Tumshukuru Mungu kutuepusha na Dr. Slaa

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,820
117,368
Mara ya mwisho anajitoa ukamanda aliahidi kuwa pamoja na yote,atakuwa bega kwa bega kuwatetea!!!

IJapo hakueleza bayana ila ilitasfiriwa kuwa ataendelea kukemea yote ya ovyo,...Siku 100 za ubabaishaji zimeshuhudiwa,Mzalendo huyu yuko kimya kana kwamba kupitia Magufuli watanzania ni kama wapo peponi.

Hata ya Zanzibar jamaa hayaoni,ni kama yanatokea nchi za mbali.

Ikumbukwe kuwa Dr.Slaa ni muhanga wa kupokonywa ushindi na CCM,kwa maneno yake 2010 alishinda!

Ameshindwa hata kukemea tu licha ya kutaka Maalim Seif apatiwe ushindi wake!Maneno ya Zito Kabwe yanasema kweli...usimwamini mwanasiasa.
 
Mkuu msamehe bure, unadhani kama mkeo/mchumba wako katoa hati ya nyumba kumpa mtu bila wewe kujua akakopee kisha unakuja shtuka bank wameiuza na mkeo/mchumba hata mshipa wa fahamu haushtuki ndio kwanza anaandika mitandaoni kuwa "tunasoma magazeti" utaweza kufikiria siasa tena? Tena Dr namsifu ana roho ngumu mwingine tungesikia yuko Segerea ya Marekani baada ya kumvunja mbavu,mguu na ngeu bibie.
 
Hata kama analo la kusema atalisemea wapi wakati ccm wamemtelekeza mkuu wameshindwa hata kukomboa nyumba yake? upande wa pili anajua wazi hawezi kupongezwa chochote na chadema kwa kuwa ule muda aliotusaliti ulikuwa ni muda ambao chama kilihitaji ushirikiano wa nguvu kuliko kipindi chochote, any way hajiamini ndio maana kaamua kukaa huko alipo, mbona Lipumba yuko nchi fresh na maisha yake yanaenda poa tu. Acha aonje ladha ya ukimbizi ndio kitu alicho bakiza kwenye maisha yake, alishakuw padri, mume, raia huru, baba watoto, mwanasiasa mashuhuri, naona anataka awe na hili la ukimbizi pia kwenye cv. yake.
 
Mjadala wake ulishafungwa,yule hata akiongea nn tunampotezea tu,hana cha maana.
 

Mi nadhani shukrani kubwa iwe ya kumwepuka Lowassa.
 
Dr Slaa ndio kiboko ya Nyumbu because.

1.Tokea aondoke chadema hawaoni Wa kuziba nafasi yake

2. Yote aliyowatabilia yametimia MF kujinyea na kutokuingia ikulu

3. Tokea aondoke, chadema imepoteza dira. Leo ndio chama kinachotetea ufisadi.
 
Dr Slaa ndio kiboko ya Nyumbu because.

1.Tokea aondoke chadema hawaoni Wa kuziba nafasi yake

2. Yote aliyowatabilia yametimia MF kujinyea na kutokuingia ikulu

3. Tokea aondoke, chadema imepoteza dira. Leo ndio chama kinachotetea ufisadi.
Anenayo mtu ndio yameujaza moyo wake, una chuki sana na hiyo ita kuumiza, nani alijinyea? ushahidi unao, nafasi yake imeshindikana kujazwa kwenye uchaguzi upi ambao umefanyika akakosekana mtu, kutokuingia ikulu imeshindikana? kwana dunia imeisha tayari hapa tunajadili tukiwa ahera? Ndugu akiba ya maneno, dunia ipo maisha yapo yanaendelea.
 
Atakuwa anakumbuka sana pale alipoambiwa na askofu wake kwa lugha ya kilatini " CUSTODISTI IUSIURANDUM, TUI PASCUNT OVES. ( Tunza kiapo chako, lisha kondoo wako )
 
MSHUKURU DR. SLAA YULE JAMAA SIO RAIS, alitueleza ukweli na watanzania TUKAMSIKIA kwa uzalendo wake uliotukuka. Yeye na Polepole wanastahili HESHIMA. Leo Dr. Magufuli ni rais kiasi fulani sababu ya mchango wao.
P.s: Sijui nitakula BAN hapa? Dah! Fingaz crossed!
 
Kwa waliosoma"Things fall apart" wanaweza kumfananisha na shujaa Okwonko aliyeishia kwa kifo cha kujinyonga - abomination!!!
 

Hamna cha Ban.
Umeongea la maana na ukweli mtupu.
Asie penda akalale.
 
ukiwa muongo kumbuka kuweka kumbukumbu,alianza kusaliti chama chake slaa hata kabla hakijamkaribisha lowassa,mambo mengine kama hanjui bora tu kunyamaza mnatia aibi
 
inatia aibu kwa cdm bungeni kunyoshewa kidole bungeni na ccm sbb yaufisadi.wapi cdm inayotetea maslah ya taifa?cdm imekuwa sacos ya mtei,luwasa ndyo kanunua sacos kwakuweka hisa kubwa.tunahitaji mbadala ya cdm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…