Wacha1
JF-Expert Member
- Dec 21, 2009
- 16,681
- 8,241
Hatuwezi kumchagua raia wa Belgium kuongoza nchi.Sisi wananchi bila shaka tutakupa Urais miezi michache ijayo Mh. Tundu A. Lissu. Uadilifu na uzalendo wako kwa nchi hii ni wa kutukuka kila mtu mwenye Akili njema atakupa kura ya kuliongoza taifa hili.
Ila tunakueleza ukiwa Rais usifanye mambo ambayo hatukukutuma, jifunze kwa yule bwana Rais Magufuli. Wew nenda Ikulu kafanye mambo haya kwetu.
1. Fanya maendeleo kwa nchi na watu ila tuachie Uhuru na Demokrasia yetu.
2. Lipa wafanyakazi maslahi yao bora, Wapandishe vyeo kwa wakati.
3. Wakulima usitunyang'anye Mazao yetu na kupiga shangazi zetu ila tutafutie masoko ya uhakika .
3. Sisi wafanya biashara usitupole mali zetu na kutufunga bila hatia.
4. Acha Uhuru wa habari utamalaki usitubambikie kesi za uhujumu uchumi.
5. Tunaomba uwasake watu wasio julikana popote pale walipo.
6.Usihangaike kuua upinzani hatukukutuma hayo. Kuna jitu liliahidi kuwa upinzani utakuwa umekufa mwaka huu cha ajabu Upinzani unamuondoa yeye.
Wamefanya mikutano miaka yote mitano peke yao leo wanatetemeka wapinzani kuongea kwa muda wa miezi mitatu tuu wameanza kujinyea nyea huko walipo.
Mnahofu kitu gani hao wapinzani si wamesha jifia? Ninyi si mmefanya mengi mazuri kwa wananchi? Kiwewe cha nini jaman?
Nyerere wakati akitangaza vita na Idd Amini alisema hivi
"Wananchi tulieni muone vijana watafanya nini "
Na sisi Watanzania tunawaeleza ccm tulieni muone Watanganyika watafanya nini hapo Oktoba. Kichapo kile kile alicho chapwa Nduli Idd Amin Dadaa ndicho atakacho Chapwa huyo Pimbi Nduli wa pili mvuruga Amani yetu .
Maendeleo hayana vyama.