Tundu Lissu: Tusipoyasema haya juu ya kifo cha Ruge Mutahaba, mawe yatasema

Ni m
Sasa kama hukujua kuwa Ruge alikuwa kada wa CCM... aliyejijengea heshima na ukubalifu basi hata suala la Ruge na Makonda huwezi kulijua jinsi lilivyotatuliwa kwa ndani!

Ndio maana wenye hekima na busara husema, ndugu wakigombana chukua jembe ukalime...

Mambo ya kushabikia na kujihusisha na ugomvi wa ndugu wakati hata hujui vizuri mahusiano yao ni kukosa hekima na busara!

Wapinzani huwa wananishangaza na kunichekesha pale wanaposhabikia ugomvi wa wanaCCM bila kujua kuwa ugomvi wao ndio unawaimarisha zaidi katika vita vya kisiasa.

Hili la Ruge kuwa kada wa CCM aliyejijengea heshima liwe ni funzo kuwa CCM ina mizizi mirefu ambayo wale wanadhani wanaweza kuing'oa kwa makelele bila mbinu makini ni kupoteza muda na nguvu zao ndogo walizonazo.

Masuala kama haya kwa mtu mwenye akili pana akisikia CCM wanaposema wataendelea kuwa chama tawala atajua huwa hawatanii bali wanamaanisha!


Ni mpuuzi tuu anaweza kupigana na Lissu. Na kwa taarifa yako habari zanasambaa kwamba zoezi kakamilisha DAB
 
Tukisema huyu lissu ni mtu mwenye chuki , mnafiki na hasidi, wana chadema mtakasirika na kuanza kurushu matusi kwa uhodari wenu.

Hata kwenye misiba lazima yeye alete uchochezi kwa njia yoyote ile, na ni lazima atajiingiza kama kiongozi wa kugimbea haki na huku anachochea. This man is syco period. TL usitafute umaarufu kwenye misiba.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ungetoa maneno yako siku ilipovamiwa clouds siyo Leo ndiyo unaona unafiki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tundu Lissu wenda akawa hayuko sawa, ila wewe nyau ni mlopokaji kiherehere kama panya malaya..!

Sent using Jamii Forums mobile app
Panya wanapofanya mapenzi yao HAKUNA BINADAMU WA KAWAIDA ANAYEONA
Maana Panua huogopa Mwanadamu ndiyo maana hujificha

kama wewe unawatambua kuwa huyu panya ni MALAYA na huyu siyo MALAYA Maana yake Huwa UNAWAONA

KUMBE WW SIYO BINADAMU WA KAWAIDA
LAZIMA UTAKUWA MCHAWI.. MSHIRIKINA

magonjwa Mtambuka NAKUPA TAHADHARI

POPO BAWA HAWAJAWI KUFA
BADO WANGALIPO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KIFO CHA RUGE MUTAHABA: TUSIPOYASEMA HAYA, MAWE YATASEMA!!!

Ruge Mutahaba amefariki dunia nchini Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa. Ruge alikuwa mmojawapo wa wakurugenzi wa Clouds Media Group, mojawapo ya vyombo vya habari vikubwa hapa nchini.

Inaelekea huu ni msiba mkubwa sana kwa taifa letu. Viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, taasisi mbali mbali na wananchi wa kawaida wamejitokeza hadharani kutoa salamu zao za rambi rambi kwa ndugu, jamaa na marafiki zake marehemu Ruge.

Hii ni sawa sawa, kwani Ruge Mutahaba hakuwa mtu mdogo kwenye jamii yetu. Hivyo, na mimi naungana na waombolezaji wengine kumuomboleza kijana huyu.

Naomba nikiri mapema: mimi sikumfahamu sana Ruge. Nilikutana naye mara mbili au tatu aliponifuata Bungeni mwaka 2012 (kama sikosei) ili nisaidie kumpatanisha yeye na baadhi ya wanamuziki wa kizazi kipya, wakiongozwa na Mh. Joe Mbilinyi 'Sugu.' Nilifanya hivyo.

Zaidi ya hapo, nilimfahamu kwa juu juu kama mmoja wa wakurugenzi wa Clouds Media Group.

Kwa hiyo siwezi kumzungumza sana kwa mema au kwa mabaya yake. Siyafahamu sana. Ninachotaka kukizungumzia ni haya maombolezo ya kifo chake.

Sikujua kwamba kumbe Ruge Mutahaba alikuwa "... kada wa CCM... aliyejijengea heshima na ukubalifu..." kwa Chama hicho. Sikujua kwamba CCM ilimtumia Ruge sana wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Haya yote nimeyafahamu kufuatia kifo chake. Nimeyafahamu kwa sababu ya salamu za rambi rambi za Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole.

Kwenye hili kuna fundisho kubwa sana.

Mapema ya mwaka 2017, ofisi za Clouds Media Group zilizoko Mikocheni, Dar Es Salaam, zilivamiwa usiku na watu wenye silaha na sare za Jeshi la Polisi, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na wengine wakiwa wamevalia kiraia.

Watu hao waliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda alias Albert Bashite. Watu hawa walifanya uhalifu mbali mbali wa kijinai kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.

Kwa bahati nzuri, tukio hilo lilirekodiwa kwenye kamera za video za ulinzi (CCTV), ambazo marehemu Ruge na wafanyakazi wa Clouds Media Group walizisambaza mitandaoni. Kwa hiyo hadithi ya 'watu wasiojulikana' haikuwezekana kwenye tukio hilo la kihalifu.

Kwa sababu ya kelele na shinikizo kubwa la umma, Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni wakati huo, Mh. Nape Nnauye, aliunda Kamati ya Uchunguzi wa tukio hilo. Jukwaa la Wahariri (TEF) na Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT) nao waliunda Kamati za Uchunguzi.

Wachunguzi wote hawa walithibitisha pasina shaka yoyote kwamba Mkuu wa Mkoa Makonda aliongoza uhalifu huo. Kwa hiyo ukweli wa uhalifu huo haubishaniwi.

Hata hivyo, mara baada ya kupokea taarifa ya Kamati ya Uchunguzi aliyoiunda, Waziri Nape Nnauye alifukuzwa kazi na Rais Magufuli.

Na alipojaribu kufanya mkutano wa waandishi habari kuelezea tukio hilo, alizuiliwa kufanya hivyo kwa mtutu wa bastola ya maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa na Ujasusi (TISS).

Na hii nayo haina ubishi maana ilifanyika mchana kweupe na picha za video za tukio zilisambazwa mitandaoni.

Jeshi la Polisi halikuchukua hatua yoyote ya kisheria dhidi ya Mkuu wa Mkoa Makonda na wavamizi wenzake wa Clouds Media Group, wala maafisa wa usalama wa taifa waliomtishia Nape Nnauye kwa bunguki. Rais Magufuli naye hakuchukua hatua zozote dhidi ya mteule wake Makonda.

Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), kupitia kwa Baraza lake la Uongozi, lilitoa kauli ya kulaani vikali uhalifu uliofanywa na Mkuu wa Mkoa Makonda na wavamizi wenzake. TLS iliazimia kufungua mashtaka ya jinai ya binafsi dhidi ya wahalifu hao, lakini hilo halikufanyika kufuatia kushambuliwa kwangu kwenye jaribio la mauaji la Septemba 7, 2017.

Kwa vyovyote vile, tukio la uvamizi wa Clouds Media Group halikushughulikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.

Ni heshima kwa marehemu Ruge Mutahaba kwamba, licha ya shinikizo kubwa la kumnyamazisha, alipiga kelele kubwa hadharani.

Licha ya kuwa 'kada mkubalifu' wa CCM, hakukaa kimya mbele ya uovu uliofanywa dhidi ya Clouds Media Group na wafanyakazi wake. Aliwataja wale waliomfanyia yeye na Clouds Media Group na wafanyakazi wake uhalifu.

Hata hivyo, wale aliowasaidia kupata madaraka ya kisiasa kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita walimsaliti Ruge Mutahaba.

Rais Magufuli aliingilia kati kwa upande wa Mkuu wa Mkoa Makonda na wavamizi wenzake. Rais Magufuli alimfukuza kazi Waziri Nape Nnauye aliyejaribu kuingilia kati kwa niaba ya Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na wafanyakazi wake.

Jeshi la Polisi halikuingilia kati. Liliangalia upepo uliokuwa unavuma kutoka Ikulu ya Magogoni likaamua kukaa kimya.

Chama cha Mapinduzi nacho halikuingilia kati wala kutoa kauli yoyote ya kumuunga mkono. Kiliangalia mwelekeo wa Mwenyekiti wake na kunyamaza kimya.

Sasa Ruge Mutahaba amefariki dunia. Sasa hatasema tena. 'Dead people tell no tales.' Sasa ni salama kwa wabaya wake kujitokeza hadharani na kumlilia machozi ya mamba.

Rais Magufuli amemwita 'kijana wake.' Wakati Ruge na Clouds Media Group walipovamiwa, Rais Magufuli alisimama upande wa wavamizi na 'kijana wake' mwingine, Paul Makonda aliyeongoza uvamizi huo.

Sasa Mkuu wa Mkoa Makonda, kiongozi wa wavamizi, anamtaja mvamiwa kama "... kijana mchapakazi, mwenye nidhamu na mzalendo wa kweli."

Sasa Chama alichokisaidia kupata madaraka halafu kikamkimbia wakati wa shida yake kinadai Ruge alikuwa na 'ukubalifu' ndani ya Chama hicho. Dead people tell no tales.

Sasa ni wakati wa wanafiki kujitokeza hadharani, na wachawi kulia kwa uchungu kuliko waliofiwa.

Ni lazima tuyaseme haya sasa na hadharani. Tusipoyasema, hata mawe yatasema.

Mwenyezi Mungu ampe marehemu Ruge Mutahaba mapumziko ya amani. Na Mwenyezi Mungu atupe sisi tulio hai nguvu na ujasiri wa kusimama na kupaza sauti zetu kwa niaba ya akina Ruge waliopo na wale wajao.

Tundu Lissu, UZ Leuven, Gasthuisberg, Leuven, Ubelgiji, 27 Februari, 2019
Naomba kuuliza.. hivi TLS ni taasisi au kilikua ni chama kilichoongozwa na mtu mmoja? Maana kwenye paragraph ya 18 ya hili andiko anasema 'TLS kupitia baraza lake la uongozi iliazimia kufungua kesi dhidi ya Uvamizi wa Clouds Media Mwaka 2017. Lakini baada yeye kushambuliwa, kesi hiyo haikufunguliwa tena. Sasa kuna uhusiano gani kati ya kushambuliwa kwa Lissu na kufungua kesi mahakamani? Aliyetakiwa kufungua kesi ni Lissu au TLS? Na je, TLS ina uhalali huo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nianze Kwa kukupa pole mheshimiwa TUNDU Kwa yote uliyopata. Lkn nasikitika kuona unavyopenda Shari zaidi kuliko Amani. Tunaomba siasa ziwe na mipaka wkt WA matatizo si wkt muafaka kuleta agenda za kisiasa. Nilifurahi ulipojibu wkt ukihojiwa Hilo USA kuwa hata ulipofiwa na mdogo wako Rais JPM alikuwa na wewe japo yeye ni CCM NA WW CDM. Wkt wa matatizo tuwe wamoja km Taiga kuliko kuleta hoja za kikatili. Inaobekana mheshimiwa bado ana matatizo ya ki saikolojia naomba apatiwe msaada. Wengine hata TUNDU akikohoa Tu utasikia hakuna mtu km yeye. Pole wafiwa Kwa msiba wa Mtanzania mwenzetu Ruge.
 
TLS iliazimia kufungua mashtaka ya jinai ya binafsi dhidi ya wahalifu hao, lakini hilo halikufanyika kufuatia kushambuliwa kwangu kwenye jaribio la mauaji la Septemba 7, 2017.

Tangu mwanzoni mwaka mpaka September TUNDU alikuwa akisubiri nini? Km siyo uongo na unafiki mkubwa. TLS ni taasisi na siyo mtu mmoja labda km alitaka kutumia vibaya madaraka ya kuwa Rais wa TLS. Km agenda ilikuwa ya taasisi hata baada ya LISU kesi ingefunguliwa.
 
1. Watu aina ya Lissu wanaamini mkikosana hamuwezi kuyamaliza ngazi ya jamii - Hii ni hatari sana.
2. Watu wa aina ya Lissu ahawawezi kuongea bila kumuingiza JPM kwenye kila maneno ya kinywa chao - Huu ni ugonjwa mkubwa mno, mtafutieni tiba.
3. Sasa Lissu hajui kwamba JPM aliwapatanisha Makonda na Ruge pale Tanga na kuashiria kwamba wote ni vijana wake - Hii inaitwa kupindisha ukweli huwezi eleweka katika jamii.
4. Lissu karaka zako zimeshaanza kupoteza mvuto lambda ubadirishe style. JPM ameshakuwini hutoboi kwa kumfanyia chuki binafasi.
 
Sasa kama hukujua kuwa Ruge alikuwa kada wa CCM... aliyejijengea heshima na ukubalifu basi hata suala la Ruge na Makonda huwezi kulijua jinsi lilivyotatuliwa kwa ndani!

Ndio maana wenye hekima na busara husema, ndugu wakigombana chukua jembe ukalime...

Mambo ya kushabikia na kujihusisha na ugomvi wa ndugu wakati hata hujui vizuri mahusiano yao ni kukosa hekima na busara!

Wapinzani huwa wananishangaza na kunichekesha pale wanaposhabikia ugomvi wa wanaCCM bila kujua kuwa ugomvi wao ndio unawaimarisha zaidi katika vita vya kisiasa.

Hili la Ruge kuwa kada wa CCM aliyejijengea heshima liwe ni funzo kuwa CCM ina mizizi mirefu ambayo wale wanadhani wanaweza kuing'oa kwa makelele bila mbinu makini ni kupoteza muda na nguvu zao ndogo walizonazo.

Masuala kama haya kwa mtu mwenye akili pana akisikia CCM wanaposema wataendelea kuwa chama tawala atajua huwa hawatanii bali wanamaanisha!

Wapo pia wanaoshangaa jinai kumalizwa kindani ndani; hiyo itakuwa ni nchi au fiefdom? Hiyo kadhia wala haikumalizwa kindani ndani bali kimabavu na wenye mamlaka!
 
Back
Top Bottom