DOKEZO Tume ya Madini, huyu RMO wa Kahama sidhani kama anatosha!

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Tuhuma za RMO Kahama
1- Anamtetea shemeji yake, ambaye anatuhumiwa kupunguza purity kwenye soko kuu la Dhahabu Kahama, tuhuma hizo kuhusu shemeji wa Kumburu zimefikishwa hadi ofisi ya DSO KHM & Task Force, lakini amekuwa akitengeneza mazingira ya kumlinda, taarifa zinaonyesha anafaidika na wizi unaofanywa Shemeji ake huyo ambaye amekuwa akisema RMO KHM ndiye aliyesema akae Kwenye mizani na hawezi kutoka.

2- RMO KHM Amekuwa akijitengezea mazingira kujinufaisha kutoka Kwenye migogoro na changamoto mbalimbali.

- Moja ya tukio la kujinufaisha ni pale alipokea kiasi cha Tsh milioni 20, ili aweze kufungua mgodi (Ntambarare No:6 ) aliyoufunga baada ya kutokea ajali iliyosabisha kifo, maduara yote Kwenye mgodi huo yalichangishwa fedha ili RMO KHM alipwe kiasi hicho.

- RMO KHM alishirikiana na mtuhimiwq (Bosi wa Pierre Elution), ambayo ilimuibia udongo mteja ambapo kesi kuhusu wizi huo ulifika polisi, lakini RMO KHM alimdanganya mteja huyo afute kesi kuwa atalipwa fidia na Elution iliyomuibia udongo, lakini PIEREE ELUTION haijamlipa hadi leo, huku RMO KHM akimalizana pembeni na PIERRE ELUTION

- RMO KHM amepokea hongo ya tsh 9M kutoka kwa mama mmoja mmiliki wa duara no: 7A (leseni ya NKANDI GOLD MINE-Mwime) ili amuondoe mmiliki wa duara no: 8A, ili mama huyo amiliki eneo jirani kwakuwa maduara hayo yanavuna mwamba mmoja.

Note: Hayo ni machache ila mengi zaidi ya hayo.
 
Nini kirefu cha RMO? Mwanzo nilidhani unamaanisha Regional Medical Officer.
 
Back
Top Bottom