Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,515
4,017
Makamu Mwenyekiti CHADEMA, Tundu Lissu akizungumza kwenye Kikao amehoji;

"Wananisema kuwa sina Pesa, siwezi kuendesha Chama, hebu watueleze pesa za Jana usiku zilitoka kwa nani? Tumeshuhudia vitendo vya rushwa kwenye Uchaguzi wa BAVICHA"
IMG_2520.jpeg

Soma, Pia:

Kimeumana! mjumbe adakwa akidaiwa kugawa nauli uchaguzi Bavicha

BAVICHA watoa ufafanuzi mazingira ya rushwa kwenye uchaguzi wao

Uzi maalumu wa matokeo Uchaguzi wa Baraza la Vijana (BAVICHA) na Baraza la Wazee (BAZECHA) CHADEMA Taifa 2025
 
Sasa badala ya kutuuliza si atwambie, au na yeye hajui ? Nadhani yupo kwenye nafasi nzuri tu ya kuwauliza hao waliopokea hizo pesa na kama walitakiwa au hawakutakiwa kuzipokea...

Nishasema kama Rushwa inatamalaki basi mfumo mzima au Taasisi nzima ndio ina mapungufu na sidhani kama kubadilisha mtu pale juu ndio itakuwa mwarobaini, jitihada kubwa zaidi inatakuwa na pamoja na kutokuwa na uwezekano tena wa Mwenyekiti kuwa na nguvu kiasi hiki (Be it ni Lissu au Mbowe)
 
Makamu Mwenyekiti CHADEMA, Tundu Lissu akizungumza kwenye Kikao amehoji;

"Wananisema kuwa sina Pesa, siwezi kuendesha Chama, hebu watueleze pesa za Jana usiku zilitoka kwa nani? Tumeshuhudia vitendo vya rushwa kwenye Uchaguzi wa BAVICHA"
View attachment 3201902
Soma, Pia:

Kimeumana! mjumbe adakwa akidaiwa kugawa nauli uchaguzi Bavicha

BAVICHA watoa ufafanuzi mazingira ya rushwa kwenye uchaguzi wao

Uzi maalumu wa matokeo Uchaguzi wa Baraza la Vijana (BAVICHA) na Baraza la Wazee (BAZECHA) CHADEMA Taifa 2025
anamuuliza nani sasa wakati yeye ndie kiongozi wa kamati ya maadili chadema Taifa 🐒
 
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Yericko Nyerere ametoa tuhuma kuwa Dola na CCM wanaingilia uchaguzi na wanamtaka Lissu kwa nguvu.
1736945911083.png
Wamejificha weeee hatimaye wamejitokeza hadharani!

Halafu mwanachama halisi anainuka anasema Lissu anafaa kuwa mwenyekiti bila kujua nyuma yake kuna agenda gani? Wajumbe wa Mkutano Mkuu msifanye makosa yatakayokigharimu Chama chetu!

Dola na CCM yake wanaingilia uchaguzi wanamtaka Lissu kwa nguvu kubwa wametoa pesa na wanafanya kampeni za Wazi kabisa, Malengo yao ni kuwa Lissu ni mropokaji tu asiyeweza kuongoza taasisi ya Kisiasa inayohitaji hekima, busara na USIRI mkubwa, Kwamba Lissu hana uwezo wa kutafuta pesa ya kuendeshea chama, Kwamba Lissu akiwa Mwenyekiti hakuna Taasisi wala Watu wa Heshima nchini na nje ya Nchi watakaoshirikiana na Chadema kwakuwa Mwenyekiti wake Lissu HANA SIRI, ni Mropokaji kwa chochote watakachoshirikiana nae! Na hivyo Chama kitamfia ndani ya miezi michache tu baada ya kuchaguliwa na CCM itabaki salama dhidi ya Chadema ya Lissu.

CCM inaamini akina Lema ni wahuni tu wasioweza hata kujitafutia pesa ya kulisha familia zao badala yake wao na Familia zao wanalishwa na Serikali za Canada na Ubelgiji kama wakimbizi wa Kisiasa. Kwavyovyote vile, hawawezi kuongoza chama cha siasa Tanzania ambacho kukiongoza unatakiwa kuwa na Maarifa, misuli ya uchumi, busara na hekima.

Wajumbe epukeni mihemko, Lindeni Chama chenu, Mchagueni Mh Freeman Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti. Freeman Mbowe ana hekima, ana busara, msikivu, ana uthubutu na anaeleweka kwa kila mtu!
 
Back
Top Bottom