Tumaini Makene: CHADEMA ni mmiliki wa makao makuu yake

Pango lao si bei kubwa maana hakuna choo wanajihudumu kwa mzee chenge, ni nyumba jirani pale ufipa, nasema nachojua
 
Je Kwa miaka 23 Chadema inalipia Pango?
Fedha hiyo haijatosha kujenga jengo lenye ghorofa 20 kwenda juu?
Fedha hiyo haitoshi kutengeneza madawati shule zote za Kata za Sekondari?
Fedha hiyo haitoshi kuwanunuliwa chakula watoto yatima kwenye makao yao kwa miaka mifano mfululizo?
Kama ndivyo kwanini wasishitakiwe kwa uhujumu uchumi?
Kwani CCM viwanja vya michezo vya kirumba sokoine n.k imevijenga kwa shilingi ngapi?
 
USD 100,000 per month only for a prime area in the city of DSM. The owner is Mr X & Y Limited.
 
Ukiwaambia Chadema wamiliki majengo na viwanja vingi kama CCM ni kuwaonea kulingana na historian ya CCM kuwa chama dola. Zamani kila palipokua na ramani za mji palikua na eneo la CCM kujenga ofisi na uwanja wa mikutano na maeneo ya akiba ya wazi. Kwa hiyo tumeingia kwenye mfumo ya vyama vingi CCM wakiwa na maeneo na ofisi nchi nzima ambayo waliyapata kupitia serikali na sio kwamba waliyanunua. Miaka hiyo ilikua ni rahisi mkuu wa wilaya awe na ofisi ya enzi ya mkoloni lakini CCM iwe na ofisi mpya iliyojengwa kwa hamasa za kiserikali na mwenge.
Nakumbuka zamani tukiwa shule ya msingi tulichanga sh 1 kila mwanafunzi kujenga ofisi za CCM wilaya.

Vijana waliozaliwa miaka ya 1990 wanafikiri CCM ni chama cha maendeleo kilichojijenga. Mpaka leo CCM bado inategemea mbeleko ya Serikali .
Chama chenye rasilimali nyingi lakini bado kinategemea kubebwa na dola kisiasa na kiuchumi na kijamii.CCM ijifunze kuwa chama cha siasa kwani kikitegemea nguvu ya dola siku ikiundwa katiba mpya na tume huru kitapotea kwenye ramani ya kisiasa kama KANU. Kwa sababu sasa hivi kina nafasi kubwa ya kufanya siasa kikiwa bado na nguvu na wabunge wengi na wenyeviti wa serikali za mitaa na madiwani nchi nzima lakini bado kinatumia mbeleko ya vyombo vya dola.


Na viwanja vingi vya michezo wamefanya kuvipora toka mikoani kwenye halimashauri kwa sababu tu ya majina ya wanasiasa waliyokuwa wameyatumia.
Lakini ukweli hawakuvijenga kama chama.

Tujiulize tu kama ingekua ni viwanja walivyojenga wenyewe imekuake Jiji kubwa kama Dar es salaam wasiwe na kiwanja chao cha mpira kama ilivyo Shekhe Aman Abeid Arusha na kwengineko.

Hata hivyo isiwe sababu ya Chadema kukosa ubunifu wa kujenga ofisi zao wenyewe.
Japo najua kabisa Chadema chini ya Mpigaji na Msanii Mbowe hawawezi kamwe kuwa na ofisi za chama na kuacha ujanja wa kupiga pesa za mapango ya kuruka.
 
Back
Top Bottom