanza kabisa alichofanya alichukua boxer ya mume wangu akavaa kwa bahati nikamuona nilipomuuliza akasema yake amenunua sikuamuni nikamvua nikahisi ni mwezi nikamua kupiga sachi begi lake ndio hapo nilipokuta na dawa za kuoga,za chakula,za kuchoma,za unyayo.za kutafuna.nilichoka niliona kama naota vile.nikamtisha nampeleka polisi binti akafunguka kuwa ni maagizo alipewa na shangazi yake kuwa asifanye kazi ya kulea watoto wa mwanamke mwenzio lazima nae aolewe na baba mwenye nyumba.nilimsafirisha siku ya pili.haya mambo yapo lazima nyumba zetu tuzilinde kwa sala na maombi mungu atusaidie.
Hata EFM Radio walirusha mkasa wa namna hii. Yule binti baada ya kuombewa akaokoka.Achaneni na hizi fikira. hizi ndio adui wa maendeleo na kubomoa Imani kwenye dini zenu
Too late nishaanza kumhisi! Huwezi kunitusha hivi halafu utegemee nichukulie poa tu!Habari za Weekend, Wadau!
Kuna baadhi ya wasichana wa kazi huonekana wapole, watiifu, wachapa kazi, n.k kiasi ambacho mabosi wao huamua kuwaongezea mishahara au kuwapa zawadi yoyote ile to show their appreciation kwa hao wadada.
Kwa bahati mbaya sana baadhi ya wafanyakazi hao ni wachawi na mabosi huwa hawajui hadi pale jambo baya linapokuja tokea kwenye familia zao kutokana na uchawi wa wafanyakazi hao.
Najua wengine humu walishawahi kuishi na wadada wa namna hiyo na zahma zikawakumba.
Nilisimuliwa mkasa mmoja na jamaa yangu kuhusiana na wadada hawa:
Familia moja ilikuwa na msichana wa kazi aliyependwa na kuaminiwa sana na kila mwanafamilia kwa sababu Kila kitu kilifanywa kwa usahihi na kwa wakati.
Kutokana na hali hiyo, yule binti alikuwa ana uwezo wa kupendekeza kitu kwa bosi wake na akasikilizwa. Hivyo, kila mama mwenye nyumba alipotaka kuwanunulia nguo watoto wake (wadogo wawili ke na me) HG alipendekeza wanunuliwe nguo nyekundu. Alikubaliwa.
Hata usiku alikuwa akilala nao na walikuwa wakimpenda sana.
Baadaye familia ikawa inaandamwa na mikosi na maradhi mfululizo kiasi cha kuitia familia umaskini.
Wale watu wakamwita mtumishi wa Mungu, akawaombea wanafamilia wote na ndipo walipogundua kuwa yule HG ni mchawi na ndo chanzo kikubwa cha matatizo hayo (maana alikiri mwenyew baada ya kuungua na moto wa Roho Mtakatifu.)
Akasema na mengine mengi tu.
1. Kazi zote mle ndani huwa hafanyi. Huwafanyisha mabosi wake.
2.Watoto alishaanza kuwafundisha uchawi na ndo kisa cha kuwachagulia nguo nyekundu.
3. Ameshawahi kuwalisha nyama za binadamu wao wakijua wanakula nyama ya ngómbe au noah.
4. Uchawi huo alijifunza kwa bibi yake (mzaa mama)
Hivyo, ili tuwe salama ni muhimu kufanya yafuatayo:
1. Tujaribu kujua familia zilizowalea na kuwakuza kabla ya kuwaajiri.
2. Tuwachunguze kwa makini tunapokuwa nao.
3. Kubwa zaidi tumwombe Mungu kabla ya kuwaajiri na hata tunapoishi nao ili tuyaone matendo yao ya giza kwa jicho la rohoni.
Angalizo: Usianze kumhisi vibaya msichana wako wa kazi
"Hayajakukuta"Hizi imani zenu za kushirikina...
Kuna moja inasambaa sana mitandaon huyo binti akiwa anahojiwaPole mkuu.
Kuna mmoja aliuliwa mwanae, kimazingara. Baada ya wk moja yule mama alichokikuta home nusura azimie. Alikwenda kazini asbh halafu akarudu ghafla home kuchukua kitu fulani alichokisahau. Akamkuta mdada uwanjani anafagia.
Akamsalimia na kuingia ndani. Nako akamkuta mdada akifanya usafi. Kwa mshangao akaingia jikoni, nako akamkuta mdada huyo huyo akiosha vyombo.
Kumbe yule dada alijiweka ktk nafsi 3 kichawi.
Mm kwangu marufuku hgeliDuh, familia nyingi zinaangamizwa na hawa mabinti lkn tunajifanya wasomi hatuamini kuwa ushirikina upo.
Mkuu hyo avatar huo mdomo ni wako? Utakuwa mkalee kwenye mambo Ya mistarMimi nilishapata house girl mshirikina yeye alikuja na furushi la dawa za kutumia ili kufanikisha mipango yake.cha kwanza kabisa alichofanya alichukua boxer ya mume wangu akavaa kwa bahati nikamuona nilipomuuliza akasema yake amenunua sikuamuni nikamvua nikahisi ni mwezi nikamua kupiga sachi begi lake ndio hapo nilipokuta na dawa za kuoga,za chakula,za kuchoma,za unyayo.za kutafuna.nilichoka niliona kama naota vile.nikamtisha nampeleka polisi binti akafunguka kuwa ni maagizo alipewa na shangazi yake kuwa asifanye kazi ya kulea watoto wa mwanamke mwenzio lazima nae aolewe na baba mwenye nyumba.nilimsafirisha siku ya pili.haya mambo yapo lazima nyumba zetu tuzilinde kwa sala na maombi mungu atusaidie.