figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,754
- 56,082
Catherine Ruge ni mmoja ya Kikundi cha ndani ya CHADEMA cha G55 chenye Malengo ya kukwamisha Kampeni ya no reforms no Election. Pia wanadaiwa kuhujumu au kuangusha Uongozi uliopo madaraka chini ya Tundu Lissu.
Kundi hilo linadaiwa kudhaminiwa na Freeman Mbowe aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA kwa madhumuni ya kuonesha Umma kwamba Tunddu Lissu na Uongozi wake haukubaliki. Wengine walio kwenye hilo kundi la G55 ni John Mrema na Mwita
Operesheni #NoReforms NoElection
inaendelea kuchanja mbuga kanda ya kusini.
Mapema wiki hii Watia nia ya Ubunge mwaka 2025 na waliokuwa watia nia mwaka 2020, (G55) wakiongozwa na Vigogo Adv. John Mallya, Catherine Ruge, John Mrema na Julius Mwita wamechapisha waraka kwenda kwa Katibu Mkuu Chadema, wakieleza kuwa wadau wengi wa Demokrasia nchini hawaungi mkono Mpango wa kuzuia uchaguzi mkuu unaotaka kufanywa na Chama cha Chadema kwani hali hiyo inatafsiriwa na wadau hao kuwa ni sawa na karibu na matendo ya uasi.
Chini kabisa nitaambatanisha Meseji za WhatsApp za G55 Wanaodaiwa kutaka kupindua uongozi uliopo.
Na Hilda Newton Chadema
Mungu fundi sana
Imagine leo story ingekuwa isomeka Katibu Mkuu wa Bawacha Taifa apinga Azimio la Chadema la #NoReformsNoElection.
Mungu awabariki sana Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Bawacha Taifa ni Kama tulikuwa mbele ya muda.😂
Ukipitia orodha ya watu waliosaini petition ya kupinga #NoReformsNoElection wote ni watu ambao kwenye Uchaguzi wetu wa ndani walikuwa wanamuunga mkono Mhe. Mbowe.
Wengine ni Wajumbe wenzangu wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu wa Chama Taifa wakati tunapitisha hili Azimio la #NoReformsNoElection chini ya Mwenyekiti Mbowe na wao walipiga kura ya Ndiyooo tena kwa sauti kubwa sana.
Sasa hivi baada ya Mhe. Lissu kuwa Mwenyekiti wale wale waliopitisha Azimio hili kwenye Vikao halali sasa wametoka dharani kulipinga.
Nakumbuka siku tunapitisha Azimio hili cha Baraza Kuu na Mkutano Mkuu wa Januari 2025 kwenye Kikao Mhe. Mbowe aliuliza kuna mtu yeyote mwenye maoni au swali lolote kwenye Azimio hili wote tulinyamaza Kimya kuonyesha kwamba tunaunga mkono.
Najiuliza, haya maswali ambayo wanauliza leo kwanini hawakumuuliza Mwenyekiti Mbowe wakati anaendesha kikao kilichopitisha Azimio hili?
Au walipitisha hili Azimio kwasababu walijua Mhe. Mbowe angeshinda asingetekeleza.?
Mwisho, Kama wao kiu yao ni kushiriki Uchaguzi kwanini wasiende kujiunga na akina NCCR ambao mawazo yao na wao yanafanana ili wapewe nafasi ya kugombea huo ubunge watimize hiyo kiu yao ya kuwagombea bila Reforms?