Tunataka wawekezaji, mara wanyang'anyeni leseni!

Wafuasi wa upinzani nawashangaa sana, yaani wananchi bariadi nzima wakose maji kwaajiri ya muwejezaji? ? Siyo serikali hii kama hampendi hamieni nchi jirani sisi tunaendelea mbele.
 
Huyo jamaa kalipa fidia ya mabilioni kwa wananchi kuchukua maeneo,kafanya exploration kwa mabilioni ya shilingi,kaweka wafanyakazi,kaagiza mitambo

Tujiandae kulipa fidia ya mabilioni,escrow na IPTL inaikumba nchi,tutalipa fidia GEITA na huko ngasamo na kwingine

Fidia mpaka sasa itafika trilioni kadhaa ikijumuisha loss of profit and business

Pia wakienda mahakamani tutashindwa na kuwafidia na eneo kubaki lao

Hawajapewa hata haki ya kusikilizwa kabla ya kunyanganywa,kesi rahisi sana kuishinda

Unajifanya kuwapenda wananchi halafu unawatwisha zigo la fidia!!!
Mkuu wawekezaji wengi hukopa kwenye mabenki sasa najiuliza mtu aliyepewa leseni kafanya exploration ina maana huo mkopo ataurudisha vipi naona tunajiweka kwenye hatari kushitakiwa na kulipa pesa nyingi zaidi
 
Leo Simiyu JPM kaagiza mwekezaji wa madini abatilishiwe kibali ,uuwi,eti tu kwakuwa tenki la maji linapaswa kukaa kwenye kilima,kwani tenki likikaa hapo ni mpaka mbatilishe hati?
 
Wafuasi wa upinzani nawashangaa sana, yaani wananchi bariadi nzima wakose maji kwaajiri ya muwejezaji? ? Siyo serikali hii kama hampendi hamieni nchi jirani sisi tunaendelea mbele.
Kwanini sasa mlimpa eneo hilo?
 
Kauli za taasisi ya urasis ni kama sheria.Kutengua hadi yeye aliyetoa, halafu anaona aibu kutengua Angalieni hizo hotuba ebo?
 
Fikirini kabla ya kuandika upuuzi.Wananchi kwanza.Mwekezaji ni nini kwa uhai wa wananchi wa tz?Water for life,not nikel for life.Think a bit you simple minded.
Mlivyokuwa mnampa hilo eneo Muwekezaji hamkujua kama kuna wanachi wanahitaji Maji?
 
Moja ya vitu vinanishangaza kwenye Utawala huu wa Magufuli, yupo Mbele saana kwamba tunahitaji Wawekezaji wa Ndani na Nje, sasa linapokuja swala la Kuwaambia tena waondoke ndipo nachoka sasa.

Juzi juzi kasema Wawekezaji waliopo huko kanda ya Ziwa (Homeland) wasiwasumbue Wananchi. Leo tena Bariadi kasema muwekezaji eneo ambalo ndipo linatakiwa lijengwe Tank la Maji kuwa kama vipi wamnyang'anye lesseni yake. Maeneo hayo mlipokuwa mnagawa hamkujua kuwa patatakiwa papitishwe nini.

Cha kujiuliza, sasa hawa wawekezaji wana kosa lipi maana wapo eneo husika kihalali. Pia, yeye anahamasisha ama kuwakaribisha wawekezaji halafu baadaye mnawageuka sijui tuwaelewaje sasa. Mwishowe wataona Serikali yako haiamiki na hawatakuja tena kuwekeza

Kumbuka hautaishia hilo, pia mtaingia hata kwenye viwanda unavyovisema nchi ndiko inaelekea. Na haya ni madhara ya kufanya hotuba ambazo zinatoka kichwani moja kwa moja bila kuhaririwa na mtu huna karama hiyo.

Hapo ulipo Mkulu nawewe Utapita tu.

Lazima tuwe na uwezo wa ku way things...Hakuna hesabu za 1+1 katika maisha ya mwanadamu...Kwamfano wewe ni Rais wilaya tatu hazina maji na watu kadhaa wanakufa kwakukosa maji...hawawezi kuishi kwakua maji ni uhai...Kati ya mwekezaji wa nikel ambaye kwanza formular ya calculation is almost haijulikani kwakua wanakuja na hadithi za ku register loss ungamua nini? Hajakataa uwekezaji na wala hajamaanisha hataki wawekezaji lakini kuna prorities in life, kwahiyo kati ya maisha ya watu 1.something milions population kukosa maji kisha tuchimbe madini hiyo reasoning nadhani inahitaji scrutiny... Rais ame challenge technology inayotumiwa...Tunafahamu nchi kama Norway barabara zimechongwa katikati ya milima bila kung'oa mti hata mmoja...Huyo investor kwanini asiangalie uwezekano wa ku exploit hiyo resoirce huku akipunguza social costs? Hivi EMA, 2005 tuliipitisha kama pambo? Hapo EIA experts kama hawakuweka hizo social costs basi Rais wa nchi katumia common sense tu kuona the project cannot out compete the pressing needs za immediate population ambao wanakosa maisha...life without water...Hizo costs za wananchi wanaokufa wamezi factor in?
 
Back
Top Bottom