Rwanda ina wataalamu wa kuiba madini Congo. Rwanda ilisomesha wataalamu hao kutoka "chuo cha misituni".Magufuli wenu anahitaji wataalamu kutoka Rwanda, kiuhalisia Rwanda ina wataalamu wa kutoka chuo gani? Na wana historia yoyote duniani? Jambo gani wamelifanya mpaka rais wetu akalainika kiasi hicho na kuonyesha mapenzi ya dhati kwao?
May be i miss some points?
Please Help!!
Saint Ivuga
Rwanda inapiga hatua kwa sababu Rais wao si "dikteta uchwara" ukileta "ujinga" anakutumia kikosi kinarudisha roho yako mbinguni na mwili wako ardhini. Ukileta upuuzi wa 5-10% anakutoa damu yote mwilini. Ili kufanikisha mipango ya maendeleo, Rais anawateua watu kwenye nafasi, utumishi kulingana na utaalamu wao na taaluma zao na hawaingilii sana. Kwa kuanzia amechukua wataalamu kutoka kila wanakopatikana wakiwemo watanzania.
Ukitaka kuanzisha biashara (kitega uchumi) hakuna kuzungushana wala kuonesha kadi ya chama.
Rais wao ana tatizo moja tu, hataki kusikia neno "DOMO-krasia". Ukijifanya unataka demokrasia ni sawa na kununua tiketi ya kwenda mbinguni mapema.
Vyuo ndio wanaviendeleza sasa ili kuzalisha nguvukazi inayohitajika kwa uchumi wa Rwanda.
Magufuli inabidi aache "uccm" wake na siasa majipu. Wataalamu na wanataaluma wa fani mbali mbali wapo Tanzania. Awape majukumu na awaamini , awapatie "visio yake" na vitendea kazi, ili kuhakikisha hawachezi au kuchezea imani na mali ya umma, apitishe sheria ya kunyonga au kupiga risasi hadharani kwa atakaetiwa hatiani kwa kupiga deals, udokozi au kuhujumu kazi aliyopewa.