Tuliotelekezwa na baba zetu tukutane hapa

Duh inasikitisha sana kuskia jinsi wakina baba wengi walivyotelekeza watoto. Kuna mengi ya kujifunza ktk uzi huu sisi kama vijana na wababa wa leo tusijefanya haya tuliyoyasoma humu. Iwe ni funzo kwetu.
 
Da hii imetufariji wengi unakuta mzee hajawahi kujua umekuaje wala umesomaje lakini baada ya kufanikiwa anaanza kukutafuta na kuomba msaada
 
Kila ninapotaka kujieleza katika huu uzi nashindwa kwa hasira,in short...My dad is full of shit! I hate him to the death,fuc**** you dad! Can't forgive u ..!
 
Sawa kwani nani amekataa kwamba mzazi ataendelea kuwa mzazi!

Kuna ndugu yangu mimi, yeye ndio mkubwa kwenye familia yetu. Kimsingi amehustle kibishi kibishi ila ametoboa bila ya msaada wa ndugu yoyote! katusaidia mimi pamoja na wadogo zangu ila kwa vile ya hiyo hali, ni mkorofi niaje!

Tukiwa kwenye vikao vya kawaida vya kifamilia kauli za kishujaa ni nyingi sana, mara jinsi alivyohustle, ila kikao cha recently pamezuka mtafaruku, huwa anapenda kurudia kurudia pesa alizotumia kutusomesha, baba na mama wapo wamekaa kimya, ila maneno aliyoyatoa dada yangu yakamshinda, akamwambia im fed up with u duuuh!

Nikasema kimoyo mama yangu mbona huu mtihani! Akaendelea kuongea kwa ghadhabu hivi bila mimi kukusomesha ungekuwa nani wewe! Hapa nyumbani kuna milioni mia, wazee wamekaa kimya, sis akamjibu mimi usininyanyase kama vipi nikurudishie hela yako jamaa kajibu poa!

Asa baadae akalianzisha na mimi hivi na wewe umekaa tu! Unaruhusu dada yako ajibu hivo ooohooo! Majanga haya, wewe si nimekupa kiasi kadhaa sasa unaona sawa umenirudisha hata mia halafu unaangalia mi sikujibu chochote aaaagh!

Mi nikajiuliza, jamani baba na mama si wapo mbona wamekaa kimya halafu unaruka na mimi! Heee! Ila mmmmh! Mambo ya family ni magumu, sis kashamlipa ila beef beef! Mpaka ngoja niachie hapa. Eeeeheee!

Ila mi nilichojifunza kwenye hili battle of the titans!Ni rahisi sana kumchukia ndugu yako tena kwa kinyongo kuliko kumpenda.
Ina maana unalaumu wazazi kwa kutokusomesha ukasomeshwa na kaka yako? Wazazi waseme nini wakati nao ni sehemu ya utegemezi? Yawezekana baada ya kusaidiwa mmeendelea kuwa tegemezi bila kusaidia wazazi wenu.
 
Ni muhanga tena mkubwa.

Biblia inasema 7x70, hivyo tuwasamehe na tuwaone kama baba zetu japo hawana watlichotufanyia chochote.

2. Kisasi si juu yetu ni juu Bwana acha Bwana apogane nao.hukohuko waliko watakutana na mgalilaya.

Ushauri: Kwa nyie wanaume, tafadhali chondechonde, msiwatenge watoto mnaowazaa hata km mliozaa nao hamwataki kabisa.

Wanaume, inauma kulea mtoto bila baba. Mnawaathiri watoto, kimungu kimaisha, kimapenzi. Mnawafanya wanawake kukosa ujasir na maneno ya kuwaeleza waliowazaa. Mnamfanya mtoto awe na maswali mengi kuhusu huyo mama yake na ww pia baba.

Mwe, nimeumia sana na mada hii. Ila tuwasamehe km nasi Mungu anavyotusamehe makosa na dhambi zetu.
The good thing sijawahi kutumia jina lake toka chekechea mpk chuo kikuu, hapa my mom alicheza kama pele. Simchukii ila I've never been proud of him....i saw him twice in my lifè time......Sijawahi kutumia chake sijui labda wakati nazaliwa.....sijawahi kumuuliza mama what happened na sitowahi ila always naaminigi he had nvr loved me coz hata kama wao watakua walizinguana it had nothing to do with me.....Narudia tena simchukii niieleweka hapo, ila nimejihaidi tu moyoni I wanna make and be a good dad so that my children shall be proud of me......In fact nitaanzisha ukoo wangu jamani mniombee, mi nitakua first generation coz wanangu watatumia surname yangu ya sasa ambayo hai-relate kabisa na babu yao........
Daa,imeniumaaa,nataman mwanangu aje kuwa shujaa kama wewe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom