Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Wakuu, hotuba ya Kamanda Lissu Bungeni jana nina uthubutu wa kusema, tena kwa ujasiri kwamba tangu Tanganyika huru iwepo hatujawahi kushuhudia hotuba kali kama ile. Ni hotuba ya kisomi iliyojaa kila aina ya vielelezo na ushahidi, zaidi ya vielelezo 70 (footnotes), sio mchezo.

Ili kukata mzizi wa fitna nawaomba advocates wa Serikali 2 waje na ushahidi na vielelezo visivyo na shaka kukanusha paper ya Kamanda Lissu na sio kupayukapayuka bila mpango wala hoja za maana. I can see kwanini jamaa wanang'ang'ania Serikali 2 kwa udi na uvumba lakini bahati mbaya kwao kadiri wanavyozidi uking'ang'anizi wao ndivyo wanavyozidi kuharibu na kuachwa uchi wa nyama.

Poleni watetezi wa Serikali 2 ambao mnadhani mna akili na uzalendo kuliko Jaji Joseph Warioba, the former Attorney General of the Republic, Prime Minister and VP; kuliko Dr. Salim A. Salim, the former Minister for Defence, Primer Minister, and OAU Chief; kuliko Judge Brig. Gen. Augustine Ramadhan, the former high ranking member of the People's Armed Forces, NEC Chair, and the Chief Justice of the Supreme Court of the People of Tanzania; kuliko magwiji wengine lukuki waliokuwa wamejazana kwenye Tume ya Warioba. Jengeni hoja mueleweke kama Kamanda Lissu alivyofanya na sio kupayuka kama wendawazimu.

Nilistuka sana kusikia eti Nape Nnauye, W. J. Malecela, na Madabida eti wanazunguka huko na huko "kumjibu" Warioba na timu yake iliyojaa vichwa! Are we serious? Kafulila aliuliza Bungeni, hivi Warioba ni binadamu wa kutukanwa nchi hii? Hata kama alifanya makosa anapaswa kukosolewa kwa staha sio kwa matusi ya dhahiri au ya kificho. Kama kweli ni waungwana, CCM wanapaswa kumwomba msamaha Mzee Warioba na watanzania kwa ujumla.

Nakala: Pasco, Chris Lukosi, et. al.

Acha fedha iitwe fedha kwa kweli inadhalilisha unakuta mtu na akili zake kabisa tena za kutosha kwa sababu ya noti anaamua kuwa -------- na mjinga big sana jaji Warioba,Dr Salim,jaji Agustino Ramadhan wote tunajua mna hela za kutosha za kuwafanya muishi vizuri for the rest of your lives still mmeonesha ujasiri uzalendo wa kweli na mmesimamia ukweli na matakwa ya wengi acha hao wapenda noti wawaangushe ila sisi wananchi tumewaelewa vizuri ukweli utasimama haijalishi ni lini Tanganyika itarudi tu
 
Mimi nipotoshe ili inisaidie nini?.

Mh. Tundu Lissu alianisha mambo manne katika muktadha wa makundi ndani ya CCM na kila jambo lilikuwa na kundi lake. Jambo la nne lilikuwa linamhusu Mwl. Nyerere na siasa za Zanzibar kama nilivyobainisha hapo juu.

Jaribu kuangalia video yake ili upate ukweli na kubainisha vizuri ninachokisema.

Mkuu.
Mbona ya Shivji , Mwakyembe na ya ma Proff. Hukuyasema.
Wale wale ambao hamsomi bible nzima, mnarukia viji mistari tu ili kujenga hoja zenu mfu.
By the way Lissu kaongea uongo kwani ?
Mkataba wa Muungano ni lini Serikali ya Kuanzia Nyerere mpaka JK ulipelekwa UN ?
Kuanzia janq binafsi nimeanza kumtizama the late Julius kwa jicho la tatu.
No wonder all the Problems we have now source yake ni yeye.
 
Mimi huwa nadhani wanasheria ni watu wazuri sana katika uwanja wa siasa hasa ukiangalia kwa kutumia darubini katika siasa za nchi za magharibi utakuta kuwa, viongozi wengi wa nchi hizo ni wanasheria na wamefanikiwa/wanafanikiwa katika siasa zao.

Kama hoja yako ni kweli, kwa nini inakuwa tofauti kwa Mh. Tundu Lissu?.

Dunia nzima masuala ya muungano ubabe hutumika...hata marekani hawaruhusu mtu
Ahoji muungano wao sababu ubabe ulituzmika
 
Ndiyo unapotosha tena unajaribu kumingo akili za watu wamuone lisu mtukutu,

-hukusikiliza wala kuisoma hotuba ya Lisu peke yako,


Jitafakali kwa kutumia hekima sisi sio wapuuzi wakukubaliana na propaganda zako kupindisha maneno nakuchomekea neno Nyerere pasipostahili ilikukidhi malengo yako.
Siko hapa kukutaka ukubaliane na kile ninachikiandika. Unaweza ukakubali kutokubaliana lakini hauwezi kuundoa ukweli wa kile Mh. Tundu Lissu alikisema na amekisema kwa ufasaha kabisa.

By the way, hata bila Mh. Tundu lissu kutokuyasema aliyoyasema, kwani ilikuwaje mpaka Alhaji Aboud Jumbe akajikuta yuko nje ya Madaraka?.
 
Tundu Lissu alifata ushauri wangu nilioutoa humu JF 7th April 2014, wiki iliyopita:

Mtaipataje Tanganyika bila kupinga hadharani fikra za Nyerere aliyeiuwa? Inatakiwa kwa dhati kabisa mseme wazi kuwa Nyerere alifanya makosa kuiuwa Tanganyika, hapo mtaeleweka, bila hivyo? itatumika fimbo ya Nyerere na fikra za Nyerere na nyinyi hamuwezi kuukubali ukweli kuwa alikosea. Sijui unafaham?

Leo mnatafuta pakutokea, kila ataekuja na lake mtalitafutia sababu, mara oohh Shivji hivi, mara Oooh Warioba vile, mara Oooh Kikwete vile.

Amkeni na mseme tu Nyerere alifanya makosa makubwa sana kuiuwa Tanganyika, mbona hapo mnapata kigugumizi?

Na bila kukataa fikra za Nyerere kuhusu huu Muungano mtatafuta sana scapegoat.

Sasa mnailaumu Zanzibar ndiyo inawanyima Tanganyika yenu? mimi naona Wazanzibari wanawasaidia sana kwenye hii cause yenu ya kuitafuta Tanganyika lakini nyinyi ndio msiojijuwa muanzie wapi. Upo hapo ulipo? Anzeni kwa kuzipinga fikra za Nyerere kuhusu huu muungano, hiyo ndio shortcut pekee ya kupazia malalamiko yenu. Ukipenda usipende hilo halikwepeki.
 
Ng'wanampalala acha kujenga hoja mfu na kutaka public sympathy, weledi wa Tundu Lissu haufananishwi na wasomi wowote walio ndani ya ccm kwani ni mtu mwenye kwenda na fact na huwa na defending points, rejea hotuba ya mwalimu nyerere kuwa yeye sio malaika na kkuna sehemu yawezekana alikosea aliomba asamehewe, na kushauri watu wafate mazuri aliyoyafanya na sio mabaya aliyoyafanya, Sasa kuna wavivu wa kufikiri mnaleta tafsiri za kupotosha, h
 
JULIUS NYERERE-Humanist,Politician ,and Thinker.-POLE SANA TUNDU LISU,HUNA HADHI YA KUMKEJELI BABA WA TAIFA,JIKITE KATIKA KUJENGA HOJA ZAKO TU,UTAELEWEKA.
 
Mkuu, nani amesema hapa kuwa Mwl. Nyerere hakuwa mwanadamu?.

Tukubalianemtu kuwa, Mh. Tundu Lissu amepasua jipu ambalo wengi waliogopa na wanaendelea kuogopa kulipasua. Kwa lugha inayoeleweka na wengi, amemchana chana Mwl. Nyerere na pamoja na kitabu chake cha Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania.

Naam, ziliondokea falme zilizotisha kuliko simba leo ziko wapi? Wengi waliuwawa, walipotezwa, walidhalilishwa, na kufanyiwa kila aina ya vitimbi na mateso ya aibu; ziko wapi falme zile? Nyakati zetu hizi nani wa kumfananisha na Babeli? Au nani mfano wa Rumi? Nani kama Ottoman? Ziko wapi leo falme hizi? Eti tutatawala milele!

Ni Mola peke yake ndiye hutawala milele enyi wapumbavu! Hakika kufuru zenu zimemfikia aliye Mtakatifu na amegeuka kuwatazama waja wake! Mtashindana naye? Mtashindana na Mkono wake ulio hodari?

Vizazi havina kumbukumbu zozote za aliye Mtakatifu kushindwa katika alitakalo. Hakika mtapotea wala hamtakumbukwa tena msipojirekebisha na kulegeza shingo zenu ngumu mkatambua mamlaka hutoka kwake. Mtatawala milele!? Kufuru ya ajabu hii!
 
Tundu Lissu ni smart lawyer na very good mwanaharakati but he is a lousy politician....huwezi mtukana Nyerere na isi ku cost

Wewe tokea Jamaa yako awe Mbunge wa Mahakama umekuwa hovyo kabisa na inaonesha umepatwa na msongo wa mawazo kabisa.
Wewe ni mfano wa watu ambao wanatenda based on interpretation ya akili za watu wengine.
 
Huyu Lissu ni mropokaji, bila Mwalimu Nyerere ajiulize leoangekuwa wapina anafanya nini? Hata afanye nini hawezi kubadili historia ya Mwalimu Nyerere katika Taifa na Dunia kwa ujumla.
 
Ndiyo unapotosha tena unajaribu kumingo akili za watu wamuone lisu mtukutu,

-hukusikiliza wala kuisoma hotuba ya Lisu peke yako,


Jitafakali kwa kutumia hekima sisi sio wapuuzi wakukubaliana na propaganda zako kupindisha maneno nakuchomekea neno Nyerere pasipostahili ilikukidhi malengo yako.


Alichoandika mleta mada yupo sahihi, nina mashaka na wewe unayetaka kumpinga kama kweli uliuona uwasilishaji wa hoja za Tundu Lissu. Na kama ulitazamana basi nachelea kusema kuwa uwezo wako wa kuelewa ni mdogo sana.
Ila una nafasi pia ya kusoma magazeti ya leo na thread nyingine hapa JF zinaweza kukufumbua.
 
nyerere ndio role model wa dr.slaa, mbowe , yericko nyerere,bensaanane halafu tundu lisu anamtukana.. lisu hana adabu kwa viongozi wake wa chama

We naye viroba tayari vimeyumbisha akili yako ni wapi Lisu katukana? Kama ulikuwa hufahamu, basi kuanzia leo unatakiwa kujua Nyerere kafanya mengi mazuri na vilevile kuna machache aliboronga likiwemo suala la Muungano so hamna ubaya wowote akina Mbowe kufuata mazuri aliyofanyia Taifa eti kisa kuna mabaya machache alifanya.
 
Back
Top Bottom