Tusijidanganye: Watanzania hawatavumilia fisadi na ufisadi 2020

FISADI unampimwaje na ni viwango vipi vinavyo onyesha yule ama huyu ni fisadi au ukomo wa fikra ndio unakufanya useme fulani ni fisadi?.
 
FISADI unampimwaje na ni viwango vipi vinavyo onyesha yule ama huyu ni fisadi au ukomo wa fikra ndio unakufanya useme fulani ni fisadi?.
Wewe humjui FISADI,Ile list of shame iliyotembezwa mikoa karibia yote umeisahau??tafadhari msituletee mafisadi
 
Unafanya kosa kubwa na tena mnalirudia mara kwa mara humu, si watanzania wote ni wanachama au mashabiki wa vyama vya siasa mkuu. Wengi ni wale ambao hata uwepo wake tu unawakera, tena miongoni mwao ni graduates, usije ukadhani ni wasosoma tu. Pokea ushauri, mlifanya kosa ambalo hata waliokuwa members wa cdm waliwakacha, hivi huwa hamfanyi tafiti baada ya uchaguzi? Kuamini kwamba kulifanyika rafu hata kama zilikuwepo kunawapofusha, hamyaoni yaliyo dhahiri.
Ok mkuu labda nirudi kwenye point yako wewe unayejivika mwamvuli wa kutokuwa na chama.
Mind U kuna kuwa mpenz wa chama, shabiki wa chama na mwanachama wa chama. Wote hao naweza kusema wanafall kwenye kundi moja.
Ukisema huyo walikosea kumuweka uweke na statistics pia. Linganisha na ambaye ulitaka na ccm walitaka wapinzani wamsimamishe pamoja na uchakachuzi yupi alikuwa na wingi wa kura za watanzania unaojifanya kuwazungumzia
 
Teh teh....
Mahakama ya 'umma' inalishwa uongo na inakubali.
Ikishafanya maamuzi, inajutia maamuzi yake baadae.
Elimu ya 'umma' ingekuwa vizuri, ningeamini hukumu yao.
 
Wewe humjui FISADI,Ile list of shame iliyotembezwa mikoa karibia yote umeisahau??tafadhari msituletee mafisadi
Mahakama ipi imesema Fulani ni FISADI?.FISADI ni ukomo wako wa kufikiri,hiyo list sijawai hiona nafikiri ilikuwa ni political game,je wewe ukuwahi sikia Kijana aliyemwagiwa tindikali nakuzungushwa kwamba chama Fulani kilikodi watu wakumtesa na nicha kigaidi
 
Tahadhari hii inahusu 2020,chonde chonde vyama vyetu tunaviomba vituwekee watu safi wasio na mawaa sasa wewe unaleta 'historia'.uchaguzi wa 2015 ulishakwisha na hakuna uchaguzi mwingine utakaofanyika hapa katikati.
Halafu mbona ushauri huu umekaa vizuri tu lakini watu macho yanawatoka sana!mtapumua siku mtakapolitua hilo zigo lenu..!!
Zigo lipi mkuu lile lililohonga nyumba za serikali hawara zake alafu likafanya ufisadi manunuzi ya mv bagamoyo juzi kati likahitimisha kwa kupiga rambirambi?kama ni lile zigo kweli 2020 lazima tulitue kama Zanzibar walivyofanya tarehe 25/10/2015
 
Mimi nashauri na kutoa angalizo lakini mkijifanya kuwa na mioyo migumu mkamsimamisha FISADI 2020 basi msahau kushinda maana waTz tunayo'machale' tutamchagua asiye FISADI
Alafu mkuu 2020 hakuna fisadi atakayegombea coz mahakama ya mafisadi itakuwa imemshughulikia kipindi hicho atakuwa kashafungwa gerezani
 
Hata historia ya Zanzibar na bara ni tofauti sana, si pa kujifananisha nako. Zanzibar ni zaidi ya siasa na uchaguzi kwao. Tusijifanye hatuzijui historia za Zanzibar. Na kama mnaamini kuibiwa zikamateni nyoyo za watz ili wawasapoti hata kuandamana.
Kwa hiyo unakubali ushindi aliyeshinda uchaguzi zanzbar uliofanyika tarehe 25/10/2015 upo wazi
 
Mahakama ipi imesema Fulani ni FISADI?.FISADI ni ukomo wako wa kufikiri,hiyo list sijawai hiona nafikiri ilikuwa ni political game,je wewe ukuwahi sikia Kijana aliyemwagiwa tindikali nakuzungushwa kwamba chama Fulani kilikodi watu wakumtesa na nicha kigaidi
Kwanini tung'ang'anie 'aliyetuhumiwa' mbona katika vyama wapo watu SAFI wasio na tuhuma wengi tu?jama waTz tunasema kwa lugha nyepesi sana wala haiitaji kutumia nguvu nyingi 'Hatutaki MAFISADI'
 
Ni kweli mafisadi wasikubaliwe hata kidogo hasa mafisadi HAWA waliibuka sasa.
Mafisadi wa sasa ni hatari zaidi tuwakatae 2020.
Haiwezekani watanzania wanakufa kwa kipindupindu kwa kunywa maji machafu,
Watu wanakosa dawa hospitali,
Elimu iko mahututi,
Umaskini umeongezeka, halafu MTU mmoja kwa utashi anachukua mabilioni ya fedha anakwenda kujenga kiwanja cha ndege cha kimataifa kijijini kwake, anaweka trafficlight kijijini kwake, anaendesha nchi kwa ubaguzi,ukabila,uchama,na ukanda..
Hakika hatutawasamehe na hatutawasahau
2020.
HAPO UNAWAHMA CHADEMA NA CUF KI AINA MAMBO YA UKANDA, UKABILA, UCHAMA UBAGUZI NA UKOO.
 
Kama hukumu ya mafisadi ni fimbo ya umma wakati wa uchaguzi mahakama ya mafisadi iliwekwa kama pambo??...alafu mafisadi wapi unaoniuliza nawapenda...wale waliohonga hawara zao nyumba za serikali or wale waliotafuna na kutokomea na rambirambi juzi???
Wale walioinunua CHADEMA.
 
KANA KANSUNGU UMWELU said:
hayo ni mawazo finyu kanywe chibuku huko fisadi unawajua ?
Fisadi si wale wakina Mbowe, Lissu ,Lema, Kubenea na magazeti ya Mwanahalisi, Msigwa na viongozi wengineo walikua wakiwatamka hadharani kwa zaidi ya miaka kumi iliyopita. Au unataka kutuambia nini wewe. Rejea list of shame mama utaona.!
 
Mafisadi ni wabaya mno,tuungane tusiwaruhusu kuingia wataitafuna nchi hii kama mchwa.
Ndio maana watanzania walistukia dili mwaka jana. Eti wanataka kupenyeza mafisadi waingie ikulu kwa tiketi ya kuzungusha mikono na mabadiliko. Utapeli wa kisiasa wa hali ya juu. Watanzania wa leo hawa wana macho na masikio sikivu. Wait and see.
 
Back
Top Bottom