Tusidanganyane, CCM ya leo bila Nape au Mwigulu hakuna kitu

Wacha wajifanye hawaijui kazi ya nape na mwigulu yani hadi mwigulu akapewa jina la savimbi!! Ccm jiangalieni!!
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya mali ya urithi na ile ya kujihangaikia mwenyewe ktk kutafuta
 
Reshuffle ya baraza la mawaziri imekaribia, ni wazi Nape amekalia kuti kavu, kuna watu walikuwa mizigo kwa CCM, ukada wao uliotukuka ndio umewapa uwaziri na sio weledi. Mwiguli anaweza kuokaka na panga hili ila Nape hachomoi
 
KABLA YAO HAKUKUWA NA CCM? JAMANI ACHENI KUTUMIKA VIBAYA KWA MAHABA AU SHEKELI, CCM INA WATU WENGI SANA MUHIMU AMBAO HAO KINA NAPE NA MWIGULU HAWASTAHILI HATA KUFUA NGUO ZAO!
Hahahaha

Mkuu hata alipoondoka yule waliyemuita FISADI miaka minane leo wanamuita RAIS WA MIOYO YA WATU walisema CCM inakufa ila ikasimama, bado wanarudia propaganda zile zile
 
Unapata wapi nguvu ya kuwatofautisha hawa na CCM ya kileo?!

Unaanza vipi kuwapuuza hawa na ulevi wa madaraka na SIFA ya kijana ambaye hata kwalo hakuwa na msaada wowote wa kukikomboa chama tokea ndani ya dimbwi la kupotea km walivyopambana vijana hao(NAPE NA MWIGULU)?!

NAsikitika sana!Si kwa sababu ya vijana hawa waliopambana usiku na mchana kukikomboa chama wanavyotendwa leo Bali kwa HATARI iliyo kuu mbele ya chama chetu endapo hawa wakiendelea kupuuzwa.

Narudia,CCM ya kileo bila NAPE na MWIGULU, ni hapo.

Kila kazi ina malipo/mshahara wake, hivyo yatakayowapata Nape, Mwigulu na wengine huko CCM ni sawasawa tu kwangu.

CCM ya akina na Nape & Mwigulu ilikuwa mwiba kwa Tanzania in so many ways. Hawawezi kukwepa hicho kikombe, pia wako na wengine wengi huko ambao nao kwa wakati wao watakunywa mvinyo walioutengeneza.
 
Voice clip za Stephen Nyerere na Mama Wema zilikusudiwa kumpaisha Makonda whether was planned or tracked.

Pia kuwanyamazisha Wema,Msukuma, Nape na Mwigulu ambao kwa namna moja au nyingine wanatambua mchango wa Wema wakati wa kampeni.

Kubeza mchango wa Wema hakuondoi ukweli kwamba CCM ilizidiwa sana kwenye uchaguzi wa 2015 na ulitumia kila njia iliyokuwepo kujinasua whether ilikuwa legal or Illegal (Nape alikuwa mwenezi automatically Ali coordinate kilakitu kuhusu wasanii).Kazi ya kuwanasa wasanii ambao kwa wakati huo JK aliwapa nguvu sana ya kukubalika katika jamii including Wema ilifanikishwa na Mwigulu na Nape (ingawa walilalamikiwa sana kwa ku infrate tozo za wasanii - walipiga au la mi hayanihusu).

Ukizisikiliza zile clip kwanza zinatoa funzo kwamba jamii na uongozi tulionao katika vyama ni unstable and dependant on our ignorance (ukweli watanzania wengi ni wajinga na ukitaka kuwakamata vizuri watukuze kwa ujinga wao) ushaidi wa hilo angalia walivyoyumbishwa na kampeni.

Hitimisho: pamoja na juhudi za makonda kupiga vita madawa, anajua namna na wakati wa kuwashambulia wanaoingia kwenye rail yake. Naamini siku JPM akiimfahamu Daudi vizuri na anatumiwa na nani atakuwa amechelewa na adhabu yake ataibeba yeye.
Kifupi mpaka sasa JPM yuko alone, na ndio maana haamini mtu zaidi ya nafsi yake.
 
Mkuu huyu Makonda awe kakosea au hajakosea ila ana ujasiri wa kumwambia mtu wewe unafanya kitu flani kibaya. Kama alivyowataja watu wa unga au alivyowataja akina Rostam na Lowassa. Wazee ndani ya CCM walikuwa wanaona vurugu za Lowassa na Rostam lakini wengi walikosa ujasiri wa kuwaambia ukweli hadharani wakabaki wanapiga umbea chini kwa chini.

Na huo ujasiri ndio ambao tunaukosa kila mahali nchi hiii

Makonda atabaki kuwa unique hata waseme yote mabaya kuhusu yeye
 
Hao uliowataja hata wao CCM siyo mama wala baba yao; na wanalijua hilo. Wewe unaetoa povu hapa unashangaza sana.
 
Unapata wapi nguvu ya kuwatofautisha hawa na CCM ya kileo?!

Unaanza vipi kuwapuuza hawa na ulevi wa madaraka na SIFA ya kijana ambaye hata kwalo hakuwa na msaada wowote wa kukikomboa chama tokea ndani ya dimbwi la kupotea km walivyopambana vijana hao(NAPE NA MWIGULU)?!

NAsikitika sana!Si kwa sababu ya vijana hawa waliopambana usiku na mchana kukikomboa chama wanavyotendwa leo Bali kwa HATARI iliyo kuu mbele ya chama chetu endapo hawa wakiendelea kupuuzwa.

Narudia,CCM ya kileo bila NAPE na MWIGULU, ni hapo.
Wana CCM watakataa hili lakini hawa vijana (Nape, Mwigulu na Makamba) ni watu wenye ushaishi, fitina na wazuri kwenye propaganda nzuri za kutafuta kura .
 
Ila baada ya uchaguzi wa 2010 hao watu tajwa wamefanya kazi kubwa sana kuibomoa chadema kwa wale mnaokumbuka ile operation ya chini chini ndani ya chadema PM7 ilikuwa ikidhaminiwa na Mwigulu.Kuhama kwa wale vijana machachari enzi hizo akina Shonza, Mtela mwampamba,Festo Sanga na wengine wengi yalikuwa ni matunda ya Mwigulu na Nape
 
Mawaziri wenye muda wa kuongea na msanii masaa mawili,wanaongozaje wizara za serikali?Hawafai hata kwenye chama zaidi ya kuwa wachekeshaji wa mfalme.
Tanzania Maendeleo tusubirie sana
 
Nyinyi si mlishaambiwa na bwana yule alipambana mwenyewe hakuchangiwa na mtu..
Push-ups alipiga mwenyewe na kuacha kabisa kutegemea nguvu ya chama bali ya kwake mwenyewe sasa hao utamweleza vipi kuwa walimpiga
khaaaaaaaaaaa! ilikuwa vita ya mtu mmoja
 
Ila baada ya uchaguzi wa 2010 hao watu tajwa wamefanya kazi kubwa sana kuibomoa chadema kwa wale mnaokumbuka ile operation ya chini chini ndani ya chadema PM7 ilikuwa ikidhaminiwa na Mwigulu.Kuhama kwa wale vijana machachari enzi hizo akina Shonza, Mtela mwampamba,Festo Sanga na wengine wengi yalikuwa ni matunda ya Mwigulu na Nape
😀😀😀
 
Back
Top Bottom