Tusipokemea, Redio Imaan itatuvuruga

Status
Not open for further replies.
Nani wa kuwagusa na raisi ni muislamu mwenzao,wanafanya kila wanachotaka maana wanaelekezwa namna hiyo na raisi,"shehe" wao!
Unadhani polisi hawapo morogoro wafanye intelijensia zao hizo?
 
Sijui unakataa nini unakubali nini! unasema alibadili jina ndo akasoma halafu unasema la kufelishwa unalikataa.sasa angefelishwa vipi wakati ana jina la kikristu? Kwa taarifa yako baadhi ya waislamu waliopenya ktk elimu walitumia ama majina ya kikristu au ya kimila.mfano Jakya Mrisho Kikwete,Ukiwaona Ditopile Mzuzuri,Makwaiya Wakuhenga,Kigoma Malima nk.Hata hivyo tatizo lilikuwa sana kutoka primari kwenda sekondari,mtu aliyekuwa anafanikiwa kuvuWlika hapo alikuwa anaendelea bila ubaguzi.Wabaguzi hata hivyo walikuwa wanauma na kupuliza walikuwa wanaachia namba ndogo sana ya Waislam ili wasije wakashtuka mapema


Kalamazoo: nimfuatlia mabandiko yako, napenda kuuliza.

Kama walifelishwa, unafikiri ni kwa sababu gani?
Walikuwa na potentials zipi ambazo zingekuwa detrimental kwa jamii kama wangeendelea kusoma?
 
Maggid,....
wewe si ni muandishi wa habari lakini?

Nisamehe nikikujumuisha kwenye waandishi wa habari "wanafiki" maana wengi wamesikia yanayo endelea katika redio hiyo lakini wanaishia kuongea chini chini tu kama hivi,kwani ni laana kwa waandishi wa habari kusema "kituo hiki cha redio kinachochea udini tanzania" katika magazeti yenu?

Sawa,umewasikia pia!
Umestuka sana,...then what?
Au kulileta hilo jf ndo mwisho na litapata ufumbuzi?
 
hicho kituo cha redio ni cha kufunga-nashangaa serikali imekaa kimya

Kufunga kituo hicho si suluhisho,
Tamko la waislamu limebandikwa hata humu jamvini kama jinsi lilivyo,
Kituo cha radio kilitumika tu ktk kuweka wazi zaidi kwa kilichosemwa,
Concept hapa ni KITUO KUTUMIKA KUREJEA TAMKO LA MASHEIKH NA KULIJADILI, hivyo kuwafungia ni kuwasha moto mkali.
Kituo jamani hawana kosa, kosa lao ni KUJADILI TAMKO TU.
 
Ndugu Zangu,
JANA usiku katika pekuapekua zangu za idhaa za redioni, nikakutana, kwa mara ya kwanza, na Redio Imaan FM. Inatangaza kutoka Morogoro. Nilichosikiliza kilikuwa kipindi maalum cha marudio kutoka Jumapili iliyopita. Niseme neon moja tu na kwa msisitizo: NILISHTUKA.

Hakika, kilichokuwa kikirushwa hewani ni matangazo ya uchochezi. Kuchochea uhasama baina ya Watanzania Waislam na Watanzania wenzao Wakristo. Nilijiuliza, kama taifa tunakwenda wapi? Na maswali yakawa mengi. Je, Tume ya Utangazaji inafahamu kinachoendelea au imelala usingizi? Je, watu wetu wa Intelijensia hawana taarifa za Kiintelijensia juu ya kinachooendelea?

Naam. uzoefu unatufundisha, kuwa kuwasha moto ni jambo jepesi sana, lakini, kuuzima moto, yaweza kuwa ni kazi ngumu sana.

Moto ulioanza kwenye nyumba moja ya nyasi kijijini, waweza kusambaa haraka na hata kuteketeza nyumba nyingine, mali na kuhatarisha maisha.

Nimekumbushia mara kadhaa, kuwa historia ni mwalimu mzuri. Mwezi Aprili 6, mwaka 1999 katika iliyokuwa Hoteli ya Kilimanjaro, Bi Joy Mukanyange , aliyekuwa Balozi wa Rwanda hapa Tanzania, alituambia Watanzania juu ya kile alichokiona lakini sisi Watanzania hatukukiona. Ilikuwa ni katika mjadala rasmi wa kumbukumbu ya mauji ya kimbari ya watu wa Rwanda ya mwaka 1994.

Bi Mukanyange alisema: " Naogopa., kwani nimeanza kuona dalili zinazojengeka za mgawanyiko wa kidini nchini Tanzania na eneo lote la Maziwa Makuu, hali ambayo inaweza kusababisha mauaji ya halaiki kama yale yaliyotokea nchini mwetu mwaka 1994," alisema Balozi huyo wa Rwanda kabla ya kuendelea kutoa ufafanuzi wa historia ya Rwanda na matukio yaliyosababisha maujai yale ya Wanyarwanda ya wao kwa wao. Ni kauli ya kuitafakari kwa makini.

Mimi sasa naamini, kuwa Afrika mvunja nchi si mwananchi, bali ni mwanasiasa. Ni kwa kutanguliza mbele maslahi ya kisiasa badala ya kitaifa. Masikini nchi yetu, Watanzania hawana udini ila kuna wachache, na hasa wanasiasa, walio tayari kutumia mtaji wa udini kutimiza malengo yao. Inasikitisha sana, kuwa baadhi ya wanasiasa, hata kwa kutumia udini, wameamua kutupitisha Watanzania katika njia isiyo salama. Ili mradi, malengo yao yatimie.

Watanzania tukubali sasa, kuwa nchi yetu imepatwa na bahati mbaya ya baadhi ya Watanzania wenzetu kuanza kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwetu. Kuna wanaotaka tuanze kubaguana kwa misingi ya kidini. Hili ni jambo la hatari sana.

Taratibu tumeanza kuizoea misamiati ya sisi na wao. Mathalan, sisi Wakristo na wao Waislamu. Sisi Wachagga na wao Wazaramo. Tunasahau, kuwa katika nchi yetu hii hakuna Sisi na Wao, kuna SISI tu.Tutakapokumbwa na maafa ya kitaifa watakaoathirika ni SISI, hakutakuwa na WAO.

Hatari kubwa ninayoiona ni tatizo la baadhi ya Watanzania kuwa na ufahamu mdogo juu ya dunia tunayoishi sasa, kibaya zaidi,ufahamu mdogo wa historia yetu. Uelewa wa historia ya jamii husika ni jambo muhimu sana.
Kiumbe huwezi kuelewa ya leo, kesho na kesho kutwa kama huelewi ya jana. Kuielewa historia yako ni kuelewa ulipo na unakokwenda.

Dalili tunazoziona sasa za kupandikiza mbegu za chuki kwa misingi ya udini si dalili njema. Haya yatatupelekea kwenye maafa.

Hii ni nchi yetu. Katika ulimwengu tunamoishi kuna mamilioni ya watu wasio na nchi. Wahenga wetu walishiriki katika kuijenga nchi hii, wametutarajia sisi tuendelee kuijenga na kuilinda hadhi ya nchi hii.

Muda wetu wa kuishi humu duniani ni mfupi sana. Tuyachambue matatizo halisi ya jamii yetu. Kisha tusiishie kwenye kuyaorodhesha, hiyo ni kazi rahisi sana. Tutafute njia ya kuyatatua matatizo hayo.

Hatuna haja ya kubaguana kwa misingi ya ukabila, dini na rangi. Sisi wote ni Watanzania. Tuna historia ya kujivunia. Ni historia yetu wenyewe.

Mtanzania halisi na mkweli kwa nchi yake atazungumzia matatizo ya Tanzania kwa ujumla wake. Hatakuwa na sababu ya kunyoosha kidole kwa Wahindi, Walutheli, Waprotestanti, Wasabato, Wakatoliki, Washia, Wasunni, Waismailia, wenye kuamini jadi, Wazaramo, Wagogo au Wachagga, kwamba ndio wa kulaumiwa.

Wenye kuathirika na umasikini wa nchi hii ni wengi mno. Si Wakristo peke yao, si Waislamu peke yao, si Wapagani peke yao, si Wamachinga peke yao na si Wazaramo peke yao.

Wahenga walisema "kamba hukatikia pabovu". Kamwe huwezi kuwavuruga Watanzania na kuwafanya wachinjane kwa sababu za kudai kuna upendeleo wa ukabila au wa kisiasa. Nchi hii ina makabila zaidi ya 125 na utitiri wa vyama vya siasa.

Mahala ambapo unaweza kuwagawa Watanzania na hata kufanikiwa wachinjane ni kwenye masuala ya imani. Tusikubali dini iwe ndiyo penye ubovu kwenye kamba inayotuunganisha Watanzania. Mungu Ibariki Tanzania.

Maggid

..... na we Mjengwa umejaa malalamishi mpaka hueleweki ! ungeweka wazi kilicho kukera na chanzo chake nini na suluhisho ni nini!
 
Waafrika mnashangaza sana. Hizo dini zenyewe mnazo gombania mmeletewa na wageni. Leo hii ndo mnataka zitutenganishe.
Huku tunakoenda siko. Kuna watu wanatoa maneno yanasikitisha sana.
Tumieni busara!
 
Kalamazoo: nimfuatlia mabandiko yako, napenda kuuliza.

Kama walifelishwa, unafikiri ni kwa sababu gani?
Walikuwa na potentials zipi ambazo zingekuwa detrimental kwa jamii kama wangeendelea kusoma?
sababu ili kuwapendelea wakristo period

detrimental..yes (as per thier belief) waislamu wakisoma watawa over power
 
Truly,
Lakini cha msing ni HEKIMA & BUSARA zitawale, nchi yetu hii kila sekta lazima kuna watendaji wakuu wa dini hizi mbili wapo. Hivyo wenye kutoa matamko makali kiasi hiki cha MAASKOFU NA TAMKO vs WAISLAMU NA TAMKO si muendelezo mwema wa jamii yetu tulivu, ni pande zote hizo mbili zapaswa kulaaniwa kwa matamko yao ambayo tayari yameshapenyeza mpk huko kwenye minority uswahilini. Muingiliano wa jamii yetu utaangamia tena kuliko kimbari ya Rwanda ilivyokuwa...NAFSI YANGU IPO KTK MASHAKA MAKUU KWA YATAKAYOJIRI KWA UDINI NCHINI NA HATMA YA TANGANYIKA NA VIZAZI VYETU VIJAVYO.

NAYAPINGA MATAMKO YOTE YA WAKRISTO NA WAISLAMU KWA 'KUAMSHA ARI & HISIA ZA UDINI' KWA WATANZANIA.

JK NDO anapalilia haya....believe me, he is desparate kuwanyamazisha Maaskofu wasiongelee elimu ya uraia. Na njia pekee ni kuwanunua baadhi ya Mashehe uchwara ili wapinge kila kitu cha maaskofu ili serikali isikosolewe ki hivyo. Bahati mbaya sana hajui kwamba hata yeye anajiingiza kwenye mkenge mbaya sana!
Nampa pole
 
Naona JK aliyeanzisha hoja hii ya udini ndiye anayepaswa kutoa tamko kwa hao watu wake. Tangu siku ya kwanza alipoanzisha porojo hizi za udini nilijiuliza "hivi huyu mtu hajui kwamba sasa ndio anawasha moto wa udini?" Huyu anapaswa kukaa pembeni haraka iwezekanavyo kabla hajaiingiza nchi matatani.
 
Kwa kweli uchochezi wa kidini kupitia miredioni na kwa kuwatumia viongozi wa kidini ni kwa ajili ya maslahi ya baadhi tu ya wanasiasa. Binafsi siwaungi hawa mkono kwa hila hizo.

Wananchi sisi tuwapuuze tu na kuendelea na umoja wetu wa kitaifa.
 
By taking sides we end up missing the real target and the solution is hardly and sometimes painfully realized.Tujenge utamaduni wa hoja zinazoenzi umoja na si ubaguzi. Tusikumbatie wote tunaoshabihiana dini wala tusibague wote tusioshabihiana dini kwa sababu rafiki au adui yako anaweza kuwa yule mnayeshabihiana au msiyeshabihiana dini. Hakuna sababu timamu ya kututumbukiza kwenye chokochoko za kidini kwa maneno au vitendo ndipo tutambue kuwa sote tunatafunwa na umaskini, wala hakuna sababu ya kupiga hatua kuingia 2015 kwa zaidi ya muongo. Hatuwezi tukafika salama kwenye neema kama tutaanza kushikiana bango wenyewe kwa wenyewe badala ya kuungana kushikia bango ombwe la uongozi.
 
radio imaan wamesema walichosema,katka yote cwaung mkono kwenye kuigawa nch,lakin kuna madai ambayo yapo kwenye tamko,naweza sema ni sensitive sana,MAZNGRA 2NAYOISH WANANCH HAKUNA UDINI,lakini kwenye taasi mbalimbli kuna udini+ukabila,nina mfano hai,pale udsm kuna mhadhir aliwapa wakristo majib ya ue kanisani,kwa bahat ukaribu na yule mkristo ulisaidia kuipata nyanga,jaman haya masuala had leo wadau wanayazungumza ujue kuna jambo,MJENGWA UMENIPATA
Utumbo mtupu. Waislam wajenge ufahamu. Msikiti wa mwenge ni balaa siku walipokorofishana wao kwa wao kupitia kipaza sauti wakadai wameingiliwa na wakristo just imagine wanatamka takbir kuwa waislam wachukue slaa walizo nazo wapambane na watu ambao wao wanadai ni wakristo, wakatoriki na CHADEMA na kuwa hiyo ndiyo Jihad. Nilitamani nikimbilie polisi kuuliza kama walikuwa wakisikiliza wito huo. Hapo hapo mwenge siku ya ibada ya Idd kubwa sikusikia mawaidha juu ya dini baada ya mwanamama kumaliza. Jamaa alikua anafurahia ushindi wa ccm kuwa ni ushindi wa uislam dhidi ya ukristo. Alidai kuwa ukristo unamiaka mia tangu kuingia nchini na uliukuta uislam hivyo hawapaswi kuongozwa na wakristo. Wanasema waislam ni wachache sana chadema hivyo hakipaswi kuungwa mkono. Hoja iliitimishwa na usemi UISLAM KWANZA. Yaani kama wewe ni kiongozi unanafasi za kazi ajiri waislam kwanza. Watu hawa shule zao ndogo na upeo mdogo wanashinda na kuongoza maisha yao msikitini lakini wanaachiwa vipaza sauti na hajabu hata baadhi ya wasomi usadiki na kujenga chuki kana kwamba wakristo ni jeshi moja. Tazama elimu ya mapadri, maaskofu, wachungaji na wazee wa makanisa ni wasomi. Kupitia kwao watu wanatambua haki zao na fulsa zilizopo. Wakati wale wenye dhamana ya dini ya kiislam ujaza watu ujinga na kuishia kulalamika. Zanzibar ni sehemu ya TZ wanaotaka uislam waende huko. Huko Rais anaandaliwa gwaride kabla ya kuutubia baraza la Idd kuliko kusubiri viongozi wasomi wa kikristo wakitoa tamko nao wanatoa tamko kinzani ni ujuha tu. CCM si Uislam na JK, serikali na Dowans si Uislam. Mtupe haki yetu kupigania maslai ya Taifa letu ili Taifa lishamiri badala ya kubaki na idadi ya viongozi wa nchi waislam haiwasaidii.
 
We kweli ni mzushi.Elimu ya madrasa ni elimu kama elimu zingine,inalenga kupanua kichwa cha mtoto na wala sio kukidumaza kama unavyodhani.Mnajitahidi kuipiga vita lakini mmefeli kwa sababu kila msikiti sasa unakuta madrsa sambamba na chekechea.kwa hiyo mmeula wa chuya.
Waislam walipomfukuza mkoloni walikuwa wanaju umuhimu wa elimu lakini Nyerere aliwahujumu.Enzi za Nyerere shule za sekondari zilikuwa chache sana hata wale waliokuwa wanakwenda sekondari sio kwmaba walikuwa wanashinda bali walikuwa wanchaguliwa kwa upendeleo,enzi hizo kama mtoto hakuchaguliwa kwenda sekondari ndo mwisho wa elimu,hapakuwapo na sekondari za binafsi.Lkini sasa kwa sekondari za kata wewe toa muda tu ndo utagundua kwamba kumbe waislam nao wanzo bongo kali.
Waislm sio malofa kama unavyofikiria.Nenda barbara ya Pugu na Mandela hesabu vile viwanda na wamilki wake ndo uje utajua kuwa waislamu ni hodari wa kuwekeza na biashara.Hakuna mafuta hapa.Hata hiyo story ya Nijeria ni upotoshaji unaleta hoja za nguvu tu.Abuja mabo ndio mji wa kisasa zaidi Nijeria uko kaskazini kwa waislamu wengi.We achana na story za abunwasi.
asante kalamazoo umemjibu vizur sana huyu abunuwas
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom