Tundu Lissu: Ninampinga Magufuli hadharani. Sio mnafiki na sijahongwa

Lissu tangu lini ulikuwa mzalendo! Uzalendo wa kutetea fisadi lowasa, au uchumia tumbo upi anausema zaidi ya huu wa kupewa kitu kidogo kumsafisha mtu aliye mchafua kwa miaka 10. Lissuu wadanganye vipofu wa vabichaa
Kweli kabisa ulichoongea. Hata mi uzalendo wake siuoni maana Lowassa ndo mwenye Acacia na ndo anayewaibia dhahabu na kusafirisha mchanga.

Kwa akili hii usipochukua nafasi ya Muhongo, utakuwa umeonewa na udai haki yako.
 
18622446_1126398777465538_2060351389369899505_n.jpg

Na mimi ni Mtanzania pia.

Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii: Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya tangu mwaka '99.

Wakati huo tulikuwa na mgodi mmoja tu wa dhahabu, Resolute Golden Pride Nzega. Bulyanhulu ilikuwa haijajengwa. Geita ndio kwanza walikuwa wanafukuza wanakijiji wa Mtakuja.

Nadhani nilikuwa wa kwanza katika nchi hii kupiga yowe kwamba tutaibiwa sana kwenye sekta ya madini.

Wewe sijui ulikuwa wapi wakati huo. Najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa MaCCM na wawekezaji hawa.

Nimepigana na wawekezaji hawa mahakamani, kwenye medani ya kisiasa ndani na nje ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 15. Nimetetea wananchi completely free of charge Bulyanhulu, Tarime, Nzega, Geita, n.k.

Sijui wewe ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa upande wa nani: wa MaCCM na wanyonyaji hawa.

Soma Rai ya tarehe 17 Julai, 2001, uone tulimwambia nini Mkapa siku anaenda kuzindua Mgodi wa Bulyanhulu.

Sijui ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa wapi: alikuwa anatetea tumbo lake na matumbo ya wanyonyaji hawa.

Nilikamatwa na kushtakiwa kwa uchochezi kwa sababu ya Bulyanhulu. Hiyo ilikuwa December 2002. Nilikaa na kesi hiyo mahakamani Kisutu kwa miaka sita.

Sijui ulikuwa wapi ila najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa watesi wa wananchi na wanyonyaji wa rasilmali zetu.

Leo Magufuli anajifanya mzalendo na anahoji uzalendo we yeyote anayepingana nae.

Ni muongo. Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata. Kwa siku chache tu. Mark my words: ataumbuka na mtaumbuka.

Mimi ninampinga hadharani. Sio mnafiki, na sijahongwa. Ninampinga kwa sababu atatusababishia matatizo makubwa zaidi kuliko tuliyonayo sasa.

Huo mchanga atauachia upelekwe ambako umepelekwa kwa miaka 16 iliyopita. Kama sheria ndiyo hiyo na mikataba ndiyo hiyo hana pakwenda.

Tatizo ninaloliona ni kwamba by the time anawarudishia mchanga wao, Tanzania itakuwa imekuwa a basket case kama Zimbabwe.

Na tutakuwa tumelipishwa mapesa mengi kama fidia na arbitral tribunals za kimataifa kwa kuvunja mikataba na wawekezaji hawa.

Kama kuna anayefikiri uzalendo ni kufumbia macho masuala haya basi huyo na amuunge mkono Magufuli kwenye upofu wake wa kujitakia.

Ripoti ya Prof. Mruma haitamaliza hata nusu saa under serious scrutiny. Zaidi ya majina ya maprofesa walioiandaa, ripoti hii haina credibility yoyote. Ni kazi ya kisiasa iliyopakwa rangi ya usomi.

Kama umefuatilia taarifa za kitaalamu za Bulyanhulu hata kabla ya Barrick Gold kuingia mwaka '99 utajua ninasema nini.

Sutton Resources, Outukumpu Oy na hata STAMICO walishafanya utafiti mkubwa juu ya utajiri wa Bulyanhulu. Taarifa zipo na zimekuwepo kwa hata mbumbumbu wa jiolojia ya madini kama mimi.

Hiki alichoambiwa Magufuli ni rubbish, hata kama ni ya kiprofesa. Rubbish. Hatuibiwi kwenye mchanga, that's the rubbish fed on the unlettered.

Tunaibiwa kwenye sheria. Kama hamuoni hilo then God have mercy on us.
I'm waiting anxiously for Tundu Lissu to be next President of Tz come 2020
 
"Hiki alichoambiwa Magufuli ni rubbish, hata kama ni ya kiprofesa. Rubbish. Hatuibiwi kwenye mchanga, that's the rubbish fed on the unlettered".

wazungu walijaribu kupunguza makali wakasema hivi:
If the amount of gold in our concentrates was in line with the Committee findings, then it implies that both Bulyanhulu and Buzwagi would produce more gold than any other mine in the world. Sadly this is not the case.
 
Najiuliza sana swali dogo tu kila nikiona post ya Lisu kiufupi nasubiri apost kuwa amepima yeye au kashuhudia upimaji wa huo mchanga na kajiridhisha kuwa hatuibiwi,nitamuelewa sana,tofauti na hapo aendelee kusoma takwimu na historia kwenye makaratasi hadi pale atakapo ikomboa nchi kwa takwimu na sheria

Mkuu;
Kumchukia Lissu hadi anachokiandika hakutusaidii. Msome tu taratiib utaelewa anaandika nini hapo. Amesema; Hatuibiwi kwenye makontena bali tunaibiwa kwenye mikataba tuliyokwisha weka mkono kuwa ni mikataba hallal. Upo hapo?? Sasa tunapofoka kuwa Lissu ni kichaa, Lissu ni taahira, Je tumeuona huo mkataba?? Huenda mwenzetu amefanikiwa kuuona, mimi na weye tumeuona?? What do yu understand about "Transparency?" Hii kitu imefichwa fichwa hata kwa ma bush lawyers wetu ambao wangeweza kwa magumashi wakaona tundu hilo la kutufungia goli hata la mkono. Tukawaambia wale wanasheria wetu waende wakiwa wamejitayarisha.
Mtabaki kumbeza Tundu Lissu mkamwacha Joka aliye weka mkono kwa niaba yetu. Mpaka mmempa uenyekiti wa Bunge!! It is a shame man!! Huku mnabaki kuwaita wengine oil chafu na makapi. Tujifunze kusoma kinacho andikwa tujibu kimantiki kama kwamba sasa tupo kwenye hiyo Tribunal ya kimataifa tunajibu maswali. Hii ni lazima ije kutokea ACACIA hawataachia sega la asali hivi hivi
 
18622446_1126398777465538_2060351389369899505_n.jpg

Na mimi ni Mtanzania pia.

Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii: Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya tangu mwaka '99.

Wakati huo tulikuwa na mgodi mmoja tu wa dhahabu, Resolute Golden Pride Nzega. Bulyanhulu ilikuwa haijajengwa. Geita ndio kwanza walikuwa wanafukuza wanakijiji wa Mtakuja.

Nadhani nilikuwa wa kwanza katika nchi hii kupiga yowe kwamba tutaibiwa sana kwenye sekta ya madini.

Wewe sijui ulikuwa wapi wakati huo. Najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa MaCCM na wawekezaji hawa.

Nimepigana na wawekezaji hawa mahakamani, kwenye medani ya kisiasa ndani na nje ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 15. Nimetetea wananchi completely free of charge Bulyanhulu, Tarime, Nzega, Geita, n.k.

Sijui wewe ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa upande wa nani: wa MaCCM na wanyonyaji hawa.

Soma Rai ya tarehe 17 Julai, 2001, uone tulimwambia nini Mkapa siku anaenda kuzindua Mgodi wa Bulyanhulu.

Sijui ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa wapi: alikuwa anatetea tumbo lake na matumbo ya wanyonyaji hawa.

Nilikamatwa na kushtakiwa kwa uchochezi kwa sababu ya Bulyanhulu. Hiyo ilikuwa December 2002. Nilikaa na kesi hiyo mahakamani Kisutu kwa miaka sita.

Sijui ulikuwa wapi ila najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa watesi wa wananchi na wanyonyaji wa rasilmali zetu.

Leo Magufuli anajifanya mzalendo na anahoji uzalendo we yeyote anayepingana nae.

Ni muongo. Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata. Kwa siku chache tu. Mark my words: ataumbuka na mtaumbuka.

Mimi ninampinga hadharani. Sio mnafiki, na sijahongwa. Ninampinga kwa sababu atatusababishia matatizo makubwa zaidi kuliko tuliyonayo sasa.

Huo mchanga atauachia upelekwe ambako umepelekwa kwa miaka 16 iliyopita. Kama sheria ndiyo hiyo na mikataba ndiyo hiyo hana pakwenda.

Tatizo ninaloliona ni kwamba by the time anawarudishia mchanga wao, Tanzania itakuwa imekuwa a basket case kama Zimbabwe.

Na tutakuwa tumelipishwa mapesa mengi kama fidia na arbitral tribunals za kimataifa kwa kuvunja mikataba na wawekezaji hawa.

Kama kuna anayefikiri uzalendo ni kufumbia macho masuala haya basi huyo na amuunge mkono Magufuli kwenye upofu wake wa kujitakia.

Ripoti ya Prof. Mruma haitamaliza hata nusu saa under serious scrutiny. Zaidi ya majina ya maprofesa walioiandaa, ripoti hii haina credibility yoyote. Ni kazi ya kisiasa iliyopakwa rangi ya usomi.

Kama umefuatilia taarifa za kitaalamu za Bulyanhulu hata kabla ya Barrick Gold kuingia mwaka '99 utajua ninasema nini.

Sutton Resources, Outukumpu Oy na hata STAMICO walishafanya utafiti mkubwa juu ya utajiri wa Bulyanhulu. Taarifa zipo na zimekuwepo kwa hata mbumbumbu wa jiolojia ya madini kama mimi.

Hiki alichoambiwa Magufuli ni rubbish, hata kama ni ya kiprofesa. Rubbish. Hatuibiwi kwenye mchanga, that's the rubbish fed on the unlettered.

Tunaibiwa kwenye sheria. Kama hamuoni hilo then God have mercy on us.
Nimesoma maneno ya hasira sana haya. Ila sijafanikiwa kujua anajibu swali gani aliloulizwa.
 
Kinacho nishangaza mm nikwamba Mafisadi wapo ndani ya Ccm kira kukicha tunasikia wanafukuzwa na hawaishi lakini pia hawapelekwi mahakani nadhani hakuna hata msafi mmoja
ila vijana wa Rumumba hawaoni hilo serekali niyao nawanaoingia mikataba mibovu niwao halafu wanakaa kwenyetivi na kusema kunawatu mafisadi wakati ni wao we nyewe
 
Na kwa kuongezea tu, namnukuu na Mh. John Mnyika (Mb) mwaka 2012...

14 Oktoba, 2012

Tarehe 27 Julai 2012 kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani niliitaka Serikali kueleza ni kwanini mpaka sasa kiasi cha dola milioni 20.1 zilizopunjwa kifisadi hazijareshwa na kuitaka serikali iache kutumia kisingizio cha kuundwa kwa Timu ya Majadiliano (GNT) kuchelewesha utekelezaji wa maazimio, suala ambalo Wizara ya Nishati na Madini itapaswa kueleza hatua iliyofikiwa iwapo Spika atazingatia mwito huu na kuchukua hatua za haraka.

Ifahamike pia kwamba mwaka 2011 kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini niliitaka serikali kuweka wazi bungeni na kwa umma mikataba ya madini, mafuta na gesi asili katika nchini ili kuongeza tija na uwajibikaji.

Aidha nilitoa mwito mwito kwa wananchi na wabunge kuongoza marekebisho ya kikatiba na kisheria ili kuweka vifungu vya kulazimisha uwazi katika mikataba katika hizo muhimu kwa uchumi na usalama wa nchi.

Uwazi katika mikataba utadhibiti pia mianya ya ufisadi miongoni mwa baadhi ya watendaji wa serikali kwa kuwa mikataba hiyo itajadiliwa na umma na hivyo kupunguza uwezekano wa viongozi kutanguliza maslahi binafsi na kuwa na mikataba bora ya baadaye yenye kuzingatia maslahi ya umma.

Usiri katika mikataba ni tatizo kwa sababu masharti kama ya kushughulikia madhara ya kimazingira na kuchangia katika huduma za jamii pamoja na kulipa kodi zinazokusudiwa yanaweza yasitekelezwe kwa ukamilifu kama hayatafahamika kwa wabunge na umma. Aidha, ipo mikataba yenye vifungu ambavyo vinakinzana na sheria nyingine ama vinalinda kupindukia makampuni dhidi ya sheria nyingine za nchi zinazotungwa masuala ambayo yanaingilia mamlaka ya bunge ya kutunga sheria na kuisimamia serikali.

Sheria mpya ya madini Tanzania ya mwaka 2010 ina kifungu kinachotaka uwazi hata hivyo kimejikita katika uwazi wa rekodi na ripoti hakijaweka bayana mfumo wa uwazi katika mikataba ya madini, sheria ya mafuta nayo haina kifungu cha uwazi katika mikataba na sheria ya gesi haipo kabisa; hali ambayo inahitaji kurekebishwa.

Pamoja na mapato uwazi katika mikataba utachangia katika kupata tija ya ziada katika uchimbaji kwa kulinda maslahi ya wafanyakazi na kuweka mfumo mzuri zaidi wa makampuni kununua bidhaa za ndani kwa majibu wa vifungu vya mikataba hali ambacho itawezesha rasilimali kunufaisha wananchi wengi zaidi.

Uwazi katika mikataba utawezesha wabunge na wadau wengine kusimamia ipasavyo taasisi za kiserikali kuhusu mifumo ya kifedha na kibenki ambayo itaongeza mchango wa sekta za nishati na madini katika kuimarisha uchumi kwa kudhibiti mfumuko wa bei na kuporomoka kwa sarafu wakati huu ambapo thamani ya mauzo imeongezeka duniani lakini mzunguko umejitika katika masoko na mabenki ya nje.

Kwa ujumla, uwazi katika mikataba utapanua pia uwajibikaji wa kuongeza umiliki wa nchi na wananchi wa michakato ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asili.

Pamoja na kuwa ibara ya nne ya katiba inasema kwamba rasilimali na mali asili zote ziko chini ya usimamizi wa serikali; na ibara ya 63 inaeleza kwamba bunge ndicho chombo kikuu cha kuisimamia serikali kwa kutunga sheria na kupitisha mipango, katiba haijalazimisha mikataba ya madini, mafuta na gesi kuridhiwa na bunge hivyo katika kipindi cha sasa mikataba hiyo iwasilishwe kwa rejea na mapitio.

Katika muktadha huo, tarehe 4 Oktoba 2012 nilimtaka Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo afute taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo kuwa lengo la agizo lake la kupitiwa kwa mikataba yote 26 ya utafutaji mafuta na gesi asili ni “kuhakikisha kwamba endapo kuna mapungufu katika mikataba hiyo, mapungufu hayo yasijirudie tena katika mikataba mipya ya baadaye” kwa kuwa ikiachwa ilivyo italinda ufisadi na kukwaza utetezi wa rasilimali za taifa.

Nilieleza kwamba ufafanuzi uliotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini unatoa mwanya kwa mikataba mibovu kulindwa wakati ambapo kuna madai tuliyotoa toka mwaka 2011 kwamba baadhi ya mikataba hiyo imeingiwa kifisadi na mwaka huu wa 2012 zimeibuka tuhuma za vigogo wa serikali kuingiziwa fedha kifisadi katika akaunti zao za nchini Uswisi na makampuni ya nje ya utafutaji mafuta na gesi asili.

Aidha, pamoja Serikali kuwasilisha bungeni mikataba inapaswa pia kuwasilisha mipango kabambe (master plan) ya mafuta na gesi asili yenye kuzingatia mabadiliko ya kisera na kimfumo yenye kuwezesha nchi na wananchi kunufaika na rasilimali husika.

Kauli hii nimeitoa leo tarehe 14 Oktoba 2012 ikiwa ni Siku ya Kumbukumbu ya Hayati Julius Nyerere ambaye alipinga ufisadi na kutaka rasilimali za nchi zitumike kwa manufaa ya maisha ya wananchi:

John Mnyika (Mb)
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini

NB: John Pombe Magufuli ni miongoni mwa wabunge/mawaziri wa CCM waliokuwa mstari wa mbele kudai mikataba ni siri haiwezi kutolewa kwa wananchi. Miongozi mwa wabunge vijana waliomtetea Prof. Sospeter Muhongo wakati huo ni Dr. Hamisi Kigwangala akiunga mkono mikataba kuendelea kuwa siri. Ajabu ni kwamba leo kwa unafiki na bila haya anao ujasiri wa kusimama bungeni na kumtuhumu Muhongo eti kwa uongo uliotukuka!

Kwa kweli Wapinzani walijitahidi sana...tatizo ni Chama cha Mapinduzi na serikali yake ambamo John Pombe Magufuli alikuwa sehemu yake kwa miaka zaidi ya 20; miaka 10 chini ya Mkapa na miaka mingine kumi chini ya Kikwete kwenye ngazi ya uwaziri. Wakati huo wazalendo kama Tundu Lissu wanawapigania wananchi hadi kusweka ndani kwa kutetea rasilimali za taifa.
 
Back
Top Bottom