Tunahusika na uzalishaji, ufugaji, ufundishaji na uuzaji wa mbwa

kingz_dawgz

Member
Oct 28, 2018
9
11
Tunahusika na uzalishaji, ufugaji, ufundishaji na uuzaji wa mbwa waliosajiliwa na wenye viwango vya juu kwa ajili ya ulinzi binafsi, majumbani na maeneo mengine. Tunafundisha na kumfanya mbwa kuwa siraha, mlinzi na rafiki.

Pia tunatoa ushauri wa kitaalamu juu ya ufugaji bora na ufundishaji wa mbwa wa ulinzi.

Mbwa tunaonazalisha, kufundisha na kuuza ni pamoja na;

1.Rottweillers
2.American Pitbull terriers
3.German Sherperd
4.Boerboel

Tupo Bwiru, Mkoani Mwanza. Karibu na kennel ya kampuni ya ulinzi KK Security.

Kwa mawasiliano;
Simu & Instagram; +255745791975
e-mail; kingsdawgz@gmail.com

BEI ZETU NI NAFUU KARIBU SANA UJIONEE UBORA NA UTOFAUTI

images%20(9).jpeg
drawn-pit-bull-muscular-pitbull-562574-5676569.jpeg
20181119_223518.jpeg
Boerboel1.jpeg
 
Hapa tutajaza kurasa, nashauri utembelee page zetu mkuu hasa kwenye Instagram (kings_dawgz) utajionea mwenyewe, au nichek whatsapp..+255745791975View attachment 939978
Mi stitumii social network yoyote mkuu, si Instagram wal FB wala nini.... wewe kua huru mwaga picha, uzi umeanzisha kwaajili hio, naamini utapata wateja wengi tu.

Huyu German mzuri sana, unauzaje wadogo?? Na unao COATED GERMAN SHEPHERD?
 
Aysee we kweli balaa, dunia hii ya leo umeweza kukaa bila kuwa kwenye social network yoyote isipokuwa JF tu, yaani hata whatsApp? utapitwa na mengi kiongozi...

Anyway, puppies wa GSD huwa tunao wenye long coat na shot coat ( coat =Manyoya), bei ni toafuti...long coat bei yao inakuwa juu kidogo, na puppies tunauza wakiwa na umri wa miezi 3 na kuendelea (umri huu wanakuwa tayari wanaweza kula vizuri na wamenyonya maziwa ya kutosha kwa mama yao), na jinsi umri unavyokuwa na bei inazidi kuongezeka.

Bei ya Puppies kimsingi hutegemea vitu vitatu;
1. Coat yake ( long coat au short coat)
2. Umri wake
3. Training Level.
IMG-20181115-WA0000.jpeg
 
View attachment 940292
Bei zipo vipi;

1) GSD Long Coat Miezi 3??
2) GSD Short Coat Miezi 3??

3) Rott miezi mitatu??
 
1. Kuamua kufuga mbwa.
Hakikisha unania madhubuti ya kufuga mbwa, kumbuka mbwa anahitaji kupendwa, mafunzo, matunzo na hasa mazoezi, hivyo ni inapaswa uwe na muda na pia uwezo wa kusimamia hayo.

2. Kutafuta mbwa/puppy.
Unaweza kutafuta mbwa mtaani ukammiliki au ukanunua kutoka kwa mzalishaji wa mbwa mfano King Dawgz. Muhimu kuzingatia km unachukua mbwa mtaani hakikisha;
a) umejiridhisha hana mmiliki
b) unampeleka kwa daktari wa mifugo kwa ajili ya uchunguzi wa afya, kinga na tiba.
Pia kama unachukua mbwa kutoka kwa mzalishaji hakikisha;
a) mzalishaji anazingatia kanuni za ufugaji wa mbwa na afya za mbwa wake b) mbwa amepatiwa chanjo zote muhimu na ionyeshe kwenye kadi yenye mhuri wa daktari wa mifugo, hizi ni kadi wa wazizi na watoto.
b) chukua mbwa angalau akiwa na umri wa miezi mitatu au zaidi.

3. Kuchagua mbwa.
Fikiria aina ya mbwa unaependa, fanya utafiti. Chagu Mbwa/ puppy aliyechangamka na mwenye afya bora, angalia usafi wake, angalia tabia yake. Je anakimbia watu? Je ni mlegevu? Je anauzito sawa? Je anakuja ukimwita? Hii ni muhimu sana.

4.Chagua jina la mbwa wako.
Jina ni mhimu hasa kwenye mawasiliano na mafunzo, Jina liwe fupi na lenye mkazo mwishoni mfn. "Buster" "Max" "Buddy" "Simba" n.k hii humsaidia mbwa kulishika jina lake kwa wepesi na kuepuka kuchanganya pili unapomwita, mbwa ambaye tiari ana jina unaweza kulibadili kwa kumfundisha jina jipya, hii huhitaji muda kidogo ( nitaelekeza kwenye makala ya mafunzo)

5. Tenga sehemu ya makazi.
Makazi ya mbwa yawe safi na salama, hii huweza kuwa banda, chumba n.k. hakikisha kuna nafasi ya kutosha kwa mbwa kusimama, kulala na kugeuka, pia iwe safi na yenye hewa, hakikisha hakuna vumbi wala unyevu nyevu. Unaweza ongeza tambaa zito safi au blanket kwa ajili ya puppu. sehemu hii itumiwe na mbwa kwa ajili ya kumpuzika na kulala.

6. Fikiria juu ya "sheria za nyumbani." kabla ya kumleta mbwa, chagua kile anachoweza na asichoweza kufanya. Je, anaruhusiwa kupanda kitandani au juu ya viti? Je! Sehemu ipi hapaswi kufika, mfn jikoni. Sheria hizi zifuatwe mara tu mbwa afikishwapo nyumbani.

Tutaendelea hatua ya 7 mpaka 10

Instagram; King_dawgz
+255745791975
FB_IMG_1537109298185.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom