Tunapinga na kulaani mawazo ya Waberoya kurahisisha mauaji ya ‘akina Bashe ‘

Hivi mauaji ya Rwanda yalianzaje? Nafikiri in hivi hivi. MTU mmoja aliuawa jamii nzima ikaamua kulipiza kisasi. Haijalishi aliuwawa namna gani
Hawa hawaelewi ni kwa kiasi gani wanapandikiza chuki
 
Ila wakuu ki ukweli mnaharibu jukwaa, sijawa mkubwa kihivyo mkuu, mpaka unanipa kiki ya kunianzishia thread! seriously?

Halafu watanzania wengi kama kawaida yenu mnakimbilia kuhukumu na wala hamjaiona hiyo post!! aisee!!

hata sikumbuki post hipi na wapi nimeandika hilo swala

hili twende sawa unaweza kuiweka hiyo post?
 
Waberoya team Bashite, anatoa vibanzi kwenye macho ya akina Bashe lakini Boriti kwenye Kengeza la Bashite halioni!!!

mzee mkubwa kama wewe ungeomba kuiona hiyo post

halafu usisahau hii ni debate club!! usiwaze kuwa lazima watu watakuwa upande wako

kuna wengine hatuna hayo mateam na wala hatuna mauchungu

siwezi kumlaumu mtu nisiyemjua

ungeomba post mkuu!! utakuja kuua mtoto wako kwa ya kusikia tu

angalia mantiki
 
Ila wakuu ki ukweli mnaharibu jukwaa, sijawa mkubwa kihivyo mkuu, mpaka unanipa kiki ya kunianzishia thread! seriously?

Halafu watanzania wengi kama kawaida yenu mnakimbilia kuhukumu na wala hamjaiona hiyo post!! aisee!!

hata sikumbuki post hipi na wapi nimeandika hilo swala

hili twende sawa unaweza kuiweka hiyo post?
Hata kama ni mdogo kama piriton, mawazo yakiwa ya kifashisti tutayapinga na kuyalaani. Ndiyo yanayosambaa na kuharibu nchi, tutawamulika popote na kwa staili yoyote mnayotoka nayo.
 
Rais ashitakiwe kwa Makosa anayofanya akiwa madarakani nafikiri hapo ndo Tunaweza kueheshimiana
 
Nimepigwa na butwaa kubwa kuona mawazo ya Waberoya ya kwamba kumuua mtu nchini Tanzania ni rahisi sana, na kwamba haihitaji kumteka mtu kama Bashe ili kukamilisha mpango wa mauaji.

Mawazo haya ni mabaya sana, ya hatari sana na ya kigaidi yanayostahili kupingwa kwa nguvu zote kwa sababu uhai wa binadamu ni kitu kilichotukuka. Uhai wa binadamu ni sacred (ni kitu kitakatifu) yaani ni kitu cha kuheshimiwa sana. Kurahisisha mauaji ni mawazo ya ki-barbaric (kishenzi na kisheteni).

Ni mawazo ya kutaka kutisha watu kutetea nchi yetu na ni mawazo ya kuwatia kiburi watawala wenye mawazo kama ya Waberoya. Tangu kuubwa kwa ulimwengu, uhai wa binadamu ni kitu cha thamani kubwa.

Ni zawadi ya pekee ambayo binadamu tunaipata kutoka kwa Mungu. Hakuna mtu amewahi kumuumba binadamu. Ndiyo maana suala la kuua haliwezi kuwa rahisi.

Mtu mwenye mawazo ya kurahisisha mauaji si wa kawaida, aweza kuwa ni kichaa au mpumbavu kupita maelezo. Mawazo ya kurahisisha mauaji ni ya kigaidi.

Hata kama unamchukia mtu kupita kiasi, haijawa kitu rahisi kuua. Ndiyo maana wauaji hupanga njama ili wasijulikane kuwa wametekeleza kitu hicho. Ndiyo maana hata sasa kuna mjadala usiyokwisha kuhusu hukumu ya kifo.

Kuua si kitu rahisi na hata majaji wanaotoa hukumu ya kifo hawaitoi kirahisi kama Waberoya anavyofikiria. Kuna simulizi nyingi zinazoeleza kuwa hata mtu anapofanikiwa kumuua mtu kwa siri dhamira humuandama mpaka anajisema mwenyewe. Damu ya mtu isiyo na hatia inawaandama wauaji, inagharama kubwa kwa wauaji.

Bashe ni mtu aweye yoyote ni binadamu ambaye uhai wake unathamani isiyomithilika, na hivyo mauaji ya mtu hayawezi kamwe kuwa kitu rahisi. Hivyo wananchi tunaoheshimu uhai wa binadamu tuungane, tupinge na tulaani mawazo ya kurahisisha mauaji ya watu wa aina ya Waberoya.

Mkuu acha kunichafua na kuniharibia, siku zingine unaweza hata kumPm Mtu kutaka clarifications badala ya kuandika post ndeeefu mtu achukiwe

sasa naomba uweke post hapa na kisha highlight sentensi niliposema kuua mtu ni rahis

weka ushahidi hapa na usipoweka nashtaki kwa mods kwa kunichafua nakupa masaa kumi ya kuuthibitishia umma na hao waliolike kukuthibitishia umeelewa wrong

na usichokijua mkuu mimi ni mpinzani mzuri tu!!

kama itathibitika nimemaanisha hivyo ulivyoelewa, then nitataka uniadhibu
 
Hata kama ni mdogo kama piriton, mawazo yakiwa ya kifashisti tutayapinga na kuyalaani. Ndiyo yanayosambaa na kuharibu nchi, tutawamulika popote na kwa staili yoyote mnayotoka nayo.

mkuu weka post acha kulia kulia, unajua nikibadilika nitakuchamba Gwajima anasingiziwa, yaani nakuvua nguo zote

weka post nzima hapa, ni muda mzuri pia wa kujua aina ya watanzania tulionao

weka post
 
mkuu weka post acha kulia kulia, unajua nikibadilika nitakuchamba Gwajima anasingiziwa, yaani nakuvua nguo zote

weka post nzima hapa, ni muda mzuri pia wa kujua aina ya watanzania tulionao

weka post
Usijifanye msahaulifu kama kuku. Kasome uzi wako uliomuongelea Bashe.
 
Ujumbe nilioupata kwenye ile thread ya huyo jamaa ni kwamba hata YEYE anaweza kufanya hayo mambo ya kishenzi ya kuteka na kuuwa.
Na Alaaniwe Milele.

kesho utaambiwa nimetembea na mama yako mzazi halafu utaanza kuniita baba

mwambie akuonyeshe post

utaolewa unajua
 
Usijifanye msahaulifu kama kuku. Kasome uzi wako uliomuongelea Bashe.

mkuu wasaidie watu ambao hawajui huo uzi uko wapi, weka link ya post

inakuchukua muda gani?

aisee

au na wewe ni wale watekaji ambao tumewagundua? mpuuzi wewe sasa unaanzisha thread ya nin? kama hauna uthibitisho

weka post hapa
 
Kama haujui uzi ulioleta mwenyewe, wewe ni wa ajabu sana.
 
weka post yangu
Haya ni maneno yako ya kifedhuli kwenye uzi ulioleta, nanukuu "hivi BASHE inachukua dakika ngapi wewe kuuawa?? nchi hii hata rais hana ulinzi wa kutisha wa kushindwa kuuawa, mabenki yetu hayana ulinzi wa kutisha kushindwa kuingiliwa!! Bashe mtu akitaka kukuua na kadhamiria unaweza kuuawa na wala hana muda wa kupoteza kukuteka!!" . Mwisho wa kunukuu
 
Hao wanaouliwa wanafamilia na ndugu uchungu wanaoupata mungu ndoanajua ila anaona rahisi kwavile hajamkuta mngese sana hawa wa bunge wa ccm ivi hao wanaowachagua kwenye majimbo wanaakili ya aina gani? Nimeapa sita mchagua m'bunge wa ccm wala rais anaetokana na ccm hata wapinzani wakiweka jiwe nitalipigia kura kuliko kupigia ccm
 
Back
Top Bottom