Tunaitaka Tanganyika yetu! Wakati ni huu...

Manyani Walimuua mchungaji mtikila..kuna kitu ccm wanaficha watanzania huu muungano ni feki..tunahitaji Tanganyika yetu..laa kuwe na serikali moja kuliko huu upuuzi uliopo sasa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mpendwa Tanganyika ni miongo sita na mwaka mmoja sasa tangu ujipatie uhuru wako kutoka kwa wakoloni wa magharibi ambao waliyumbisha maisha yako na kukupiga danadana kama mpira.

Hao sio wengine bali ni Ujerumani walioanza bada ya mkutano wa Berlin na baadaye kwa ulafi wao wa kugombani kile ambacho sio chao ukajikuta unaangukia mikononi mwa ukoloni wa Waingereza.

Nafurahi kufikia umri huo kwa sababu bado unakumbukwa na baadhi ya watu watu wachache wenye uzalendo wa kulienzi na kulitangaza jina lako japo wengine wamekusahau na kukuita Bara.

Nasikitishwa na baadhi ya watu waliojivisha sura ya mkoloni mweusi kwa makusudi na kulipiga kisogo jina lako halisia. Juu ya majukwaa na mbele ya vyombo vya habari wanakuita Tanzania Bara badala ya Tanganyika tofauti na mwenzako Zanzibar.

Nafahamu imelazimishwa hivyo baada ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar Januari 12, 1964 na muungano wetu bora wa Aprili 26,1964 uliokukubebesha picha kubwa ya Muungano na kukupa jina la Bara.

Mpendwa Tanganyika, kumbukizi hii ya uhuru wako ikawe chachu ya kuwakumbusha Watanzania wote kuwa wewe ni Tanganyika sehemu ya Tanzania na ungependa kujulikana hivyo kama mwenzako Zanzibar anavyofahamika ndani ya Jamhuri na nje ya mipaka ya Muungano wa Tanzania.

Yamkini ungefurahi zaidi kama katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sura ya kwanza na sehemu ya kwanza inayoelezea 'Jamhuri ya Muungano na watu', kipengele cha 2 (1) ikasomeka kuwa 'Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Tanganyika na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo'.

Hali hiyo ingeleta ladha tamu badala ya kusomeka vile ilivyo sasa "Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo".

Kama inavyosisitiza sheria ya 1984 namba 15, ibara 6 (1) "Kila mtu ana wajibu wa kufuata na kutii Katiba hii na sheria za Jamhuri ya Muungano". Lakini pia ibara ya 6 (2) "Kila mtu ana haki, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria, kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba na sheria za nchi".

Basi leo tukiwa tunatimiza miaka 61 ya uhuru wa Tanganyika ni vyema haki na utaratibu wa sheria ukatumika kutafuta namna bora ya kurejesha uhai wa Tanganyika. Hali kadhalika ni vyema sana ikaeleweka kuwa 'tunalazimika kuita Tanzania Bara kama tutatumia jina Tanzania Visiwani na Tanzania Tanganyika tukitumia Tanzania Zanzibar'. Pande zote kwa usawa na usawa kwa pande zote.

Inasadifu kusema na kuitamka Tanganyika kwa kuwa huo ndio uhalisia wake na hakuna litakaloharibika bali inakuwa ni kuongeza kiini cha chimbuko la ndugu wawili walioungana na kuiiunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa maana hiyo leo basi tuna kila sababu ya kuiimba na kucheza “Happy Birthday to You” Tanganyika.

#kitabukinakurasanyingi

Mwisho.

✍🏾 Tanganyika Leo

20221208_114517.jpg
 
Back
Top Bottom